Mkuu wa chama cha wanawake wanacheria Tanzania (TAWLA),Maria Kashonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutuna na waandishi hapo uliofanyika leo.kulia ni mjumbe wa chama hicho,Sakina Simba.
Mkuu wa chama cha wanawake wanacheria Tanzania (TAWLA),Maria Kashonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano ulioitishwa leo katika ukumbi wa idara ya habari -MAELEZO,kuhusu kuadhimisha miaka ishirini (20 yrs) ya utetezi na kuunga mkono haki za Wanawake na watoto.maadhimisho hayo yatafanyika siku ya tarehe 10 Mei,2010 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Katika sherehe za maadhimisho hayo TAWLA itaungana na Rais Jakaya Kikwete. Pia katika kuonyesha mafanikio yake TAWLA watakuwa na maandamano ya amani kuanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Viwanja vya Mnazi mmoja. Pia kuzindua mkakati endelevu 2010-2014. Vilevile mnamo tarehe 10 Mei 2010 itatoa Msaada wa kisheria katika viwanja hivyo na kuendelea kwa wiki nzima kaunzia 11-14 Mei ,2010 kutoa huduma sehemu za Bagamoyo,Temeke(ofisi za UMATI)na TAWLA ofisi ya Ilala Shariffu Shamba jijini Dar es salaam.(Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...