TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION BANGALORE
INDIA (TASABA)
Mwaka wa kwanza – USD 3650
· Maka wa pili - USD 1250
· Mwaka wa tatu - USD 1250
NB/ MFUMO HUU WA ADA NI KWA MASOMO YOTE ISIPOKUWA KOZI ZA SHERIA NA UDAKTARI.
GHARAMA ZA MAKAZI.
· Kodi ya nyumba kwa mwezi – USD 90 – USD 150
(KULINGANA NA SEHEMU)
NB/ Mfumo wa kupanga nyumba ni tofauti kidogo na sehemu nyingi. Unapotaka panga nyumba inabidi uweke dhamana ambayo huwa ni kodi ya miezi 10 mf: kama kodi ni USD 90 kwa mwezi inabidi uweke dhamana ya USD 900 inamaana (kodi x miezi 10) pesa hizi huwa zinarudishwa pale mkataba unapoisha.
· Gharama ya kununua vitu vya ndani kwa kadirio la kawaida ni –USD 500
· Gharama ya matumizi ya kawaida si chini ya USD- 100
Gharama hizi ni kwa ajili ya Bangalore tu.Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi pale inapotakiwa tafadhali wasiliana nami :
Fidelis Msomekela – mwenyekiti (TASABA)
Mob: +919742176980
E-mail: marshallza@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    kwa garama hizo lol, better niende ulaya hata nikipata kazi ya kufagia mtaa pesa italipa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Unamaanisha nini? kwa kusema garama za kununua vitu vya ndani 500, matumizi ya kawaida dola 100? changanua vitu kama msomi. au?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Kwani kubeba boksi huko hamna?vyumba vya kulala mzungu wa K kama mlimani je?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    hehehehe, kumekucha kumekucha bangalore, jamani msije India kunatisha hasa kwa ss waafrica. Vijana nipo india hyderabad kazi kwako

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    inasikitisha kuona kiongozi kama unavyojiita kutoa tafarifa potofu na za uongo kama hizo .

    pili naomba uchanganue vizuri na kuelezea hasa nia na madhumuni ya kuweka taafifa hizi kwenye mtandao .

    siku chache zilizopita Bangalore wametokea matukio mengi kwa sisi watanzania, mfano kuwawa kwa mwenztu kikatili , watu kuchomewa nyumba na juzi tu mtu kapigwa bila sababu .

    na bila aibu na kukosa kwako akili (mwenyekiti) ukishirikiana na wapumbavu wa ubalozini mkaamua kuwaachia wahusika waliotaka kuchoma watu ndani mwao, unaweza ukatuelezea sababu ya kufanya ivyo ?? je msaada usingipatikana tungekuwa tunaongea nini leo hii ? au we haujasikia matukio haya ? ni kwa sababu ya watu kama nyie ndio maana watanzania tunapata mataizo uku kila siku , mnasema maswala ya kidiplomasia , na tukio la watanzania kufunywa Mysore haulijio au diplomasia ni kwa wahindi na sio sisi ?

    haya ndio mambo tunayotaka kuyasikia sio kuingilia maisha binafsi ya watu , najua utasema unasaidia wanafunzi wanaotaka kuja ,kila mtu kabla ya kuja India huwa ana mtu anayemfahamu uku kwa njia moja au nyingine , sasa nashindwa kuelewa nia yako hasa ni nini ,

    au umesahau India haupo peke yako , elezea basi bei ya kitanda, usafiri , chakula n.k , unakuwa kama sio msomi na bado unanijiita kiongozi .

    p.s let it pass Mr. MICHUZI , ili ujumbe ufike.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2010

    kaka mi nalipa usd 2500 kila mwaka. samani ni mzazi ndio anatuma na anajua naishi vp Bangalore. pole kwa kupoteza muda..

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2010

    Mwenyekiti naona umechemka unamuda mwingi sana mkononi. Mitihani imeisha ukobored kidogo au...Kabebe box kidogo kama ama nenda gym.

    Hayo mambo ya kuweka bei huku za watu na kuwapangia watu hela ya kula kwa mwezi sio mazuri. Utawaharibia watoto wa baba. Ukishaweka hii hela wengine wakiomba hela wataambiwa niliona kwa Michuzi hivi na vile....

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    Huyu mtu nadhani analipwa kwa kila kichwa anachopeleka kwenye vyuo vya kizushi...! hamna kitu hapa, anazunguka zunguka tu na maneno

