Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi (shoto) akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya taifa ya Wanawake ‘Twga Stars’ Sofia Mwasikili wakati wa hafla ya kuagwa kwa timu hiyo iliyofanyika leo kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Eritrea kwa ajili ya mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Eritrea. wachezaji wa Twiga Stars wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ulinzi,Mh. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati wakikabidhiwa Bendera ya Taifa kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye mechi ya marudiano na timu ya Erirtea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2010

    Sasa mbona hamtuambii mechi ya kwanza iliisha vipi kama hii wanayokwenda kuche ni ya marudiano?

    Bora hata msingetuletea habari hii haina hata ladha yeyote ile kutokana na kutokujua mechi ya kwanza iliisha vipi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2010

    Je ni Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi au Mh. Emmanuel Nchimbi????

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2010

    mdau wa kwanza yaonekana hukuona matokeo ya mwanzo alafu unalaumu mbona matokea ya mwanzo yalionyesha kuwa timu ya twiga iliibangua Eltrea mabao 8 kwa 1 na sasa ndo wanaenda marudio.

    MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2010

    kwa kumsaidia mtoa maoni wa kwanza match ya kwanza iliyofanyika Dar twiga waliipiga eritria 8-1

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2010

    we mdau hapo juu, wakati mwingine ujifunze kuuliza kwa upole ueleweshwe na s kuanza kutoa lawama. unategemea habari za wiki iliyopita uletewe leo kweli...??? "Kuuliza si ujinga bali anayesita kuuliza ndiye mjinga zaidi"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...