BOFYA HAPA usikilize kipindi cha jahazi juu ya TUCTA
Hii ni tafakari ya Gardner G Habash na Ephraim Kibonde katika kipindi cha Jahazi kilichorushwa na redio CloudsFM siku ya Jumanne terehe 4 Mei 2010 wakizungumzia juu ya mgogoro wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Serikali kuhusu madai ya nyongeza za mishahara na maboresho mengine. Bofya kifute cha play kwenye pleya iliyopo chini ya picha nawe upate kusikiliza.
Shukrani kwa www.Bongo5.com kwa kuwezesha radio CloudsFM kusikika mtandaoni nasi tukaweza kurekodi.
Shukrani kwa www.Bongo5.com kwa kuwezesha radio CloudsFM kusikika mtandaoni nasi tukaweza kurekodi.
Mdau Subi wa www.wavuti.com
Audio ya alichokisema Raisi ipo
Audio ya alichokisema Raisi ipo
katika posti iliyotangulia (bofya hapa
-----------------------------
Angalizo: Habari zinasema Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA Nicholas Mgaya atakuwa katika kipindi cha Jahazi leo Jioni, kwa mujibu wa Kepteeeeein Gadna G Habash.
---------------------------------
Posti za Mkutano wa JK na wazee
------------------------------
Audio ya sehemu ya hotuba ya JK



Nilikisikia redioni, machache niliyoyasikia yalikuwa ni pumba tupu, walimsifia sana JK
ReplyDeleteHivi jamani hizi ndio Radio mnazosilikiza huko nyumbani, kwa nini hawazungumzi lugha moja?
ReplyDeleteHii radio ya online ya Clouds ni ya kubahatisha sana radio haipatikani 80% ya muda wote. Kama imewashinda itoeni tuu.
ReplyDeleteWaambieni hawa watangazaji kuwa the bucks stop with the president. Nadhani Radio clouds inabidi wapepeze bendera ya CCM !
ReplyDeleteNilimsikiliza Kibonde ila nilimwona mpuuzi tu, kwani hata yeye hakuwa na chochote cha maana. Eti wafanyakazi wa serikali hawajitumi, watajitumaje wakati mazingira yao ya kazi ni magumu?! Kibonde kama mfanyakazi anapata laki na nusu kwa mwezi unategemea atakula nini, watoto watakula nini, wanaendaje shule na yeye atasafirije kuja kazini?! kumbuka kuna ada za shule, matibabu na mengine lukuki kama maji, umeme nk. Kibonde acha matusi, tunakutambua wewe ni CCM ila usituletee uCCM wako pindi tunapopigania haki zetu. Mbona Kikwete yeye anashinda ng'ambo tu anapata allowance kiasi gani?? wabunge wanapata kiasi gani? mawaziri kiasi gani? Kibonde msaliti mkubwa wa wapenda haki. Sintasikiliza tena kipindi chako.
ReplyDeleteKibonde you are my friend lakini kuhusu issue hii mlichemka kwa kusifia raisi tu, lakini amkwenda deep kwenye issue yenyewe, kwa kuwa kama utapima pande zote utaona wapi kuna tatizo, raisi kuna namna moja au mbili wamemshauri vibaya sasa sijui nani mwenye makosa na yote hii ni funika kombe mwana haramu apite.
ReplyDeleteHiki kipindi mimi nilikisikia LIVE jana ile ile, kwakweli afadhali nimepata uwanja kuyasema haya; Huwa siwaelewi Kibonde na Gadna linapozungumzwa jambo linalomhusu JK, huwa kama vibaraka wenyewe ni kumpamba tu tena unaona LIVE kuwa wanajipendekeza kwa JK, kipindi cha jana ndio kabisa unaona jinsi ambavyo wamekuwa bendera fuata upepo.
