Salaaam Ankal!
Napenda kuwataarifu na kuwakumbusha wadau wote wote waishio Ukerewe kuwa mnakaribishwa kwenye uzinduzi wa Movie ya £ovely Gamble mjini Kusoma( Reading) Tarehe 29.05.2010

Kuanzia saa 18.30-11.30. Uzinduzi huu ni maalam kwasabau utakuwa ni kuchangia watoto yatima waliohathirika na Ukimwi Tanzania wanaolelewa na Tanzania Mitindo House. watoto hawa wanahitaji huduma zote za msingi sawa na wototo wote. Wanahitaji chakula bora, malazi, makazi na muhimu sanaa kuonyeshwa uthamani wao katika jamii.

Pia Kuja kwako kutaweza kuchangia Jumuia yetu ya kitanzania hapa Reading kuendeleza shughuli za kusaidia na kuimarisha jumuia yetu kuhusuiana na mambo yanayomhusu mtanzania.

Hivyo tungeomba watanzania wote mjitokeze kwa wingi ili tushirikiane kujenga taifa letu na kuitangaza nchi yetu Ughaibuni. Pia kutawepo na burudani ya mziki, chakula, vinywaji kwa bei nafuu nyote mnakaribishwa.

Tiketi zinauzwa £10.00 na zitapatikana kwanza katika Duka na Bongo Flava, na Vicent Pub Kuanzia kesho mchana. Pia unaweza kupata ka kupiga simu 07810 11 8157 au 0786 55 945 76 pia ununua on line tafadhali bofya hii link hapo chini
http://www.wix.com/effort111/urbanpulse-tmh

Pia unaweza tembelea ukurasa wa kitabu cha uso(facebook) for more details
http://www.facebook.com/event.

php?eid=115572898479817&index=1

Tutawashukuru wote mtakao fika na kushuhudia Historia ya filamu ya kwanza kufanyika na kuzinduliwa Ukerewe na Wabongo.
Mdau
Frank Eyembe
Urban Pulse

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. son of alaskaMay 10, 2010

    10 £'s you guys must be having a laugh

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    Mbona sijawahi kusikia movie za kibongo kuzinduliwa? Hii ina nini zaidi, au kwa sababu imeectiwa uk.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2010

    Wewe unaeshangaa £10 kwani kuna ubaya gani?? Kwanini watu hatupendi kusaidiana? Halfu hiyo £10 unaenda kununa bia ukalewa si bora utoe ikasaidie hao watoto???

    Movie za kibongo huwa zinazinduliwa kwa hiyo sioni ajabu yeyote kuzinduliwa kwa hii filamu Lovely Gamble. Hebu tuwape support kidogo hawa vijana

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2010

    MESHIKILIA MJI WA KUSOMA MJI WA KUSOMA!!!!!!!! (HIYO READING)INATAMUKWA REDINGI SI RIDING, NAHISI FROM RIDINGI NDO UNATAFSIRI MJI WA KUSOMA. HAYO SI MATAMSHI YAKE

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2010

    Utu wa mtu kazi. Bora huyu dada kapata kazi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2010

    hawa watu wanaojifanya wamekaa mji wa reading mbona hata kutamka reading kunawashinda sio riding bwana ni reding na ungana na mdau wa hapo juu halafu utoe ten pound na vinywaji ununue mnakazi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2010

    wewe anon 8:01 ni afadhali tu usingesahihisha maana na wewe umechemsha. SIo mji wa kusoma kutokana na inavyotamkwa lakini ni jinsi inavyoandikwa haina tofauti na neno "kusoma" kwakingereza linavyoandikwa "Reading". Mara nyingine tusiwe tunapenda kukosoa sana maadam umeelewa tulia tu maana ukilalamika unaishia kuchemsha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...