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    KIONGOZI HAPO UMETUANGUSHA NAZANI UNA MENGINE UNAYATAFUTAAA KWANINI TUKUPIGIE WEWE SIMU?..HUUU SIO UONGOZI KABISAA HATAA MANENO YAKE YAMEKAA KITAPELI TAPELI JAMANI TUMUOGOPE MTU HUYU CHONDE CHONDE TUWENI MACHO YASITUKUTE MAMBO YALE YA DECI MKALIZWA JAMANI MAISHA MAGUMU SASAIVI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2010

    awa ndo viongozi 2liowachagua inaonyesha ni jinsi gani uwezo wao wa kufikiri umefikia mwisho.badala ya kuongelea mambo ya msingi kama kiongozi ameamua kuingilia maisha ya watu binafsi mbona yeye matumizi yake sio ayo alioandika.kila siku tumbo lina mtoka je ni kwajili ya iyo dola 100?ama kama anataka kufanya admision kwa style hii ili watoto wa watu waje kuteseka aseme tujue.umefuliiiiiiiiaaa bwege wewe jaribu kuangalia mambo ya kuandika ya msingi na maendeleo sio hayo sisi tulijua umegundua kifo cha ndugu yetu imrani kumbe unaandika upuuzi au kwa vile watu hawakualiki kwao ndio unaamua kuandika ivyo!!watu wamekukimbia kwa umbea raisi wa kwanza kuwa mbea bangalore ila sio wewe ni demu wako mwenye ukimwi amekuchanganya akili mpaka unaandika vitu vya ajabu!!!michuzi naona sasa watu wana tumia blog yako kufanya admision na umaarufu!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2010

    NDUGU WATANZANIA WEZETU NA WAZAZI WETU HUYU RAHISI WA TASABA ANA SAHAU KAMA KUNA UONGOZI ANA WEKA TAMAA MBELE KWANI KAMA KWELI NI MKWELI KWANINI KATAJA ADA YA CHUO KIMOJA AMBACHO ANASOMA YEYE!!!AU NI KWA AJILI YA IZO PESA WANAZOPEWA ZA ADIMSSION NDIO ZIMEMFANYA AANDIKE IVYO ILI WAZAZI WAONE MAISHA HUKU NI RAISI WAWEZE KUWALETA WATOTO ZAO WAZAZI KAENI MUELEWE KUWA YEYE ANAFANYA ADMISSION HUKU KILA AKILETA MTU MMOJA ANAPATA $500 NDIO ZINAFANYA ANZE KUCHANGANYIKIWA NA KUONGOPA KWA TAMAA ZA PESA AFIKIRII KUTESEKA KWA WENZAKE BAADAE YEYE ANAANGALIA UPANDE WAKE JE HUYU KIONGOZI AMA!!JAMANI WAZAZI ANGALIENI HILO SWALA HUYU NI KIONGOZI AMBAYE NI MBINAFSI NA NYINYI WANAFUNZI WENZETU WENYE TAMAA KAMA HIZO MUANGALIE!!!TUNAKUOMBA KAMA KWELI TUMEKUCHAGUA SISI MTUMIE MICHUZI HABARI ZA KUKANUSHA HABARI ULIZO ZIANDIKA NA KUSEMA NI TAMAA ZA PESA ZIMEKUFANYA UWE HIVYO JARIBU KUANDIKA VITU VYA MAANA KWANI JARIBU KUJUA HATA WAZAZI WETU NI WASOMI WANAELEWA MAISHA TUSIWE TUNAKANDAMIZANA KWA TAMAA ZA PESA!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2010

    unajua unashangaza jamii ndugu yaangu.Hizi ni hesabu za chuo chako na hostel yako ama ni matatizo tu unaleta.
    Maisha sasa yamepanda hata vijijini ila wewe upeo wako unaona hapa tu.Kiongozi usiyeweza kutofautisha uongozi na biashara unataka tukuelewe vipi.
    Post vitu vya maana basi vinavyogusa afya na ulinzi kwa watanzania sio gharama zao za maisha
    Estimation siku zote zinatakiwa zizidi hali halisi na sio pungufu kama unavyosema.
    Maisha yamepanda ndugu..fanya uchunguzi tena

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2010

    tupe maelezo kama msomi mwenyekiti.. je wewe ulitumia garama hizo ulipo kwenda huko?....mm kama mzazi na mwanagu hapo bangalore nanilimpeleka mwenyewe hadi chuoni kwake..chuo kinaitwa endo asian academmy kipo chini ya bangalore university na mpaka makazi nilimtafutia mwenyewe..bona ujaongelea swala la ma broker na malipo yao kwakikutafutia makazi? na shangaa hizi garama wewe mwenyekiti umezitoa wapi? because nilifanya research ya vyuo tufauti kabla ya kumleta mwanagu, je wewe umelinganisha garama hizo kwa maeneo yapi ya makazi..? kamanali ,hnoor ,acharya au tis pallya?..je adaa ya garden city college inalingana na maelezo yako?..rai kwa wazazi tuwe waangalifu na tujaribu kufanya reseach wenyewe kabla ya kuwapeleka watoto wetu huko..hali ya amani kwa wanafuzi huko nitata sana !!! wanapingwa wanyanyaswa bila sababu za msingi.. maelezo alioyatoa mwentekiti wajumuiya ni potofu si sahihi..hayo mahesabu yapo chini sana ukilinganisha na hali halisi ya mwanafuzi kujikimu kimaisha masomoni bangalore india..wazazi tuwe waangalifu na maelezo kma haya

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2010

    madalali hawajafurahi.....wanajaribu kubadilisha main idea....kwa kifupi hapa mwenyekiti anatoa mwongozo tu hajalazimisha mtu afuate na pia kama kawaida huwa una margin of error ndogo!.....Madalali mlizoea kula pesa za watu, poleni

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2010

    Nampogeza sana mwenyekiti kwa kutujulisha juu ya gharama, maana vijana wengi wamedanganya gharama na kuwaumiza wazazi wao.