ReplyDeleteMimi nawashauri wajaribu kubadilika kidogo maana wanajisahau kuwa kipindi kinasikilizwa na watu tofauti tofauti na wenye akili na mitizamo tofauti vinginevyo waweke bayana kuwa redio clouds ni ya CCm au ya JK au kipindi kiko sponsored na CCM! Kipindi huwa kinaboa sana when it comes to JK matters!! Wanajipendekeza kweupe kabisa mpaka aibu.
TUBADILIKE JAMANI!!!!
Usibane hii ni kero kubwa sana ANKAL.
Walimsifia?Labda wanajipendekeza,ila nadhani ukweli wanao moyoni kwamba mchemko ulikuwepo.
ReplyDeleteHawa jamaa Kibonde na Gadner wana ganga njaa kama sisi wafanyakazi wa serikali lakini kumfagilia rais kunaonyesha dhahili kuwa mnajikomba kwa JK sijui mnataka mpewe pande siku za kampeni za urais mwe maMC wake mzunguke nchi nzima? Ni dhahili kadanganywa na wasaidizi wake mfano angalia rais kasema kuwa tucta waliitwa kwenye kikao saa 4 wao wamefika saa 8 wkt ambapo si kweli tucta wenyewe wameonyesha barua toka wizarani ilionyesha wafike saa 8 nyie bana acheni kujikomba, mnajikomba mpaka mnajisahau na kupitiliza sasa inakuwa inaboa. Tunajua mnaishi kwa kupiga domo mngekuwa serikalini mngejua kama hiyo 104000/= ni ndogo au kubwa sijui kama mngethubutu kusema hivyo.
ReplyDeleteKuweni makini mauaji ya kimbari Rwanda kuna waandishi wamefungwa kwa ajili ya ushambenga kama wenu huu.
Mitthupu ukiibania hii comment utakuwa hujatenda haki hapa tunaongea ukweli na uhalisia.
Mvuja jasho.
clouds wanataka kuteuliwa ubunge ndio maana wanajipendekeza kama ilivokuwa kwa shosti wao amina.
ReplyDeletewanasahau kujua kwamba wao (kina gadna ni wanaume, so itakuwa ni issue kuteuliwa ubunge ili hali mkulu yeye yupo interested ina mademu zaidi as we all know)
Afadhali Gardner hakuonyesha upande wowote, ila Kibonde wewe uliboronga ile sio radio yako ni wasikilizaji hukutakiwa kuwa na upande.
ReplyDeletehilo jukumu la kumpamba rais na serikali yake iachieni radio ya chama radio uhuru...
ReplyDeleteWE KIBONDE UTAACHA LINI KUJIGONGA KWA JK, HIVI ANAUFAHAMU HATA UWEPO WAPO? MAANA JANA NILIHISI KICHEFU CHEFU MAANA ULIKUWA KAMA MSEMAJI WA JK, KILA SMS YA MAONI ILIYOKUWA INATUMWA ULIKUWA UNAI CRUSH AS IF HAKUNA UHURU WA MAONI..ACHA HIZO BWANA UNAJIDHARIRISHA..
NAOMBA HII COMMENT ICHAPWE ILI HUYU KIBONDE AIPATE, MAANA ANACHEFUA HADI TUNAHAMISHA STESHENI, NA AMEKUA NA KAWAIDA HIO SIKU NYINGI KAMA ANA MASLAHI NAO HAO ANAO WASIFIA, TUTAKUWA HATUMSIKILIZI TENA..
AHSANTENI WADAU..
