mawili kati ya maboti matano ya maharamia wa kisomali yaliyokamatwa na meli ya vita ya Uhollanzi HNLMS Johan de Witt katika bahari ya hindi hivi karibuni wakati ikiwa njiani kuja Dar inakofanya ziara ya siku tano. Katika tukio hilo askari wa meli hiyo walikamata mafuta ya dizeli, petroli na vilainisho vingine kiasi cha lita elfu kumi ambayo yalikabidhiwa kwa JWTZ.

askari wa majini wa uholanzi wakiwa bandarini Dar wakitelemsha mafuta ya maharamia waliyokamata maji makuu katika bahari ya hindi

Kamanda wa meli ya vita HNLMS Johan de Witt kepteni Ben Bikkering akitoa maelezo kwa balozi wa uholanzi nchini (kulia) na afisa mwingine bandarini dar leo



Kepteni Ben Bikkering akimkabidhi Afande Omar wa JWTZ nyaraka za makabidhiano ya mafuta hayo leo bandarini Dar

Kepteni Ben Bikkering akiongea na wanahabari.


Tatizo la maharamia wa Kisomali kuteka meli karibu kila siku limekuwa sugu kiasi ya kwamba nchi kadhaa zimeanza kujipanga ili kuwashughulikia. Tatizo hata ukiwakamata maharamia hao utawashtaki kwa kifungu cha sheria ipi na ya nchi gani?






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2010

    SAFI SANA WADACHI BIG UP

    mdau wa mahakama kuu ya dunia uholanzi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2010

    HAKUNA BIG UP HAPO KWANZA WANAKIUKA SHERIA NA TANZANIA WANAWAACHIA BANDARI YETU SIE HAPO PIA TUNATAKIWA KUWA KAZINI NA KUWAFAHAMISHA WAO SIO WAO WATAWALE HIYO BANDARI? JE YETU YAKITOKEA? WANAWAACHIA MABAHARIA WETU WAFANYE KAZI KWA KUTAWALA BANDARI YAO?.

    ReplyDelete
  3. Afande Mwamunyange JAMBO AFANDE!

    Nakushauri msipokee hayo mafuta. Au mkiyapokea msiyatumie kwenye vifaa vyenu-magari, vifaru nk.

    Hamuwezi kujua usalama wa hayo mafuta kama ni safi au ya kuungaunga kama yale wanayoiba vibaka kwenye malori ya mafuta na kutia kwenye mifuko ya Rambo.
    Maana yamenyang'anywa toka kwa maharamia ambao hawana tofauti na hao vibaka wetu tu.

    Huwezi kujua utunzaji wake ulikuwaje.

    Kama sio salama yataharibu mitambo/magari yenu yote. Kumbukeni Bure/Nafuu ni GHALI.

    Wao waholanzi bado wana safari ndefu kwa nini wasiyatie kwenye meli yao?

    Huu ni ushauri kwa nia nzuri tu na wala sio wa dharau kwa watu waliyotupa zawa.

    Au muyagawe kwa watu. Vifaa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    Mbona akiwa anaongea mbongo waandishi wanakuwa wengiii ila akiwa anaongea mtasha hawatoshi hata kwenye kiganja???

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2010

    Sasa hawa wadachi washatuchonganisha na hao maharamia. Wakijua kuwa tumepewa haya mafuta, tujiandaeni kwa lolote kutoka kwa wasomali. Nihayo tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...