    Tunahitaji viongozi kama wewe kwa maendeleo yetu.

    Hongera sana

    GJK

    nb. wanaolalamika wote ni wahuni watupu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2010

    Nashukuru kaka michuzi kwa habari unazoweza kutupa kutumia blog yako..
    Mi ninasoma hapa Bangalore nimesikitika sana kuona kama hawa viongozi ndio wanakuwa mstari wa mbele kupoteza watu na wazazi huko nyumbani na Watanzania kwa ujumla.
    Ndugu Watanzania ada hizo ni za uongo sana kwasababu mi mwaka wa kwanza nimelipa Dola 1000 na huu mwaka wa pili nimelipa ada ya dola 500.
    Watanzania hapa Bangalore kuna vyuo vinacharge bei ya juu sana lakini mfumo wa kusoma hapa ni kama wa huko shule za sekondary nyingi hapo nchini Tanzania ambazo zipo chini ya Baraza la Mtihani..
    College zote huku zipo chini ya Chuo Kikuu cha Bangalore na mitihani na usahishaji yanatolewa na chuo hichi cha Bangalore.
    Sasa mwenyekiti naona unataka kudanganya jamii kama wewe na uongozi wako kushirikiana na mwakilishi wa ubalozini mlivyotudanganya kuhusu kifo cha Ndugu yetu Imran Mtui , kwamba kajiuwa wakati aliuwawa.
    Nakuomba uache tabia ya kudanganya watu tena Watanzania kwa ujumla fanya kazi yako kama kiongozi na sio kutupelekapeleka na kupotosha jamii. Asante

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 20, 2010

    sorry to add, but it depends which college u go to. college start from 300usd to 5000usd just for business and arts studys... apart from that not only B.Sc and law cost alot but some other courses too. my parents pay approximately 4000usd/year. and im not doing any of the above course.
    please be specific in your details.. do the research and put it up in the tasaba blog... i mean i think i got more info than what u have on colleges.. also there are other universities in bangalore that you can do the course in why not mention those too.

    Also why not tell people bout the Masters programmes... cuz they cost from bout 5000usd/yr - 20000usd/pr.

    The living standards in bangalore are quite high compare to any other city in southern india. Houses start fro 100usd (1bhk) to bout 350usd(2bhk). but depending on the area these costs are subjected to change. For the inside stuff the cost of everything has gone up so i wouldn't say 500usd is enough. Pocket money for bangalore students shud start from bout 200usd onwards.

    Any how all i wana say is that get your facts straight before you put em up on the net or anywhere else.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2010

    Hebu nipe ukweli ,mimi niko mbioni kwenda huko kimasomo. Nyote hapo juu mmenichanganya.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 21, 2010

    kwa kweli sasa mnachanganya sana sasa mdogo wangu haji tena huko uchawi mtupu hapa nani mkweli? anyway canada vyuo vya kumwaga tena viko kwenye rank ya vyuo bora duniani ataenda huko

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 21, 2010

    kaka kuishi kwako manzese usifananishe na mimi nayeishi masaki.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 21, 2010

    Mr president,i would like to clarify on your statement concerning fees structure.

    please just tell the world that maybe you were mislead by whoever you gave him/her the research job of the Tanzanians living in Bengaluru.hizo gharama zako mbona hazieleweki kenge wewe,yaani dola ngapi???sasa kingfisher moja ni kiasi gani unataka watoto wa watu wasile vyombo???hembu kanusha watu wale maisha kwa raha zao.
    Auto na mita za uwizi umeziwekea gharama ama watu wanatembea?au wote wapande BMTC?wapate TB na Leprosy?to be honest i am shocked by this news sasa unataka wazazi waelewe vp?just be a man na waeleze tuu njaa ilizidi akili na nia haikuwa kama ilivypokelewa na wtu watakusaidia tuu kupata wanafunzi na utaendelea na maisha mheshimiwa otherwise it is a shame to post such unauthentic information while you know that people nowadays do believe in whatever they read so be a man and stand up and apologize for such a wrongful act we will sue you for defamation yaani mimi nalala kwenye nyumba ya dola 90 ni ipi ni zile za juu kabisa kwenye roof top au?guys lets be serious if we do not have things to post just do something else hata ukiamua kuwa bouncer club italipa tuu maisha kokote..tubadilike tafadhali na sema ukweli..

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 21, 2010

    Wewe anon. wa Fri May 21, 11:11:00AM, yaani umewaza umewazua na umehitimisha kuwa Canada is next to India, kachori za bure wewe! Unajua unaongelea nini lakini? Jamba jamba mkubwa!

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 21, 2010

    huyu jamaa kapata wap mda wa kuandika kipind cha mitihan au hasom

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...