Tunaruhusu maoni, ni kweli kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni lakini si haki kwa mwananchi kupotosha jamii na hili Kibonde umeridhihilisha kwa kauli zako za kinafiki. Tukuulize mwenyewe hivi unaweza kuishi kwa laki moja kwa mwezi Dar es Salaam? Hiyo laki tatu tu kwa mwezi haitoshi hebu tafakali hili mshahara sh.laki 315,000/= familia ya watu 6 yaani Baba Mama na watoto wa 4 wanaosoma shule ya msingi na sekondari. Nauli ya baba kwenda kazini (posta) ni sh.700*21=14700,watoto nauli pamoja na hela ya kupunguza njaa shuleni ni sh.400*4=33600, chakula kwa siku asubuhi mikate sh.2,1200*30=36000,Mchana dash! Usiku unga sh.800,mkaa sh. 500, mafuta ya kupikia sh.300, nyanya sh.300, vitunguu sh.200,maharage nusu kilo sh.600,dagaa fungu sh.300,ndimu sh. 200 hesabu hii jumlisha kisha zidisha mara 30 utapata (800+500+300+300+200+600+300+200)*30=105000. Hii jumlisha na nauli ya baba na watoto wa nne: 105000+36000+33600+14700=189300! Yaani hapo umeishi kimkanda ile mbaya lakini matumizi yameshazidi mshahara wa laki moja! Na hapo hatujaingiza gharama za maji, umeme,na kodi ya nyumba ya kutosha watu 6. Hebu tujaribu kidogo. Kwa nyumba ya kupanga yenye umeme,bei ya chini ni sh.20,000 kwa chumba hivyo vyumba viwili na sebule ni sh.60,000 bei za mbezi mwisho makabe huko au mbagala ndani ndani(kumbuka ukienda nje ya mji pia nauli zaongezeka!. Maji ya kununua tuseme ndoo shilingi sh.50(kawaida ni sh.150-400 maeneo mengi jijini) unatumia ndoo takribani 8 yaani lita 160 tu! za maji kupikia,kuoshea vyombo,kuogea na n.k itaenda sh.12000 kwa mwezi. Umeme utakugharimu say sh.16000 tu kwa mwezi hapo itakua sh.(60000+12000+16000=88000/= )ukijumlisha na ile nyingine unapata sh.277,300/=,hapo unadaiwa sh.37700 tu ili ufikie kima cha chini alichogomea Rais.Kumbuka pia hela hiyo ie 315,000 itakatwa kodi PAYE (sh.27525/=) baada ya makato ya mifuko ya hifadhi(mfano NSSF ni 10% ya "Gross salary",jaribu kuingiza
ReplyDeletehapa hiyo hela utapata kodi, pia kuna makato ya nayoenda mifuko ya hifadhi ya jamii(eg NSSF ni 10% ya mshahara kabla ya kodi ie31500 ) Ukitoa mshahara 315000 unapata (315000-31500-27525) shs.255975 huku matumizi yakifika sh.277300/ na hapo Baba uache pombe,sigara, na familia msimiliki simu ya mkononi wala msiumwe au kununua nguo,wala kupaka mafut,kuoga na sabuni au kusugua meno kwa dawa za meno vinginevyo hesabu itapanguka kabisa . Mheshimiwa Rais hebu tuombe radhi sisi wafanyakazi wako maana hukututendea haki kwa kutukorome kiasi kile kwani madai yetu ni ya Msingi mno.
jamani mmeongea mengi nakubaliana nanyi. Huyu kibonde, hata na gadna ni wa kusamehe tu. Ngoja tuwaulize wao wana kazi gani ya kutambia kama sio kuganga njaa na kutafuta kazi za ziada kwenye uMC? ingekuwa kazi kweli wangekuwa na ziada au umaarufu njaa wao unawadanganya. Kuna watu wana mafanikio hawasemi kitu wala kukashifu watu wa chini kama akina kibonde. kwanza wasikilize kwa umakini hawa jamaa kwenye jahazi utaona jinsi wanavyo showoff, mara gari langu, mara mke wangu, mara blackberry, mara sijui ninacheo shule gani!! Yaani ni inaonyesha ni watu wa aina gani. utoto mwingi na majigambo ya kizamani!, lakini tuwaache wakue... wazazi wenu wangelipwa laki moja mngesema nyie au mngeendesha vogue si tungekoma! Shame on cheapness!
