Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa leo na kesho ni siku za kujiandikisha kwa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, muda huu wa siku mbili umeongezwa ili...
Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa leo na kesho ni siku za kujiandikisha kwa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, muda huu wa siku mbili umeongezwa ili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliokosa fursa hiyo waweze kufanya hivyo.
Hii ni nafasi yako mdau kushiriki katika zoezi hili muhimu katika kuchagua viongozi imara kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Natoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao hawana kadi za wapiga kura waende kwenye vituo na kujiandikisha. Mchango wako katika kuchagua viongozi bora unaanzia kwako.
Mdau wa
Je kutakuwa na nafasi nyingine ya kujiandikisha? Kuna utaratibu gani wa Watanzania walioko nje ya nchi kujiandikisha?
ReplyDeleteYah nami pia nimeguswa na hilo maana nategemea kurudi home baada ya miezi mne hivyo nitakua nimepoteza haki yangu ya kujiandikisha?
ReplyDeleteBraza Mvano
kwa tulioko nje ya Tz hakuna kuvote jamani??? na km sintakuwa na kadi this year inabidi nisubiri tena hadi uchaguzi mwingine ndo nijiandikish nipate kadi!! ama sio wadau.Hii inakuwaje?
ReplyDelete"It's not the people who vote that count. It's the people who count the votes." (Josef Stalin)
ReplyDelete