Ndugu Khamis Hamad Mnondwa miaka (28)kulia Mfanyabiashara akitangaza kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari -Maelezo leo jijini Dar nia yake ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Handeni Mkoani Tanga kwa tiketi ya CCM. Jimbo hilo kwa sasa Mbunge wake ni Mh. Abdallah Kigoda. Kuume kwake ni Mwirabi Sise, Afisa Mwandamizi wa Idara ya Habari.
Picha na mdau Anna Itenda -Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2010

    Wote CCM , hakuna jipya.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    safi sana!!
    Ubunge handeni ugombewe dar!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    Mdau hapo juu kula five.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    Kila kitu kinafanyiwa Dar ndio maana sehemu zingine haziendelei na hakuna mashindano ya habari au hata radio..

    Watu waanzishe magazeti ya mikoani hata radio za fm za mikoani..

    Hapa college yangu tuna radio station na gazeti letu...Chuo kina wanafunzi 21,000

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    Kumtoa kigoda pale Handeni ni kazi kweli maana al -maaruf na shulfu pia anazo na sie wazigua sijui kama tunaweza kumwendea kinyume , ngoma iko nzito sana na huyu ni kigogo wa kamati kuu (CC) mndolwa anahitaji kujiunga na chama kingine na sio CCM maana hapiti lakini sio mbaya kujaribu

    ReplyDelete
  6. Kijana ujiangalie sana. Huyo incumbent ni Gogo haswa halafu masuala ya utamaduni ni mkali sana. Kumshinda huyo lazima uwe na nguvu ya ziada ambayo ni ya Yesu Kristo. Unauona ujasiri wa jirani yake pale Kilindi mama Beatrice Shelukindo? Yule yuko fit kwa sababu anaye Yesu. Si unajua mdogo wake mheshimiwa naye ananyemelea pale?

    ReplyDelete
  7. Kumbe anaGOMBEA KWA TIKETI YA CCM??? huu ni usanii kwani hata Kigoda ni CCM na handeni imelala doro kipindi chote cha utawala wake,sasa huyo Mndolwa atafanya nini tofauti,Kwa Handeni nafikiri tunahitaji mgombea wa chama tofauti na CCM kwani CCM wayeyushaji hebu fikiria kwenda Handeni kwa kupitia mkata mpaka leo mvua ikinyesha mwalala njiani hata cku 2 tangu enzi na enzi huu ni ufisadi wa waziwazi tena inakera sana.

    Majoy
    Mzigua wa Handeni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    mimi namuunga mkono sana kijana mwenzangu maana kigoda hana kipya.alipewa madaraka mengi makubwa zaidi ya huo ubunge lakini ukienda handeni,hakuna kipya.barabara mbovu,maji hakuna maisha mabaya ya wananchi.mimi nipo nje ya nchi ila kama ningekuwepo msimu huu,ningesimama nae.Nitamuunga mkono kijana mwenzangu kwa kumuwezesha tuondokane na hao wazee walioishiwa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2010

    KWA NINI ASIENDE HUKO HANDENI AKATANGAZE NIA YAKE HIYO? SASA ANAENDA MAELEZO HAPA NI HANDENI?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2010

    Kwanza nampongeza kijana mwenzangu, hawa wazee wa CCM waliharibu nchi yetu

    songa mbele songa mbele

    regards
    mdau ufini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...