ReplyDeletewadau wawili hapo juu ukishaobofya hapo juu mwanzo wa habari kushoto chini ya picha kibonde pameandikwa BOFYA HAPA ukurasa ukifunguka bofya palipoandikwa ukurasa wa audio ukishafunguka play sasa hapo we tega masikio yako tuu usikilize jahazi
ReplyDeleteIn this issue and like Clouds Radio has been caught naked. It was a whole load of nonsense, really shame.
ReplyDeleteBut then looking at the guys and their levels of education, what do you expect??
Na bora hao TUCTA hawakwenda, they have reduced them to nothing!!
Sorry guys.
Hayo ndio matatizo ya utangazaji wa kujifunzia kijiweni.. hakuna balance ya mambo kabisa ni kuhukumu watu tuu..
ReplyDeleteMtu huko katika public media halafu unakazania msimamo wako binafsi..
Maadili gani ya habari hayo?
Kibonde na Gadner, hamjuli mlitendalo. Hata kama mnanjaa msijidharirishe kiasi hicho.Message za wadau hapo juu zinatosha kujua jinsi gani mmewakera WaTZ.Mfahamu hizi sio zama za zidumu fikra za mwenyekiti.
ReplyDeleteBofya hii link may be mtajua mpo wapi?
http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2254
Someni kwenye nakala inayosema "Kikwete awaombe radhi wafanyakazi"
Jamani, si ameshaweka wazi kuwa anaitwa "Kibonde"....mbona na nyie mnageuka vibonde kwa kumkosoa...someni alama
ReplyDeleteSHULE...SHULE...SHULE...SHULE...NDIO TATIZO KUBWA...ACHENI KUAJIRI WATU AMBAO HAWAJASOMA ILI MUWALIPE MISHAHARA MIDOGO...PERSONALLY HUWA NIKIAMUA KUSIKILIZA JAHAZI NI PALE AMBAPO NINAHITAJI RELAXATION AU NI KAMA VILE MTOTO KATOKA SHULE KACHOKA SASA ANARELAX KWA KUANGALIA KATUNI....HUWEZI KUPATA CONCRETE NEWS KWENYE JAHAZI...NI KAMA COMEDY FULANI HIVI...KIBONDE NA MWENZAKO HAMUWEZI KUPATA UBUNGE AU CHEO CHOCHOTE NDANI YA CCM AU SERIKALINI KWA KUWA WACHEKESHAJI...TENA HUKU KWA ANKAL MNAPAVAMIA TU! MNATAKA KUTUPOTEZEA STEP KWENYE BLOG YETU NZURI YA JAMII...SASA UMEWADIA WAKTI ITUNGWE SHERIA KUHUSU MAADILI NA QUALIFICATIONS ZA UTANGAZAJI KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA KUWE NA CHOMBO KINACHOREGULATE HIYO SHERIA.NAWASILISHA.
ReplyDeleteAnonymous wa Wed May 05, 06:10:00 PM has said it all...what more can we say?? brilliant one.
ReplyDeleteA propaganda radio. In a balanced media you don't take sides but these nuts are.
ReplyDeleteSome People are alive only because its illegal to kill them.
ReplyDeletemsichanganye lugha jamani. Kipindi ni ch Kiswahili sasa so so za nini? Kama unataka weka mada kwa Kizungu tujue moja
ReplyDeleteAnkal maoni yangu kabana!.....kisa nimemtaja DINA na GEA nini!? Ankal wacha watu wafunguke!!
ReplyDeleteTuache uongo jamani kwa hali hii rushwa ndogondogo zidumu, na mimi(sio chizi jamani) nasimama kifua mbele kutetea rushwa hizi ndogondogo kama unabisha hebu soma vizuri maoni ya anonymous wa Wed May 05, 06:10:00 PM. Huyu mfanyakazi anamudu vipi kuishi katika mshahara huo huku mkewe akiwa mama wa nyumbani(maarufu kama golikipa)? Bila rushwa hapa jamaa anaweza kweli kuchangia harusi? Inatisha hali hii Hakika Mgaya unastahili pongezi,Mgaya hoyee! Mgaya for Pres........ mh, eh Presision air!
ReplyDelete