TRA Imenichosha!
(By US Blogger)
Wadau wa Globu ya Jamii,
Kwanza nianze kwa kumshukuru mdau aliyetuletea habari za hawa mawakala wa kutoa mizigo bandarini na uwanja wa ndege kuwaliza wateja kwa kutumia hila na mbinu chafu katika kutoa huduma ya kutoa mizigo bandarini na uwanja wa ndege wa eapoti.
Wadau tuweke pembeni masihara, ukweli ni kwamba hawa TRA sasa wamekuwa ni mzigo na kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya nchi hii. Ukifika pale bandarini utakuta containers kibao zimekwama si kwa sababu waagizaji ni wapumbavu na hawakuuliza ushuru utakuwa kiasi gani kabla ya kuleta mali bali wanalazimishwa kupoteza mali zao kutokana na utaratibu mbovu na rushwa iliyokithiri miongoni mwa maofisa wa TRA.
Moja ya vigezo vikubwa vinavyotumiwa katika kupima kama kampuni inaendeshwa vizuri ni kwamba kampuni iwe na bajeti (makadirio ya mapato na gharama) na matokeo halisi yawe karibu na makadirio hayo.
Kwa mfumo tuliokuwa nao Tanzania hili haliwezekani, moja ya sababu zinazosababisha hili kushindikana ni TRA. Yaani hawa jamaa wanafanya kazi kwa uadui na chuki na dhamira za kuwaibia wateja badala ya kusaidia mteja alipe kodi halali na Serikali ipate cha kwake ili iendeshe shughuli zake.
Ujanja wanaofanya ni kwamba wanakubali kutumia viwango vya kodi vilivyo rasmi lakini wanakuja na thamani wanazotaka wao. Mfano, kama duty ni 18% na unaamini kabisha na kuwa na ushahidi kama mali unayoingiza ni ya $100 na unakadiria kulipa $18 wao watakugeuzia mchezo, wanachofanya wao ni kudai kwamba mali hiyo ina thamani ya $500 na hivyo ulipe $90!!!
Mzigo wangu wa biashara ulikuwa na vizawadi vidogodogo ndani yake kwa ajili ya ndugu, jamaa na marafiki na wala sikuvificha, vilikuwa katika hali ya kuonekana kirahisi kabisa na wala havikuwa vya bei mbaya. Jamaa wa TRA wamediriki kudai nilitaka kuficha kwa kuwa havikuwa katika invoice na kunitishia faini ya $10,000 kwa ajili ya vizawadi visivyozidi hata $200.Niliwaambia basi chukueni hicho ambacho mna mgogoro nacho na muniachie hivyo ambavyo havina ubishi na waligoma. Hapohapo wakajifanya eti watanionea huruma na niwape wao chochote (10% ya hiyo $10,000) ili yaishe juu ya ushuru ambayo tayari wameni assess.
Wafanyabiashara wadogowadogo wanaumia sana nchi hii, wengine wanalazimika kupitia nchi za jirani kutokana na dhuluma hii. Wafanyabiashara ambao hawasumbuliwi sana ni wale ambao wana ubia na vigogo. Siamini kama wakala wangu alishiriki kunila kwa sababu wakala ni baba yangu mdogo na nimeweza kuthibitisha independently kwamba risiti zangu zote ni halali.
Nimelazimika kulipa makodi ambayo ni kama mara 4 ya kodi nilizotarajia kulipa kutoakana na initial assessment. Fedha ‘nilizoliwa’ zimeingia katika mfumo rasmi (official) na nimepata risiti za malipo ambayo ni mara 4 zaidi ya malipo niliyotegemea. Hizo assessment na ‘re-assessment’ na ‘uplifting’ walikuwa wakizipiga na kuongeza kama masihara, yaani kama vile fedha huchumwa kutoka kwenye miti. Kimsingi waliamua kunikomoa kabisa huku wakitoa comments za kukirihisha. Huwa wanafanya hivyo ili kuchochea malipo ya mlango wa nyuma. Kwa mtu ambaye ana matatizo ya moyo namshauri kwa upendo kabisa asifanye biashara Tanzania, TRA inaweza kumsababishia kuwahi safari ya kwenda akhera kabla ya muda.
