
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Wananchi na Wanasheria Wanawake katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA)Zilizoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam, kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki ya Mwanamke ni haki ya Wote.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha vitabu vya mpango kazi kwa mwaka 2010/2015 wa umoja wa Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), mara baada ya kuzinduwa Vitabu hivyo katika Maadhimisho ya kutimia Miaka 20 ya Umoja wa wanasheria wanawake Nchini (TAWLA) zilizoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki ya Mwanamke ni Haki ya Wote.

Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akizinduwa Mpango Kazi kwa mwaka 2010/ 2015 wa Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA), kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Umoja huo yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti mstaafu wa Umoja huo Bibi Victoria Mandele, kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki ya Mwanamke ni haki ya Wote.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanasheria Wanawake wa Tanzania (TAWLA) Bibi Victoria Mandale kutokana na kutambuwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza Umoja huo, katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA)zilizoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam, kauli mbiu ya mwaka huu ni haki ya Mwanamke ni Haki ya Wote.

Wasanii wa kikundi cha muziki cha Savaev Sisters wakionesha umahiri wa usanii wao, kwenye maadhimisho ya kutimia miaka 20 ya Umoja wa Wanasheria Wanawake wa Tanzania (TAWLA) zilizoadhimishwa rasmi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Maendeleo Jinsia na Watoto,Dkt Lucy Nkya akiwa amebeba bango lenye ujumbe "HAKI HAINA JINSIA" wakati wa maandamano ya sherehe za Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaa.
Baadhi ya wadau mbalimbali Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali zililokuwa zikitolewa na viongozi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya utendaji kazi wa TAWLA hapa nchini.sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi mmoja.
(Picha na Aron Msigwa-Maelezo na Amour Nassor -VPO)
Duh...Hivyo vitenge vyenye white and blue me like. Viko poa sana!!!
ReplyDeleteTAWLA VIPI MIAKA ISHIRINI MMESHINDWA KUWASAIDIA WANAWAKE WENZENU KUANZISHA CHAMA KISICHO NA ITIKADI ZA KIDINI NA KISIASA AMBACHO KINGEKUWA NA UWEZO WA KUWAELIMISHA WANAWAKEKATIKA SIASA NA UCHUMI UNDELEVU. WAKATI NYIE MKISHEREHEKEA WAPO WENZENU WENGI SANA WANALIA KWA KUPORWA NA KUNYANYASWA WAKIWA HAWAJUI WAPI WATAPATA MSAADA WA KISHERIA. NAJUA NI VIGUMU KWA CHAMA CHENU KUWAFIKIRIA HAO LAKINI KAENI NA MTAFAKARI JUU YA HATIMA YA WANAWAKE WASIO NA KUCHA WALA MENO.
ReplyDeleteHongera TAWLA kufikisha miaka 20
ReplyDelete