Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Geoffrey Wilfred (kushoto) akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula mwenyekiti wa kituo cha watoto yatima group cha mbagala chamanzi, Winfrida Rubanza(kulia)
Mlezi wa watoto washio katika mazingira magumu wa kituo cha yatima group trust fund cha mbagala chamanzi Tuma Simba(kushoto) akimuonyesha Emmy Njau biringanya kwenye moja ya mradi wa shamba ulioanzishwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya watoto hao wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho kwa lengo la kutoa misaada mbalimbali.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima na walezi wao katika kituo chao cha mbagala chamanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2010

    Hii nimeipenda zaidi, kuliko ile ya kuwapelekea sukari, unga, sabuni n.k. ambazo zitatumika kwa siku chache au wiki moja tu. Kuwasaidia kubuni miradi kama huu wa bustani unawasaidia sana sana hawa vijana. Kwanza wanajifunza kujitegemea, wanajifunza namna ya kuzalisha mali, na pia wanazalisha chakula cha siku nyingi kidogo.

    May God bless you Vodacom

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    Vodacom, mkumbuke basi na yatima wengine wako kigamboni huko vijibweni, yaani hao ndio wanahitaji hasa msaada tena wa haraka. nio watoto wadogo, idadi yao haipungui 60manake misaa yote inaishia huku, nendeni na vijibweni jamani mkawaone hao yatima ninao wazungumzia, wanasikitisha mnooooo!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2010

    Sawa Jofrey wakilisha wana kawe,safi sana kukuona hapo,mdau ughaibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...