Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kulia)akimkabidhi Aishwarya Nair wa Traince Asyla Attorneys charities(kushoto) hundi yenye thamani ya Tsh 1,800,000,baada ya mbuzi wao kuibuka kidedea na wapili toka kulia Mtaalamu wa Mambo ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, John William, Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Vijana wakiwa na mbuzi waliokuwa wakiwafundisha wa Ultimate Security katika kushiriki kwenye mbio za mbuzi zilizofanyika leo barabara ya Kenyata oysterbay jijini Dares Salaam kwa lengo la kuchangisha fedha na kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza,Ultimate Security walitoa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,200,000.
Vijana wakiwa nyuma ya mbuzi wa Vodacom Tanzania katika mbio za mbuzi zilizofanyika leo barabara ya Kenyata oysterbay jijini Dares Salaam kwa lengo la kuchangisha fedha na kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza.
Baadhi ya wapenzi wa mbio za mbuzi wakikimbia kwenda kuangalia mbio hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    Ni "mbuzi hao" SI "mbuzi hizo".

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2010

    Welcome to the welthiest nation in Africa.
    This is not a joke. Soma utaelewa nazungumzia nini.
    Wajinga ndio wali....
    Poleni Wadanganyika wenzangu, wacha tuendelee kudanganywa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2010

    Hivi hii huwa ni shughuli ya wazungu au kuna wamatumbi wanahudhuria? Sipati picha mmatumbi anashangilia mbuzi kukimbia bila kukimbizwa, na wala hayupo mawindoni kwa hiyo kwa nini akimbize mbuzi?

    medusa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Kila cha Mzungu ni swafi tu hata kama ni cha chooni!

    There is the propensity for Wamatumbi wengine kupewa wazo na Wazungu na kulifanya lionekane kuwa Wamatumbi ndio progeniture wake!

    Amkeni, jamani!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2010

    HIVI TUNAWACHEKEA HAWA WAZUNGU WAMEKUJA NCHINI KWETU NA TUNAWAPA VIBALI VYA KUISHI NA KUFANYA KAZI HUKU SISI WANATUFUKUZA HAWATAKI WAGENI, UCHAGUZI WA JUZI TU UNITED KINGDOM ISUUE YA WAHAMIAJI ILIKUWA MBELE HAWATAKI KABISA WATU TOKA NJE YA EU COUNTRIES: THEY JUST STOP SHORT TO SAY THAT HAWATAKI WATU TOKA AFRIKA KUJA HAPA KWAO, HIVI SASA KUNA MAKUSUDI MAZIMA YA KUFUKUZA WATU WA KUJA WENGI TU KWA MTINDO WA KUNYIMA KUONGEZEA MUDA WA KUKAA HAPA WATU WENGI WANARUDI WAKINYIMWA VISA EXTENSION. CHA AJABU SISI TUNACHEKA NAO TU. WAKATI UMEFIKA SASA NA SISI TUSIWACHEKEE WAONDOKE WARUDI MAKWAO NA SISI TUSHIKE HIZO NAFASI ZA KAZI NYUMBANI KWA VILE WANATUFUKUZA MAKWAO. KAMA TUTAKATA MAHUSIANO NAO TUTAENDA CHINI, URUSI NA INDIA MARAFIKI WA KWELI KILA KITU KINAPATIKANA HUKO WALA HATUNA HAJA YA KUWAKUMBATIA TENA HAWA WABAGUZI, NA VIONGOZI WETU WAGANGAMALE WASIKAE KIMYA TU KWA VILE WAO HAWANA SHIDA WANAKULA NAO SAHANI MOJA WAIGE MFANO WA RAIS WA MEXICO ALIYEENDA MWENYEWE AMERIKA KUPINGA HATUWA YA JIMBO LA ARIZONA KUPITISHA SHERIA YA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU KWA MTINDO WA KUSIMAMISHA WATU BARABARANI NA KUWAULIZA VIBALI, HUO NI UKIUKWAJI WA HUMAN RIGHTS. HATA WA-USA WENGINE WANAPINGA HILO MFANO JIRANI ZAO WA JIMBO LA CARLIFONIA WANAPINGA HILO NA WANSEMA WATAWAKATIA UMEME KWA VILE UMEME MWINGI WA ARIZONA WANAPATA TOKA CARLIFONIA, NA WAMEWAAGIZA WANA-CARLIFONIA WOTE KUSUSIA KWENDA KUTEMBEA ARIZONA. WAZUNGU HASA WA-UK SI WATU NI VIATU

    ReplyDelete
  6. MsemakweliMay 23, 2010

    Mtoa maoni 03:03 tuliza jazba. kama huna kazi hapo UK fanya urudi au ungangamale mwenyewe kimtindo, oa au baki kihivyo . Usilalamikie wazungu kila mara, uliwafuata wa nini huko kwao si ungebaki tu hapa TZ na kazi ungepata hapa hapa bwana, Acha masinyongo na mtima nyongo.
    Rais wa Mexico ni lazima aende US, kwani ana-wanachi karibu zaidi ya nusu ya TZ (15 millioni) wako kule, wakifanya kazi na kutuma fedha kwao. Nchi yake inategemea fedha zao hao jamaa kama vyanzo vya fedha.
    Nyinyi hapo Uk, labda waTZ 5000 tu, na katika hayo ni wewe na wenzako ishirini ndo mnajengea chuki zisizo na usomi wala fikra dhidi ya watu walioko TZ wa rangi nyingine.
    Tuliza ball, kama maisha hayakupangwa kwa ajili yako UK, basi zaa na watoto wako watakushukuru sana kwa kuwa raia wa UK baadaye.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2010