Niliwauliza maofisa wengine wa TRA kama tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa kuangalia namna ya kupata partial refund , jamaa wa TRA akaniambia ‘wewe US Blogger unadhani hii Marekani? Hapa tunapokea tu harudishiwi mtu hela , mambo ya refund hayo ni ya Obama’.Tena aliyeniambia hayo ni swahiba wangu ndani ya TRA ila hana la kufanya kutokana na system kuwa mbovu.
TAKUKURU muko wapi? Mzee Kitillya hawa vijana wako wanakuchafulia sana jina la mamlaka hii ya kodi. Rais na maofisa wa Serikali kila siku wanaalika wawekezaji na kutushawishi sisi diaspora tuwekeze nyumbani, tukiwezeka tunakumbana na hizi pressure na mazingira ya kufa mtu, kwa nini wanaachiwa hawa ‘mamilionea wa TRA’ tena wengine wana ‘vijisenti’ vya kutisha kwa kuiba fedha za Serikali na kunyanyasa wafanyabiashara!!! Inawezekana kabisa kwa mtu kukopa fedha ughaibuni kwa lengo ya kufanya biashara nyumbani na kulazimika kufilisika kutokana na rushwa iliyokithiri TRA. Yaani mtandao (website) wa TRA hauna hata link ya sehemu ya ‘malalamiko’ ama sehemu ya ‘Kutoa taarifa za siri’ ili hawa wasio waaminifu tuwaripoti na taarifa zifike kwa wahusika walio independent katika kusafisha TRA. Maofisa wana frustrate wajasiriamali na kulazimisha rushwa kama vile nchi haina wenyewe.
Ni haki kweli kushawishi Diaspora waje kuwekeza wakati nchi inanuka rushwa na assessment zinafanywa kwa kutumia thamani ya mali iliyo mara 4 ya thamani halisi?
USBlogger11@gmail.com

ndugu yangu acha tu, yaani unalipa kodi kubwa kuliko thamani ya mali! TRA si kitengo ninachokifurahia utendaji wake hata kidogo. cha ajabu wanaonekana kama mitandao wanaitembelea, na vitu kama magari vinauzwa mitandaoni kwa hiyo kujua thamani yake ni rahisi sana, lakini wata-uplift hizo thamani za magari kwa utashi wao!
ReplyDeleteMFUMO WA KODI NI ULE UNAOMKANDAMIZA MFANYABIASHARA MDOGO MBAYE ANATAKIWA ALIPE KODI KABLA YA KUFANYA BIASHARA! NAPIA KIWANGO CHA KODI KIKO JUU ZAIDI KULIKO MFANYABIASHARA MKUBWA MBAYE HUPEWA MSAMAHA WA KODI VIVYO HIVYO KWA MUAJIRIWA AMBAYE PIA KIWANGO CHA KODI YA MAPATO KIKO JUU UKILINGANISHA NA MFANYABIASHARA MKUBWA! LAKINI HAYA YOTE YANATOKANA NA SISI WANANCHI KUSHINDWA KUILAZIMISHA SERIKALI KUBADILI VIWANGO HIVI VYA KODI, TUMEKALIA NDIYO BWANA. tunalalamika leo kesho tunawapigia kura haohao watumishi ambao wanakuwa mabilionia bila kufanya biashara! nchi hii ni ya kipekee ambayo mtumishi serikalini anakuwa bilionia bila biashara na halipi kodi stahili.
ReplyDeletehapa ndo balaa la hii nchi jamani,nchi inaliwa hii???
ReplyDeleteafu ndo mnamsikia rais na hotuba zake za jazba na ubabe dhidi ya wanyonge badala ya kukemea na kuchukulia hatua kali dhidi ya ushenzy kama huu wa TRA
eeeeh Mungu unaona aya,hatuwezi vumilia!!
