Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa wakitembelea baadhi ya maeneo ya ukanda maalum wa uwekezaji kwa ajili ya kuuza nje ujulikanao kama Benjamin William mkapa Special Economic Zone huko Mabibo, jijini Dar asubuhi ya leo ambapo Rais Kikwete alifungua rasmi ukanda huo mpya wa uwekezaji



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. YAANI MAWAZO YA MKAPA NI KUUZA NCHI TU.......DUH!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2010

    Hongereni sana viongozi wetu kwa hatua hiyo njema kiuchumi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2010

    Ankal Michuzi naomba ufafanuzi

    Tunapenda pata ufafanuzi juu ya ukanda maalum wa uwekezaji, ni mradi binafsi, wa kitaifa, ubia? kuwekeza katika nini? kwani habari hii haitoi ufafanuzi badala yake inaibua maswali mengi yasiyojibika. Naumba ufafanuzi zaidi Bwana Michuzi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2010

    maendeleo huko bongo ni zero

    watu wana hela hata hawajui cha kuzifanya huyo mjamaa ana mihela sio mchezo alafu bado anaendelea kufungua njia za kujiingizia mihela mingine

    wenzangu namimi masikini wa nchi watabakia kuwa omba omba tu

    kweli bongo ujanja kuwahi jamaa wanakusanya mihela yote ya taifa wanyonge wanabaki kupiga kura tu

    fanyeni basi kila kitongoji mjenge japo nyumba 100 kwajili ya raia wenye hali ngumu wapate maisha bora

    ankal sikufichi roho inauma sana yani nasikia mpaka kulia nchi yangu wana jamii wanateseka hawana pakulala hawana chakula hawana madawa hawapati elimu bora

    huko sirudi na narudia sirudi hata ankal akiwa raisi wa nchi sirudi sirudi sirudi

    mungu ibariki nchi yangu wabariki wana nchi na watokomeze mafisadi

    ankal nakuomba itundike hiyo waione wana jamii wenzangu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2010

    ni nchi chache sana marais walioachiana nafasi kukaa pamoja. mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete
  6. Andoni ZubizaretaMay 17, 2010

    Mdau wa Mon May 17, 07:12:00 PM, sio kosa lako naona somo la EPZ halijakuingia bado ndio maana ukatamka hayo uliyotamka. Afadhali mdau wa Mon May 17, 06:51:00 PM, yeye kakiri kutofahamu na kuomba ufafanuzi. Ni juu ya ankal sasa kusaka information za mradi huo wa EPZ. Kuwa na jina la Mkapa haimaanishi huo ni mradi wake for God' sake! Ankal tusaidie ufafanuzi zaidi kabla watu hawajazidi kupotea maboya. Ni hayo tu.

    Mdau +447404578801

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 17, 2010

    The Benjamin William Mkapa Special Economic Zone (BWM- SEZ) is a Special Economic Zone at Mabibo in Dar es Salaam, Tanzania.

    It is the Government`s initiative of enabling the country to attain semi-industrialization status. It is under the 2020 Mini-Tiger plan which aims to create economic growth at a comparable rate to the Asian Tigers.These are
    Hong Kong,Singapore,South Korea South Korea,Republic of China Taiwan.

    Hi,just to answer those questions above on behalf of Ankal.

    Mtu anayesema kuwa hataki kurudi Tanzania na asirudi aendelee kubeba maboksi na kuwatunza wazee huko,wala hatumuhitaji.Mradi kuitwa jina la Mkapa haiimaanishi kuwa mradi huo ni wake,mbona mnakuwa kama hamjaenda shule?.