    Wadau mbona mpo negative sana? Ulizeni mueleweshwe, Goat Races ni kwa ajili ya kupata funds za kusaidia charities nyingi hapa Tanzania, hata CCBRT naamini imewahi kupata msaada kwa makampuni yanayoendesha Goat Races, mwaka jana Goat Races iliraise milionii mia moja na ushehe ambazo zote zimesaidia shughuli za maendeleo hapa nchini na hata taarifa ya matumizi yake wametoa, tafuta kijitabu cha Goat Race uone mwenyewe.
    Kama tunapewa misaada na sisi wenyewe wa-Tanzania hatupeleki kwa walengwa sasa tatizo ni hao wazungu wanaofanya shughuli ya kukimbiza mbuzi na kutupatia milioni mia moja yetu wenyewe wa-Tanzania halafu sisi tuache kuifanyia kazi na kuwalaumu wao?
    Kukimbiza mbuzi nadhani hata enzi za mababu zetu kulikuwa na michezo kama hiyo, kama nchi za kiarabu wanavyokimbiza ngamia... acheni visa wabongo, maendeleo tunayarudisha nyuma wenyewe!

    ~Kidawa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2010

    upuuzi kwanini wasi organize mbio za watoto yatima? sisi mbuzi tunakula si pets!
    Mdau ktk majonzi

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2010

    Mbuzi namba nane, (wa kwanza kulia) yuko ofside trick.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2010

    acheni kulalamika ovyo lipi jema kwenu?? kama hujapata makaratasi kaa mkao wa kurudi kwenu ulipofika huko ulipo ungeanza shughulikia mapepa kwanza mnajisahau na kujiona mko juu na bado fyekeo likipita tu mnalo ndio mrudi bongo muone wenzenu wanavyofanya mambo na sio kutwa kuuza sura kwenye mablogu na wewe unayedai ati watoto yatima wakimbie sijui ushuzz gani umewahi hata kuwapelekea pipi gololi?? mbio za mbuzi ni mchezo kama michezo mingine tembea uonee wewe kuna mashindano hadi ya miss mbwa utajijeijei

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2010

    Nawashauri wale wasiopenda mashindano ya mbuzi waanzishe mashindano ya konokono au bata kuchangia charities wanazozitaka. Kama unapenda kitu kifuate, kama hukipendi kiache! Pilipili usiokula unakuwashia nini???

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2010

    "wewe unayedai ati watoto yatima wakimbie sijui ushuzi gani umewahi hata kuwapelekea pipi gololi"
    We uliepinda, unaeshabikia upuuzi wawazungu hapo ulipo usijichanganye hao wazungu wanawa enjoy tuu tulia fikiria alafu wacha comeent zako usipagawe... unafikiri wakumaindi wewe na wenzeko weusi mkaa?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2010

    NAMUUNGA MKONO MDAU ALIYEZUNGUMZIA
    JUU YA MANYANYASO YA BAADHI YA NCHI KWA WAAFRICA,JAPANI NAYO INAONGOZA,MISAKO NA KUULIZWA VITAMBULISHO KILA KUKICHA,PIA WAAFRIKA WANABAGULIWA SANA HATA SEHEMU ZA KAZI NK.KWA MTU ALIAYEWAHI KUISHI JAPANI ATANIUNGA MKONO KWA HILI,JAPANI NAYO IMULIKWE
    KWA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU NA KUBAGUA WEUSI HASA KUTOKA AFRIKA.
    MDAU JAPAN.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 23, 2010

    Japani pia inaongoza kwa ubaguzi
    hasa kwa weusi toka Afrika wanaongoza pia kwa kukiuka haka za binadamu,misako kila siku,kuulizwa
    vitambulisho na kugongewa milango mara kwa mara,pia majirani kwaitia
    polisi foreighners bila sababu za msingi,kwa aliyewahi kuisghi Japanai ataniunga mkono kwa suala hili.
    mdau Japani.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2010

    Sema msemalo mie mbio za mbuzi nazifagilia wawaaaaaaaa. Adumu Bwana Paul Hicks.

    Mnajua wa Tz tusiende mbali:mara japan mara wapi..... ubaguzi kila binadamu anao, hata watanzania tunabaguana wenyewe kwa wenyewe. Hapa sioni kama ubaguzi ni issue kuuubwa! Hapa tuangalie mbio zenyewe. Mie binafsi huburudika sana siku hiyo. Ni kama outing ya aina yake. Wanaolalamika ni wale ambao hawajawahi kuhudhuria . Ila cha msingi ni kujiuliza : je! zile hela zinazopatikana kweli zinawafikia walengwa?

    Endelea Paul, tuletee hata mbio za vipepeo tutaruka tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2010

    sijapinda kama unavyodhani kilaza wewe tumia oblangata yako mmezoea kukejeli kila kitu anzisha hayo mashindano ya watoto yatima tukuone unahara na mdomo tuu vile domo lako halilipiwi vat walichofanya hao wazungu ni sawasawa na wamejimix na wabongo sio mnakurupuka tu ka vibaka nakuanza kuandika pumba hapa na hizo hela zinaenda kwa hao hao watoto yatima happy blue monday!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...