Daraja la Umoja kwa upande huu
Daraja la Umoja linavyoonekana kwa juu
Daraja la Umoja kwa pembeni

Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji wakikata utepe kufungua rasmi daraja la Umoja huko Mtambaswala,wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara leo asubuhi Daraja hili linaunganisha nchi hizi mbili na ni kielelezo cha mshikamano na udugu wa kihistoria uliopo baina ya watu wa nchi hizo.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 720 na upana wa meta 13.5 ni kiunganishi kizuri kwa nchi hizi na tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya barabara. Ni ukombozi kwao.

Wazo hilo lililotolewa na marais waasisi; marehemu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji mwaka 1975 na kutekelezwa na viongozi waliofuata na kukamilishwa na waliopo sasa.

Wazo limesimamiwa na mkandarasi M/s China Geo- Engineering ambaye alisimamiwa na Mhandisi Mshauri NorConsult kutoka Norway, kwa uvumilivu wao na juhudi kubwa za kukamilisha daraja hilo, ambalo litabaki kuwa alama ya uhusiano mzuri na wa kihistoria wa nchi hizi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2010

    Inapendeza sana tu kwani huo ndo mwanzo wa maendeleo, kazi sasa itabaki kwa madereva hasa wale wazembe hala hala tu wasije bomoa daraja letu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    SASA HIZO KOFIA ZA CCM ZAHUSIANA NINI NA DARAJA LA UMOJA? INAELEKEA CCM MNATAKA KUWEKA MWEKEZAJI HAPO.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    That is great.Big achievement for our countries.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2010

    Mzee mithupu mbona naona hili daraja la umoja kila siku linafunguliwa au??

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2010

    kwa nni serikali isliite hili daraja jina la mzee ruksa,maana daraja alojenga yeye liliitwa mkapa,na hili liitwe mwinyi,maana lile la mwanzo lilistahili kuitwa daraja la mwinyi,lakini blikaitwa mkapa

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2010

    "tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ...."

    Ni kweli ndugu mwandishi kwa wosia wako wa kama 'litatumika kwa maslahi WATU wa Tanzania na Msumbiji' maana yapo mengi sana ambayo hayatumiki kwa maslahi ya umma. Tunawapongezi kwa kufungua daraja hilo, na sasa fanyeni utaratibu wa kufungua jengo la 'WAMACHINGA COMPLEX' Mnasubiri uchaguzi upite ili wakubwa wagawane vyumba vya biashara?

    ReplyDelete
  7. Sitaki Kura za WafanyakaziMay 12, 2010

    mita 720 siyo mchezo, ni daraja lefu sanaaa...ulinzi unatakiwa ili jamaa (mijizi) wasianze kuiba vyuma hapo liweze kudumu muda mrefu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2010

    MWINYI HAJAJENGA DARAJA LA MKAPA/LA MTO RUFIJI LIMEJENGWA WAKATI WA UONGOZI WA MKAPA. KWA NINI LIMEITWA MKAPA HUO NI MJADALA MWINGINE

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2010

    ASANTE SANA MZEE MKAPA JUHUDI ZA KAZI ZAKO BADO ZINAENDELEA KUONEKANA; WENGI WATAENDELEA KUKATA TEPE ZA KAZI ZAKO. TUNASUBIRI KAZI ZAO.........................UBARIKIWA AFAYA NJEMA NA UTULIVU WA MWILI NA AKILI.

    KWA MWENDO HUU WA MKATA TEPE INAWEZEKANA CCM SASA WAKAUNDA SERIKALI YA MSETO NA CHAMA CHA KIPYA KINACHOKUJA...MAANA SASA CUF BASI WAMEPIGA RANGI MAGARI YALE YELE YA ZAMANI "LIPUMBA NA HAMAD" WAPI NA WAPI TEN...

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2010

    Jamani wadau wa hii Blogu.Mwalimu Julius Nyerere si marehemu ni hayati.Hatumuiti Mwal. Julius Nyerere marehemu bali hayati Mwal.Julius Nyerere.

    Nafikiri mmenipataaaaa...tehe teh teh

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2010

    MARAKUMI KUFANYA BIASHARA NA CONGO, MSUMBIJI, MALAWI NA ZAMBIA....HATUWATENGI (WAKENYA NA RWANDA) UGOMVI WAO BADO MBICHI..

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2010

    VIVA FRERIMOOOOO....VIVA MSUMBIJIII..

    anaesema ushirikiano wa Tanzania na Msumbiji ufe afe yeye kwanza.Hebu utafuteni huo wimbo nilioweka kibwagizo chake hapo juu,uliimbwa na kamanda GURUMO na wenzake ndani ya JUWATA JAZZ BAND JJB enzi hizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...