Daraja hilo lenye urefu wa meta 720 na upana wa meta 13.5 ni kiunganishi kizuri kwa nchi hizi na tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya barabara. Ni ukombozi kwao.
Wazo hilo lililotolewa na marais waasisi; marehemu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji mwaka 1975 na kutekelezwa na viongozi waliofuata na kukamilishwa na waliopo sasa.
Wazo limesimamiwa na mkandarasi M/s China Geo- Engineering ambaye alisimamiwa na Mhandisi Mshauri NorConsult kutoka Norway, kwa uvumilivu wao na juhudi kubwa za kukamilisha daraja hilo, ambalo litabaki kuwa alama ya uhusiano mzuri na wa kihistoria wa nchi hizi.


Inapendeza sana tu kwani huo ndo mwanzo wa maendeleo, kazi sasa itabaki kwa madereva hasa wale wazembe hala hala tu wasije bomoa daraja letu.
ReplyDeleteSASA HIZO KOFIA ZA CCM ZAHUSIANA NINI NA DARAJA LA UMOJA? INAELEKEA CCM MNATAKA KUWEKA MWEKEZAJI HAPO.
ReplyDeleteThat is great.Big achievement for our countries.
ReplyDeleteMzee mithupu mbona naona hili daraja la umoja kila siku linafunguliwa au??
ReplyDeletekwa nni serikali isliite hili daraja jina la mzee ruksa,maana daraja alojenga yeye liliitwa mkapa,na hili liitwe mwinyi,maana lile la mwanzo lilistahili kuitwa daraja la mwinyi,lakini blikaitwa mkapa
ReplyDelete"tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ...."
ReplyDeleteNi kweli ndugu mwandishi kwa wosia wako wa kama 'litatumika kwa maslahi WATU wa Tanzania na Msumbiji' maana yapo mengi sana ambayo hayatumiki kwa maslahi ya umma. Tunawapongezi kwa kufungua daraja hilo, na sasa fanyeni utaratibu wa kufungua jengo la 'WAMACHINGA COMPLEX' Mnasubiri uchaguzi upite ili wakubwa wagawane vyumba vya biashara?
mita 720 siyo mchezo, ni daraja lefu sanaaa...ulinzi unatakiwa ili jamaa (mijizi) wasianze kuiba vyuma hapo liweze kudumu muda mrefu.
ReplyDeleteMWINYI HAJAJENGA DARAJA LA MKAPA/LA MTO RUFIJI LIMEJENGWA WAKATI WA UONGOZI WA MKAPA. KWA NINI LIMEITWA MKAPA HUO NI MJADALA MWINGINE
ReplyDeleteASANTE SANA MZEE MKAPA JUHUDI ZA KAZI ZAKO BADO ZINAENDELEA KUONEKANA; WENGI WATAENDELEA KUKATA TEPE ZA KAZI ZAKO. TUNASUBIRI KAZI ZAO.........................UBARIKIWA AFAYA NJEMA NA UTULIVU WA MWILI NA AKILI.
ReplyDeleteKWA MWENDO HUU WA MKATA TEPE INAWEZEKANA CCM SASA WAKAUNDA SERIKALI YA MSETO NA CHAMA CHA KIPYA KINACHOKUJA...MAANA SASA CUF BASI WAMEPIGA RANGI MAGARI YALE YELE YA ZAMANI "LIPUMBA NA HAMAD" WAPI NA WAPI TEN...
Jamani wadau wa hii Blogu.Mwalimu Julius Nyerere si marehemu ni hayati.Hatumuiti Mwal. Julius Nyerere marehemu bali hayati Mwal.Julius Nyerere.
ReplyDeleteNafikiri mmenipataaaaa...tehe teh teh
MARAKUMI KUFANYA BIASHARA NA CONGO, MSUMBIJI, MALAWI NA ZAMBIA....HATUWATENGI (WAKENYA NA RWANDA) UGOMVI WAO BADO MBICHI..
ReplyDeleteVIVA FRERIMOOOOO....VIVA MSUMBIJIII..
ReplyDeleteanaesema ushirikiano wa Tanzania na Msumbiji ufe afe yeye kwanza.Hebu utafuteni huo wimbo nilioweka kibwagizo chake hapo juu,uliimbwa na kamanda GURUMO na wenzake ndani ya JUWATA JAZZ BAND JJB enzi hizo