Bw. Laurence Mato aliyekuwa mshereheshaji akiwajibika
Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Mhe. DK. Marwa Mwita Matiko, wa kwanza kushoto akizikiliza maoni ya wajumbe.
Uandikishaji wa wana UTARWA ukiendelea.
sehemu ya wana UTARWA wakisikiliza hotuba kwa makini
sehemu ya wana UTARWA wakisikiliza hotuba kwa makini.
Wajumbe wakifuatilia marekebisho ya katiba ya UTARWA

Mkutano wa Umoja wa Watanzania waishio Rwanda, ulifanyika katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, uliopo eneo la Nyarutarama, jijini Kigali. Mkutano huu ambao pia ulikuwa mkutano mkuu wa uchaguzi, uliitishwa na kusimamiwa na mheshimiwa balozi wa Tanzania nchini Rwanda Dr. Marwa Mwita Matiko, siku ya tarehe 08/May/2010.
Mkutano huu ulikuwa ni kilele cha juhudi za siku nyingi, za Watanzania waishio Rwanda, za kutaka kuwa na chombo kinachowaunganisha wa kama watanzania waishio nchini Rwanda, bila kujali tofauti za shughuli zao zilizowafanya kuwepo nchini Rwanda. kimsingi kumekuwepo na mikutano mingi huko nyuma hadi kufikia kufanikiwa kwa mkutano huu mkuu.

Madhumunio ya umoja huu ni pamoja na Kuwaunganisha watanzania waishio Rwanda katika shughuli za kukuza mahusiano mazuri kati yao na wenyeji wananchi wa Rwanda, Kusaidina katika maswala ya kijamii ya majanga au maendeleo, Kuhamasisha Watanzania kushiriki kwa bidii na kutumia fursa nzuri za Kibiashara ndani ya Rwanda na kati ya Tanzania na Rwanda, Kubadilishana taaluma mbalimbali, Kupeana habari za nyumbani Tanzania, na kushiriki kuchangia uchumi wa Tanzania, kwa kushirikiana na taasisi au vyombo husika, Kushiriki katika utekelezaji wa sera za Tanzania, Rwanda na Afrika Mashariki kwa ujumla, kama sehemu ya diaspora, Kubadilishana taarifa za kijamii, Kiuchumi na maendeleo ya siasa safi za nyumbani Tanzania na zile za Rwanda nakadhalika, kama zilivyoainishwa katika Katiba ya UTARWA.

Mkutano huu ulichagua viongozi wa UTARWA kama ifuatavyo:- Mwenyekiti- Bibi Josephine Marealle Ulimwengu, Makamu mwenyekiti ni- Bw. Stephen Thambikeni, Katibu ni Bw. Elias P. Maigeh, na Makamu wake ni bw. Suleiman Everest Mziray; Mweka Hazina ni Bibi Hilda Shayo, na msaidizi wake ni Bibi Judith Elimhoo Mziray.
Walichaguliwa pia Wajumbe wa kamati ya utendaji, wanaowakilisha makudi mbalimbali kama ifuatavyo:- Kundi la kinamama, ni Bibi Rebeka Ruzibuka, kundi la wafanyabiashara ni Bw. Nurdin Mohamedi Chombo; na kundi la wafanyakazi alichaguliwa Bibi Petty Mloka Mbago. Kundi la wanafunzi, halikuwa na muwakilishi aliyehudhuria mkutano huu, hivyo mwakilishi wao atachaguliwa baadaye.

