JK na Mtendaji Mkuu wa MCC Bwana Daniel Yohannes(kushoto) na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt(wapili) wakifunua kitambaa kwenye jiwe la Msingi kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Tanga-Horohoro.
JK na Mtendaji Mkuu wa MCC Bwana Daniel Yohannes(kushoto) na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt wakishangili muda mfupi baada ya kuzindua uejnzi wa Barabara ya Tanga hadi Horohoro leo mchana.
Baadhi ya wananchi wa eneo la Mikocheni Tanga wakisalimiana na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Tanga Horo barabara ya Tanga Horohoro leo mchana

JK akipiga stori na mwanafunzi ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga ambapo alizindua mtambo mpya wa kuzalisha saruji na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tanga-Horohoro
JK akifunua kitambaa kushiria kuzindua rasmi Mtambo Mpya wa kutengeneza Saruji katika kiwanda cha Saruji Tanga leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2010

    NEMEFURAHI JINSI HUYU MTOTO ANAVYOMWANGALIA RAIS USONI HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA WATOTO WAWE WAJIAMINI NI MWANZO MZURI KATIKA MAISHA YAKE: ANAJIFUNZA GOOD COMMUNICATION.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2010

    Mhe JK pamoja na kufungua Kiwanda hicho inakuwaje bei ya saruji inakuwa juu hata mtu wa kawaida anashindwa kuimudu? Gharama za uzalishaji zikoje? Serikali ifikirie kuwapa nafuu wazalishaji kwenye umeme wanaotumia kuwapa wananchi unafuu waweze kujijengea nyumba nzuri kwa bei nzuri.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2010

    SERIKALI IFUATILIE BEI YA SARUJI ILI WANANCHI WAACHANE NA MBAVU ZA MBWA JAMANI

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    Mhe JK pamoja na kufungua Kiwanda hicho inakuwaje bei ya saruji inakuwa juu hata mtu wa kawaida anashindwa kuimudu? Gharama za uzalishaji zikoje? Serikali ifikirie kuwapa nafuu wazalishaji kwenye umeme wanaotumia kuwapa wananchi unafuu waweze kujijengea nyumba nzuri kwa bei nzuri.



    HIVI WEWE UNAFIKIRIA KWA STYLE YA MAFISADI TUTAFIKA KATIKA MAISHA AMBAYO TUNAJIDAI KWA SASA HII KWA TZ ITAENDELEA KUWA NDOTO KWANI HAPA TZ MZUNGU ANAPEWA KIPAU MBELE KULIKO MZAWA SO ILI TUFIKIE MALENGO BORA TUENDELEE KUNUNU SARUJI TOKA YEMEN/DUBAI N.K KWANI NI NZURI NA PIA SI UZURI TUU NI IMARA MIMI NDIO NINAYOTUMIA.

    KAMA UKINITAFUTA HUNIPATI NAOGOPA WATANITAFUTIA SABABU WANISWEKE LUPANGO......... HABARI NDIO HIYO

    ANY COMENTS AM READY FOR REPLY

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2010

    Anon May 28, 03:36

    How very true indeed. Confidence ni kitu muhimu sana kuelekea mafanikio. Shida yetu tulio wengi ni jinsi ya kujenga hiyo confidence.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2010

    MIMI NINGESHAURI UCHAGUZI UWE UNAFANYIKA KILA MWAKA AU HATA BAADA YA MIAKA MIWILI. MAENDELEO TUNGEYAPATA SANA.

    VIIONGOZI WENGU HUWA WANALALA MPKA WAKATI WA UCHAGUZI NDIO MAMBO YANAAMKA...IMAGINE RATE HII YA UFUNGUSI WA VITU INGEKUWA KILA BAADA YA MIAKA MIWILI TUNGEKUA WAPI?

    God
    Bless
    Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...