TATIZO KUBWA TULIONALO WATANZANIA NILAKUKULUPUKA KABLA YA KUFANYA JAMBO, KIKAWAIDA KUNATARATIBU YA KUINGIZA VITU HAPA NCHINI, KTU CHOCHOTE KINACHOINGIZWA NCHINI KINATAKIWA KIWE NA INVOICE NA PACKING LIST,NAZIPO TARATIBU MBALIMBALI KUTOKA NA THAMANI YA KITU CHENYEWE AU AINA YA KITU CHENYEWE. TRA OFFICIAL NA MAWKALA WAO HUPENDA KUJINAFAHISHA NA UMBUMBU WA IMPORTERS, SASA BASI KABLA HUJA AMUA KUIMPORT KWANZA JITAHIDI KUJUA PROCEDURES NA UKUBALIANE NA GHARAMA ZA WAKALA WAKO MOST IMPORTANT USITUMIE MAWAKALA VISHOKA. MWISHONI NA KUBALIANA NA MTOWA HOJA KWAMBA MAAFISA WA TRA WANACHAFUA SANA JINA LA KITLYA NA PESA ZAO WAZAO WANAZIPATA KWA DHURUMA SANA
ReplyDeletethat really bongo,president dnt care abt thm bt they deeply worrying about him,,,,,,the time wl come for hope and change,,,,,kazi kwako Misupu
ReplyDeleteNahisi hii TRA ibinafsishwe maana Serikali imeshindwa,Ukileta kitu wanapiga thamani ili ulipe kodi bila kuzingatia kwamba kitu chenyewe ni used!kwani hawa hawajasoma accounting wakajua kama kuna kitu kinaitwa depreciation? kwanini wasitumie viwango hivyo? Pili nilituma ufunguo tu wagari kwa njia ya DHL kwa kuwa niliogopa gari ikafunguliwa Uliganda TRA hadi nililipishwa 50,000 TSH wakati nili include registration za gari na bill of lading ndani ya bahasha kuonesha kuwa nilishatuma gari kabla, still wamesema ati ni wa biashara kwa kuwa una FOB! HADI LINIII MBONA ULAYA KUINGIZA GARI SIO BIG DEAL KABISA? hulipi hata cent badala ya gharama za kusafirisha zisizozidi 80 euro kutegemea na CC- hapo ukitoa ZNZ kwenda DAR unapigiwa difference kama ulilipa mil 3 na bara ni mil 5 unalipa 2 za juu sasa.TUNAUMIAAAA(mdau nuramo)
ReplyDeleteUnasema hizo fedha za ziada zinaingia kwenye mfuko rasmi (official) kwa sababu ulilipa benki? au kwa sababu uliewa risti unazina ni halali? Kalaghabaho!!
ReplyDeletenatamani osama aje aachie bomu hizo ofisi mfilie mbali nyinyi mashetwan wa tra wezi wakubwa!
ReplyDeleteKuna Kolabo ya hali ya juu sana kati ya maofisa wa TRA, wa Bank na hao clearing agents. Hapo ndiyo waru wanapolizwa. Usidhani ukilipa bank mwenyewe umeokoa chochote, hayo makaratasi ya porini yapo huko pia!
ReplyDeleteYesu alisema wazi kabisa ni vigumu kwa watoza kodi kuuona ufalme wa mbinguni. Ndio haya tunayaona sasa. TRA inahitaji mabadiliko makubwa na magumu, kama mheshimiwa Rais yuko serious tumpe majina ya wala rushwa wakubwa pale awachukulie hatua. Nguvu aliyoitumia jana kukemea walalahoi inatosha kabisa kurekebisha mambo TRA.
ReplyDeleteWEWE US BULOGA BWANA WEWE SIYO MAKINI NDIO MAANA TRA WANAKUFANYIA UMAFIA. SISI WATU WA MUZUMBE CHUO KIKUU CHA UNIVESITI CHA KULE MOLOGOLO BWANA TUKO JUU. KAMA NI SISI TUNAONEWA HIVYO TUNAENDA MOJA KWA MOJA HADI PALE NYUMBA KUBWA NA KUMBWAMBIA MUNENE BWANA TUMA TAKUKUKURU ILI HAO MANYANG'AU WANYANYASWE NAO. BWANA INABIDI URUDI UKASOME MUZUMBE UPATTE DIGIRII INAYOKUBALIKA KIMATAIFA BWANA. WAKISHAONA TU JINA LAKO LINA JINA MUZUMBE, BWANA MIZIGO YAKO HASHIIKU MUTU, MIE NAKWAMBIA
ReplyDeleteNd'o mana nathemaa thirudi ng'oo! Ushenzy na ushuzy mtuuup! Amani haiji ila kwa ncha ya upanga. Mtabaki kulalamika wee hadi mnaingia kaburini! Akt noowww! Muuuuvvv dudee!