Katika hotuba yake Mhe. Balozi Dr. Marwa Matiko, alisisitiza umoja huu ukuze ushirikiano wa jadi ambao watanzania wanao, na kuhamasisha watanzania waishio Rwanda kutumia fursa nzuri za kibiashara zilizopo Rwanda, na kuhamasisha Watanzania kutoka nyumbani, kuja na kufanya biashara Rwanda, kama wafanyavyo wenzetu wakenya na Waganda. Hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania imepakana kabisa na Rwanda, na sasa miundo mbinu ya barabara imekuwa nzuri sana, ya kiwango cha lami, na kufuatia makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashriki kuwa na ushuru wa forodha mmoja na nafuu, hatuna budi kutumia fursa hizo kuleta bidhaa za kilimo, hasa chakula, na bidhaa za viwandani kama za vinywaji, vyote vinazalishwa kwa wingi na bora nchini kwetu, na vina soko kubwa nchini Rwanda. Alikumbusha kuwa Ubalozi utakuwa mstari wa mbele kutoa ushauri wa kiuchumi na za kiutendaji ili kurahisisha uelewa na taratibu husika katika kuendesha biashara kati ya nchi hizi.

Aidha allikumbusha watanzania waishio Rwanda, kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi mkuu wa Raisi na Wabunge, nchini kwetu, hivyo kwa wale watakaopata nafasi ya kuwa nyumbani wakati huo, basi washiriki vyema katika uchaguzi. Vile vile nchini Rwanda pia mwaka huu ni wa uchaguzi wa raisi na wabunge, hivyo aliwaasa Watanzania waishio Rwanda kuwa makini hasa kwa usalama wao, kwa kupunguza matembezi yasio ya lazima nyakati za usiku, kutojihusisha na makundi yoyote ya harakati za kisiasa au kuepuka kuwepo kwenye mikusanyiko ya kampeni za kisiasa za ndani ya Rwanda, kwani hazituhusu.

Nae Mwenyekiti mpya wa UTARWA, Bibi Josephine Marealle Ulimwengu katika hotuba yake ya shukrani, alimshukuru Mheshimiwa balozi Dr. Marwa Matiko, kwa juhudi zake bila kuchoka hadi kufanikisha kuzindiliwa kwa Umoja huu., aidha aliahidi kupitia viongizi wote waliochaguliwa, kuwa watashirikiana vizuri na watanzania wote wanachama na hata wale ambao hawjajiunga, ili kutekeleza changamoto zote alizotoa Mhe. balozi katika hotuba yake.

Vile vile, alisisitiza kwa Watanzania, kutumia taaluma zao kuwa mabalozi wazuri nchini Rawnda, ili kukuza picha nzuri ya watanzania kwa Rwanda, na hivyo kuongeza soko la watanzania katika kuwekeza taaluma zao nchini Rwanda, ambako kuna soko la taaluma mbalimbali. Vilevile, aliwashukuru wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Tanzania Rwanda, kwa ushirikiano wao wanaoutoa, wakati wote wanapohitajika, hivyo watanzania tunajivunia ukarimu na utendaji mzuri wa ubalozi wetu. Alitoa changamoto kwa watanzania wote kuwa tuchangamkie fursa na mazingira mazuri ya kibiashara nchini Rwanda, na pia kupeleka nyumbani utamaduni wa utendaji mzuri na uwajibikaji Rwanda na taasisi zake, na kuiga mwenendo mzuri wa uaminifu tunaoushuhudia kwa watendaji wa Rwanda, kama katika nyanja za usafi na mipango miji.

Wana UTARWA waliitikia wito na changamoto za Mhe. Balozi Marwa Matiko, na za mwenyekiti UTARWA, na kuahidi ushirikiano. Baadae kulikuwa na tafrija kwa wana UTARWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2010

    Mjifunze kwa Kagame jinsi ya kuendesha nchi...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2010

    udumu ushirikiano wa nchi zote mbili rwanda na tz majirani zetu sote ni waana wa africa .idumu EAC idumu jumuia ya madola.chapeni kazi kwa bidi msikwepe kulipa kodi karibu tena rwanda.

    mdau kigali makazi boxini kusaka chake

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2010

    Hayo ndio mambo yanayotakiwa sio mashina ya CCM kila kukicha..

    Tujifunze mambo ya mshikamano tukiwa nje ya nchi wote ni watanzania nje ya nchi sio mambo ya wanachama wa ccm, wanachama wa hivi na vile

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...