    Mdau toka Holland.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 17, 2010

    sasa hii imekaa kaaje? Benjamin William mkapa Special Economic Zone, jamani kwani hiki ni kimatumbi au? si tumeambiwa sasa lugha ni kiswahili? mbona watoaji wa sheria ndio wavunjao sheria?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2010

    Jamani kama mtu hujui kitu bora uulize au unyamaze. Mambo ya kusambaza uvumi bila sababu na kuharibia baadhia ya viongozi majina bila sababu si mzuri.
    Hilo jina limeitwa hivyo kwa kiingereza kwa sababu huu mradi haukuanza leo. Huu mradi nafikiri ulianza 2005/2006 kama sikosei na kwa sababu za kiutendaji/kipesa ndio sababu unakamilika mwaka huu. Huu ni mradi wa kwanza wa aina hiyo na ni wa serikali na uko chini ya hiyo wizara ya biashara (chini ya mheshimiwa mama nagu)
    Lengo lilikuwa kujenga "infrastructures" za maji, umeme, simu, posta ndogo, jengo la utawala, n.k. kisha kuwagawia wawekezaji viwanja (wajasiriamali) ambao ni mtu yeyote si lazima awe mgeni ajenge viwanda vidogo vidogo vinavyotengeneza bidhaa ambazo asilimia kubwa zitauzwa nje ili kuiletea nchi mapato ya fedha za kigeni.
    Swala la kuitwa Benjamin Mkapa hata mimi sijui, ulizeni wizarani au huko EPZ kwenyewe kwa Dr Meru ila muache kumsingizia Mheshimiwa Rais mstaafu kwa mambo ambayo hata hahusiki nayo. Mwacheni apumzike kama alivyosema Kikwete alifanyia nchi mambo mengi mazuri na kama binadamu yeyote hata wewe hakuwa perfect, alifanya makosa pia!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2010

    Mimi sina tatizo wala sitaki kujua ni mradi wa nani wala unausu nini Tatizo langi ni kwamba ni lazima kila kitu kibatizwe majinaya marahisi ?? jamani mimi naomba kujua tu hilo kwani mimi naona ni ulimbukeni na ujinga si airport si viwanja vya mpira si barabara ni majina yao tu sasa ndo nini au ndo wanagawana nchi ??

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 17, 2010

    ankal kama mtu ana hasira za kutowini maisha asimalizie munkal wake huku kwenye blog hata kama huna pesa ya nauli ya kurudi ni bora ukae kimya kuliko kusema hovyo kuhusu tanzania, nyumbani ni nyumbani naipenda nchi yangu na watu wake na iko siku nitarudi
    mdau USA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 17, 2010

    Jamani ni vyema kama hamjui kitu au taarifa si lazima kuchangia.Ni vyema ukapata maelezo ya kina kama unahitaji,inashangaza sometimes kukurupuka kama unasain mikataba ya madini na kuja kuwachafua viongozi wetu kwa mema waliyoyafanya kwa ajili ya watanzania.

    Kwa taarifa; Wazo la mradi huo lilitolewa na Mh.Mkapa, na shughuli za mradi huo zilianza mwaka 2005 wakati huo nikiwa UDSM (mabibo hostel)ana kama nakumbuka vyema hilo eneo lilikuwa ni la radio Tanzania,tuliitumia njia hiyo wakati tunaenda Kanisani-Makuburi.
    Hii ni moja ya project iliyoanza katika uongozi wa Mh.Mkapa ukiacha zingine ambazo bado hazijakamilia.Mradi huu umegharimu kiasi cha bil.30 za Ki-tz na kinategemea kuajiri wafanyakazi 4,500. Lengo likiwa ni kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa nje ya nchi na kuiongezea Serikali fedha za kigeni. Sioni kama ni tatizo kama jina La Mkapa likitumika na isitoshe jina hilo halijaanza leo ni toka hiyo project inaanza, kwa nini msihoji toka siku za mwanzo?
    Binafsi naona kama ni heshima kwa Mh.Mkapa kumuenzi kwa jina hilo na isitoshe hata jina la Uwanja Mpya ilistahili pia lipewe jina lake.

    Watanzania tubadilike sio kila kitu kuponda tu. Natumaini wadau walioponda hapo juu watakuwa wamepata taarifa kwa kuanzia!

    Mkapa oyeee!