ReplyDeleteDayasipora
Mkuu US blogger kama unafikiria kuwa umelipa zaidi nadhani TRA watakuwa na njia ya kufuata ili uweze kulrudishiwa pesa zako, na kama unawajua hao waliokulipisha zaidi nina hakika utaweza kuwasema huko juu na ukapata haki yako. Peleka official complain TRA uone kama utapata majibu gani
ReplyDeleteBongo mtakaa wenyewe. Hamna cha Diaspora wala nini, hamna nia yoyote ya kuleta maendeleo, wizi tu na mitambi inazidi.
ReplyDeleteWafanyakazi wote wa TRA wanalindana kwa kula Rushwa,ni mijizi tu na Rais wetu na serikali ya Tanzania imewafumbia macho,Yaani watu wa hali ya kawaida na hali ya chini wanaishi taabu sana kimaisha Tanzania,Haki hakuna na uonevu uliojaa!Yaani Rushwa imekuwa ni kero na karaha kubwa hadi mtu hautaki kurudi nyumbani,ukiangalia ni sehemu nyingi sana serikalini kuna Rushwa,kwa mfano TRA,AIRPORT,POLISI,TRAFIK,WIZARA YA ARDHI,HOSPITALI,WIZARA YA ELIMU N.K,Kila sehemu ni inanuka Rushwa tu!Hivi nchi yetu itaendelea lini?Na Serikali inaelewa sana kuwa kuna kero la Rushwa katika Ofisi na wizara za Serikali lakini cha ajabu bado inawafumbia macho na kuwalinda watu hao wabadhirifu na mafisadi wa nchi yetu nzuri!
ReplyDeleteHii ni Moja ya sababu inazonifanya nichanganyikiwe na wazo la kurudi Kwetu. Nchi imejaa majangili kila kona, kimara majambazi, posta matapeli, TRA majangili, polisi watemi, mamlaka ya maji wamelala, tanesco walishastaafu, muhimbili wamejaa madaktari waliofaulu mitihani badala ya kuwa na elimu basi kazi kweli kweli. JAMANI HIVYI TUMELAANIWA????
ReplyDeleteHEY MICHUZI,
ReplyDeleteNILIKUWA NA USHAURI KWAKO UNAJUA HAPA KWENYE BLOG YA JAMII KUNA IDEAS NYINGI SANA ZA KUBORESHA MAENDELE YA NCHI YETU. LAKINI IMEKUWA DESTURI TU TUNATOA LAWAMA NA SOLUTION LAKINI HAKUNA FOLLOW UP KWA WIZARA AU MHUSIKA KUJIBU AU KUSIKIA YEYE ANASEMA NINI? KUHUSU SHUTUMA HIZO HIYO NDIO TUNAIITA A TRUE JOURNALIST!!!!! KWA HIYO MZEE KWA SIKU HIZIMBILI SWALA HILI LA TRA TUNAOMBA UTAFUTE INTERVIEW NA WAHUSIKA WA TRA KWA NJIA YA VIDEO HATA DK 10 WAJIBU TUHUMA HIZO NA TUWASIKIE WANA MPANGO GANI KUTATUA MATATIZO YA USHURU NA UTAPELI WA MAOFISA WA TRA.
mdau opulukwa
wazee mbona mnamtetea kitilya.TRA ndo ofisi yake inabidi aisafishe.sijui hao wazee wanatia timu ulaya kulearn nini kwani mvuja jasho wa uk anapewa cha na serilkali vile vile ili ainuke ila bongo tambalale unachinjiwa baharini ufilie mbali na ka mtaji kako.nina mzungu anawish tuunganishe nguvu tuwekeze home ila nafikiria sipati jibu
ReplyDeleteHii mijitu ya TRA inakuja MAREKANI kununua nyumba kwa cash $500,000 na kuendelea. Ondoeni kisiki cha CCM ni wingu kubwa linaloendelea kula nchi kama vile mchwa kwenye kichuguu.
