Washiriki wa Tamthilia ya Lovely gamble wakiwa na Viongozi wa TA pamoja na Afisa wa Ubalozi Amos Msanjila. Mwandishi wa TZ-ONE Ally Muhdin akiwa na mshiriki wa Tamthilia ya Lovely Gamble Ann Lynn Kapinga.


Urbun Purse wamezindua rasmi tamthilia ya "Lovely Gamble" katika mji wa Reading, nchini Uingereza.

Tamthilia hiyo inayohusu Mapenzi, Muziki, Usaliti na Uongo imetungwa na Frank Eyembe pamoja na Alan Kalinga.

Mhariri wa tamthilia ya "Lovely Gamble" Baraka Baraka amesema wamejaribu kutengeneza tamthilia hiyo katika kiwango cha kimataifa ili kuweza kulingana na tamthilia nyingine zinazoonyeshwa duniani.

Mtunzi wa tamthilia hiyo Frank Eyembe amesema jina la tamthilia limejieleza kwani kila kitu kinachohusiana ya tamthilia wamecheza pata potea kwani hawakujua jinsi gani wataweza kufikia hapo walipofikia.

Matukio na mambo yaliyofanyika katika tamthilia hiyo hayajalingana na tamthilia nyingine.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa tamthilia hiyo Mwenyekiti wa TA John Lusingu amesema amefurahishwa na kitendo cha Watanzania kujitokeza na kuonyesha kuwa na uwezo wa kufikia mbali katika utengenezaji Tamthilia.

Akiongea kwa niamba ya Balozi Maajar, mgeni rasmi Amos Msanjila alitoa shukrani kwa waandaaji na watayarishaji wa tamthilia hiyo kwa kukumbuka kama kuna ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kuweza kushikiana nao katika hafla mbalimbali.

Bw. Msanjila alifurahishwa sana na kazi waliyoifanya Watanzania walio nje ya nchi kwa kuweza kujitafutia ajira na kuitangaza nchi yao katika masuala ya tamthilia.

"Jamani tupende vyetu" miaka ya 90 hatukuwa na uwezo kama tuliofikia hivi sasa. Alisema Msanjila.

Amewashauri Watanzania wasiogope Uthubutu, wakubali kurekebishwa na tupeane moyo.
Akifunga hafla ya tamthilia hiyo, Bw. Eyembe alitoa shukrani za dhati kwa Watanzania wote waliojitokeza na kutoa michango katika kufanikisha kuitangaza tamthilia hiyo.

Pesa zitakazopatikana katika mauzo na maonyesho ya tamthilia ya "Lovely Gamble" zitachangia watoto yatima na jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Uingereza.
Ally Muhdin
wa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2010

    Hivi bado mimi sijaelewa kuhusu hii movie ya Lovely Gamble kwanini imepigiwa debe saaana!! ina kitu gani spesho tofauti na movie tulizozizoea hapa bongo? au ni kwasababu ime rekodiwa UK??

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2010

    tuelekeze njia rahisi ya kuipata tafadhari.mdau uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2010

    Yesuuuu na maria,now we can rest in peace.Too much it was!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2010

    mbona kwenye picha Kanumba hayupo?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2010

    miss kapinga dada una rangi murua

    naskia iyo movie ina kiwango
    hongereni wabongo na mzidi kujitaidi pia

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2010

    high quality movie thats why..movie ngapi zimeactiwa UK?love you sis ann lynn k...u luk gawjuz..guess ts in a family...na huu ni mwanzo tuu..a u k

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2010

    afadhali sasa tulishachooka na uzinduzi

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 31, 2010

    sijalizika kwa nini isizinduliwe bongo basi iuzwe huko huko

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 31, 2010

    tehe tehe ,ule wako wewe kidudu mtu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2010

    Si mnasema bongo tambarare? Mhhhhh hela yote iko huku...wanataka kuiuza huku huku....Bongo tambarare wakati mafisadi hawajui kuangalia movie. teh teh tehhhhh

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 31, 2010

    Michuzi mbona umegoma kutoa comment zangu za jana?au na wewe una deal nao

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 03, 2010

    Sijui wanaosema hiyo movie kiwango wamezoea kuangalia filamu gani. Ni heri wangeiigiza kwa kiswahili yote, kiingereza kwenye filamu hii ni kibovu. Sauti mbovu, na editing ndio mbovu zaidi. Story nzima haileweki...ila mwanzo mgumu. Tunasubiri filamu nyingine...rekebisheni kiwango.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...