    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 17, 2010

    Huo mradi ungeitwa tu Tanzania Special Economic Zone kwa vile unalenga masoko ya nje, unless wenye busara zao wameona jina la Mkapa lina umaarufu mkubwa kuliko Tanzania kwa manufaa ya Watanzania wote.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 18, 2010

    We anony wa saa 17:07:12:00pm umedata kweli! nahisi ulikuwa umelala ukakurupuka tu kutoa maoni! Inaelekea huwa hujali unaandika nn! Asante mdau Andoni Zubizareta kwa kumuelewesha huyo mdau mtumwa wa nchi za watu! yy kila kitu kifanywacho na viongozi wa nchi yake hata bila ya kuelewa anakuwa na mawazo negative tu! mijitu mingine bwana! eti ooh bongo sirudi! kaa huko uliko! wewe kwanza inaelekea ulitoka bongo miaka 10 au zaidi iliyopita! hujaiona bongo ya sasa inafananaje! pia yaelekea hata makaratasi huna! nauli yenyewe yaelekea tatizo kwako! Me pia nipo nje lkn naimiss bongo ile kinoma! Naipenda nchi yangu! Kurudi TZ Mungu akinipa uhai ni lazima! wadau tujifunze kuuliza unapoona kitu hukijui! siyo unakuja kuchafua hali ya hewa humu kwa ze fulazzzz!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 18, 2010

    AllAfrica.com recently had a good piece explaining pros and cons of EPZ http://allafrica.com/stories/201005130221.html

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 18, 2010

    we mdau wa Mon May 17, 11:27:00 PM, unachekesha kweli. Sasa ukiitwa Tanzania SEZ....kama wana mpango wa kila mkoa kuwa na eneo ka hilo moja au zaidi yataitwaje? Wewe uwe wazi tu kuwa humpendi mheshimiwa Mkapa hata kwa mazuri aliyofanya.... hata Kikwete, Mwinyi, Nyerere kuna mazuri na mabaya waliyofanya msiwe mnamuonea Mkapa tu!!! Mtu utakumbukwa kwa mazuri!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 18, 2010

    Patamu hapo! "Hawataki" kujadili mradi, wanakomaa na jina!
    Kukaa umangani hakuondoi "uswahili" ndani ya "mswhaili".
    Naogopa kama asingeenda umangani kabisa!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 18, 2010

    EPZ wametuchukulia mashamba yetu Zinga, Bagamoyo... wanachukua jumla ya Ekari 50,000/= sehemu ambazo tumeshajenga, tumeweka Zahanati, shule, umeme, na maisha yanaendelea tunafuga na kulima kwa nguvu zetu huu ni uwekezaji gani? Upande wa pili tu wa barabara ni mapori makubwa kwa nini wasipewe mapori wayasafishe, waweke barabara, maji na kuleta maendeleo kihivyo badala ya kutufukuza walala hoi tuliosave hela zetu na kununua ardhi kutengeneza maisha yetu.

    Anayekunyang'anya Aridhi, Amekuua.

    Ndio nimejua sasa kwamba anayekunyang'anya Ardhi Amekuua maana matumaini yako yote ameyachukua na najua wazi serikali haipo katika upande wetu maana mpaka Ofisi ya Raisi hili suala limeenda ila wale wenye uwezo wameachiwa sehemu zao kama wale wa Kiromo.

    Mnatuua waTanzania wenzenu kwa kumuweka mgeni ambaye hata siku moja hatochangia pato la nchi hii na bado mnatupa mishahara ya kima cha chini.

    Na kwa kima cha chini hicho tumepata ardhi yetu na bado mnatunyang'anya, mtalipizwa hapa hapa duniani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 18, 2010

    MTAWASEMA WABEBA BOKS USIKU NA MCHANA LAKINI MJUWE WENZENU WANA BETTER LIFE

    ANAEBEBA BOKS HAKOSI LAKI 5 ZA HUKO NYUMBANI KWA WIKI

    SASA NANI HUKO NYUMBANI ANAPATA MSHAHARA WA LAKI 5 KWA WIKI?

