
Picha na Habari na Albert Sengo
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Leonard Bandiho Bihondo (64) amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Mwanza jana na kusomewa shitaka la kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya kada wa CCM Marehemu Bi. Bahati Stephano.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Mkoa, Yujnia Rujwahuka ndiye aliyemsomea mashtaka hayo. Kesi imeahirishwa hadi itakaposomwa tena tarehe 4 Juni 2010.
Bihondo. alikamatwa Jumatano jioni katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea jijini Dar es Salaam, amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 10. Anahusishwa na maujai ya kiongozi wa CCM, kata ya Isamilo, Bi Bahati Stephano, aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani akiwa ofisini kwake Ijumaa iliyopita.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Silo ananukuriwa kusema kwamba katika upelelezi wa mauaji hayo, polisi waliwahoji washukiwa watatu, ambao wote alisema wamemtaja Bandiho kuwa amehusika katika tukio hilo.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Mkoa, Yujnia Rujwahuka ndiye aliyemsomea mashtaka hayo. Kesi imeahirishwa hadi itakaposomwa tena tarehe 4 Juni 2010.
Bihondo. alikamatwa Jumatano jioni katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea jijini Dar es Salaam, amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 10. Anahusishwa na maujai ya kiongozi wa CCM, kata ya Isamilo, Bi Bahati Stephano, aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani akiwa ofisini kwake Ijumaa iliyopita.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Silo ananukuriwa kusema kwamba katika upelelezi wa mauaji hayo, polisi waliwahoji washukiwa watatu, ambao wote alisema wamemtaja Bandiho kuwa amehusika katika tukio hilo.
Kuuwawa kwa kiongozi huyo wa CCM kumekuwa kukihusishwa na masuala ya kisiasa hususan uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mauaji hayo ambayo yamelitikisa jiji la mwanza yalielezewa na Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Laurence Masha kuwa ni ya kinyama na yalitokea saa chache baada kukutana na kiongozi huyo wa CCM.
Suali, ufungaji wa pingu namna hii ni kwa watuhumiwa wa aina gani? maana nakumbuka mkuu wa polisi na wenzake walipokuwa wanatuhumiwa kuua walikuwa hawafungwi hata mashati pamoja
ReplyDeletekwa nini lakini? mzee mzima kama huyu kweli na anafamilia inayomtegemea anafanya jambo la kikatili kama hili? Muogopeni mungu jamani enyi viumbe
ReplyDeleteWatu wengi sana wamejiunga na CCM kutafuta Pesa na vyeo kwa njia zisizo safi. Kama mwaka huu kila ambaye anajijua ana kauwezo fulani kuanzia wasanii mpaka watangazaji wa radio/TV. Kila mwenye jina amejiunga na CCM. Sasa shughuli ipo kwenye kugombea hizo nafasi chache. Ukumbuke watu hawa hawana dhamiri (conscience) wala maadili kwenye kutafuta wanachokitaka. Tutarajie matukio mengi zaidi ya jinsi hii kuanzia sasa!!!!!
ReplyDeleteJamani huyu si ndio baba yake yule super model wa USA aiiiiii pole sana dada kwa kukutwa na hili janga
ReplyDeleteKama kweli anahusika na mauaji basi naye auliwe tu, there's no need for him ale na alale vizuri wakati kapoteza maisha ya mwenzie.
ReplyDeleteKAZI KUWAONEA VIDAGAA TU....MAPAPA HAYOOOO YANATAMBAAA NA TENA HATA KUPEWA NGUVU ZAIDI KUFUNGUA MMMMMHHHH SISEMI MENGI... WAMEUWA HADI LEO WANADUNDAA TU..NDIO KWANZA WANAPEWA CHANCE YA KUTAMBA...
ReplyDeleteKAZI YA CHAMA HAINA MAKOSA,KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,!!!!NA VIONGOZI
ReplyDeleteWAKE WOTE !!!????
ISOMEKE: MSHITAKIWA "MSTAHIKI" MEYA WA JIJI LA MWANZA.
ReplyDeleteSASA SIJUI ANASTAHIKI NINI NA NI MSHITAKIWA,KWA KUTUHUMIWA TU NA MAUAJI USTAHIKI UNAKOMA NA NI KAMA KIBAKA AU JAMBAZI- A COMMON CRIMINAL
He is innocent until proved guilty!
ReplyDeleteCynthia pole sana dada yangu na familia yako nzima kwa hii balaa. Nafahamu sana familia yako siamini macho yangu kwa hili jambo. Muombee baba yako mungu atawasaidia.
ReplyDeletewafanyasiasa mwanza waha style yake, mie nakumbuka enzi zile walianza kurushiana makonde pale makao makuu ya jiji baina ya madiwani wa chama tawala na yule mmoja wa chama cha cheyo. zikafuatia nyakati za tindikali, sasa wameingilia na syle ya visu, zamu ijayo itakuwa vya moto....ubabeubabe...maslahi kwanza wananchi kivyao
ReplyDeleteHuyu atakuwa na visa na mkubwa fulani, na kufungwa pingu ni makusudi kuwafanya mjisikie mnavyojisikia na kukanza kumdhihaki kabla hata kesi haijasikilizwa wala ushahidi kutolewe maana mmeshamuona ana kosa tayari!
ReplyDeleteAnony hapo juu uliyesema pingu ni kwa nani na nani kweli umeona hili vyema, maana wengine walikuwa wanapelekwa na ma-baloon na kuvaa kofia za pama tena baada ya kuua hadharani pale njia panda ya Kawe! Hatujasahau!
Siku ya mwisho yote yatakuwa hadharani.
Mungu Ibariki Tanzania!