ReplyDeletemwandishi michuzi kama kweli ungrkua hunafanya kazi yako ya huandishi ungesha fanya follow up za hizi comment za watu make unaona mwenyewe watu walivyo na hasira kuhusu ili swala manake 90% ya watu wako wamechoka na TRA wewe kama muhusika wa hii blog ungesha waonyesha wafuasi wako kua you care nenda kwa viongozi wa ngazi za juu omba kufanya interview nao na kuwauliza maswali kuhusiana na shutuma wananchi wanazotoa kwako pili nenda tukululu nao wape mahojiano kuhusu hili swala kwanini raia wanaona ili jambo nawao wanalifumbia macho na sisi wafuasi wako tutakuelewa kwamba mnajali wa handishi duniani kote ndio viongozi wa kwanza kutoa uchafu wa serikali yoyote husika nenda acha woga na kubeba hao watu fanya kama BBC WANA HOJI HATA MARAISI WA NCHI KWENYE KITI MOTO
ReplyDeleteDiaspora, achaneni na kuwekeza bongo hadi pakae sawa...pengine hali itakuwa nzuri kwa wajukuu wenu. TRA wanaiba kila wakipata upenyo...na wanatuangusha sana wafanyabiashara. Mimi nafikiria kubadilisha profession sasa, ni kero sana pale. Na si takukuru wala usalama wanawaweza jamaa wa TRA, wote wamethibitisha kushindwa. Kilichobaki ni kumpa mchawi mwanao akulelee, yaana rais amshague kibosile wa TRA aongoze takukuru.
ReplyDeleteWEWE UNAESEMA UENDE PCB LABDA HUJUI KINACHOENDELEA.WAO PCB UKIENDA TU NAO WANAKUZUNGUKA KWA KWENDA KWA HUYO MLALAMIKIWA NA KUMTONYA KUWA ATATEGEWA MIPESA YA MOTO HIVYO JAMAA WA PCB NA TRA WATAPANGA NAMNA YA KUKUMALIZA KABISA WEWE MLALAMIKAJI,UTAJISHTUKIA UPO POLISI UNANYEA DEBE.TANZANIA IMEOZA,PERIOD,SYSTEMS ZOTE ZIPO BROKEN AND NO ONE CARES.WANACHOJALI HAO VIONGOZI WENU NI KUCHAGULIWA TENA THATS ALL IS IN THEIR MIND.WAHANA DHAMIRA YA KUBORESHA MAISHA YA WATU WA KAWAIDA NI KULINDANA TU AND THATS IT.
ReplyDeletemie kwenye maswala ya kutuma zawadi wala sipati tabu nanunua mizawadi nadunduliza weee then akitokea mzungu anaenda bongo nampa sanduku lina mizawadi ya kufa mtu na anapita nalo kwa ulainiiii na hawagusi ng'ooo si wanajua hawa ni watalii?? namshukuru Mungu nilipo kuna wazungu wana kampuni huko home so kila mwezi lazima kama wawili watatu watue bongo natuma zawadi nazotaka nazinafika poaaaa kurudi kusalimia ni mie na nguo zangu tu! hela ngumu ati halafu jitu moja limeamka asubuhi linakuja kukufanyia tuu usanii inauma sana
ReplyDeleteSio peke yako Us blogger, mi nilirudi mwaka jana na Ka-tv nilikokuwa natumia chuoni UK, nilichajiwa bei mara mbili ya ile niliyonunulia kule kisa nini ilionyesha mwaka 2008 ndio mwaka iliyonunuliwa, lakini ukweli ni kwamba niliibua kwenye sell. tena kumbuka nilikuwa na student visa ambao tunatakiwa tusilipie kodi.
ReplyDeleteNdio nchi yetu hii cha kufanya ni kupiga kelele kama hizi tutafika.