    MTABAKIA KUPIGA KURA WANAOKULA NCHI WENGINE KAZI KUSEMA WENZENU WABEBA BOKS KAMA MMEKOSA VISA WAULIZENI WALIPATA VIPI WAWASAIDIE

    MSHAHARA WA JUU HUKO NYUMBANI NI LAKI 3 KWA MWEZI ALAFU UNAJARIBU KUMSEMA MBEBA BOKS ANAEPOKEA LAKI 5 KWA WIKI SASA NANI MWENYE MAFANIKIO HAPO?

    WABEBA BOKS OYEEEEEEEEEEEEEEEE PIGENI KAZI MKIRUDI NYUMBANI WAPENI KAZI HAO WAPIGA KURA WANAOFAGILIA MAFISADI THEN WANALALA NA NJAA

    ANKAL MZEE WA FULANAZ UTAKUJA LINI TENA HUKU KUTUTEMBELEA TUNAKUMISSSSSSSSSS

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 18, 2010

    Naungana 100 kwa 100 na Anonymous wa May 17, 10:17.

    Pia nadhani ni vizuri vivutio vikizidi kusogezwa karibu na sehemu zenye walaji waliopo tayari (Ready Market), kama Mabibo Hostel.

    ReplyDelete
  21. Candid ScopeMay 18, 2010

    ASANTE SANA MICHUZI KWA KUJIBU SWALI LANGU LA KUPATA UFAFANUZI WA MRADI HUO, NASHUKURU, NIMEELEWA NA NAWAPONGEZA SANA TU WALIOBUNI HILO.

    NAOMBA WATANZANIA TUWE NA UPEO WA JUU KIMAENDELEO, KISIASA, KIJAMII NA KIUTAMADUNI. UZOEFU WANGU WA KUISHI NA KUFANYA KAZI TANZANIA NA NJE YA TANZANIA NIMEFUNGUKA ZAIDI AKILI NA KUJUA MENGI AMBAYO NINGEISHI TANZANIA TU NISINGEKUWA NA UPEMBUZI YAKINIFU KATIKA MASUALA MENGI.

    KWA WENZETU WALIOENDELEA MTU ANAYETOA WAZO AU KUJENGA HOJA YA KUANDAA MKAKATI FULANI MRADI HUO HUBATIZWA KWA JINA LAKE ILI KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA KWA JAMII NA TAIFA. NASHANGAA KWA WANAOBEZA PROJECT HIYO KUITWA KWA JINA LA RAIS MSTAAFU BEN MKAPA WAKATI HAKUNA PINGAMIZI KWA VILE NDIYE ALILITOLEA UVIFU. MTAKUMBUKA MENGI ALIYOFANYA KAMA KUSAMBAZA MAJI YA ZIWA VICTORIA BADALA YA KUFAIDI WA SUDAN NA WAMISRI TU KUPITIA MTO NILE NASI WENYE KULINDA ZIWA HILO TUNANUFAIKA NAYO.
    MSUMBIJI INABAKI HISTORIA TU YA KUVUKA KWA MITUMBWI AU MELI.

    NAMPONGEZA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE KUWA NAYE KARIBU NA KUTAMBUA MENGI ALIYOFANYA KWANI KWA NJIA HIYO TUNARITHISHANA MENGI KWA UFANISI NA RAIS ATAKAYEFUATA ATAKAMILISHA ALIYOANZISHA KIKWETE.

    mpoooooooooooooo?

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 18, 2010

    please leave mzee mkapa alone.kimsingi ni raisi aliyeweza kuunda mfumo wa nchi kwani ulikuwa haujawahi kuwepo tangia awali yake.angalia maeneo yote, mishahara, ukusanyaji kodi, majeshi, barabara, mahospitali - scanner kila wilaya, mashule....n.k. na yote haya aliyafanya kwa kumobilise local resources. kulaumiwa kupo pale pale kwani na utakuwa mzuri sana kulaumu kama hukuwahi kuwa hata calss monitor.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...