Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Jaji Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na wajumbe wa tume hiyo katika sherehe zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wajumbe wa tume hiyo ambao pia waliapishwa ni pamoja na Jaji Hamis Msumi na Ndugu Gaudios Tibakweitira.Pichani Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kupokea miongozo ya kazi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Tume ya Maadili ya uongozi muda mfupi baada ya kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto ni Jaji Hamis Amir Msumi,Ndugu Gaudios Tibakweitira na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2010

    Tanzania hatuna wasomi wengine zaidi ya hao??? Hawa si wanastahili kupumzika sasa wapishe vijana. Wasomi wetu wanaograduate kila siku watashika nafasi hizo lini???? Toka tukiwa wadogo hadi sasa tunazeeeka majina ni hayohayo, ajira kwa vijana wasomi iko wapiii???!!! Mungu tusaidie TANZANIA yetu iwe na huruma kwa vijana watakuwa machinga hadi lini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    TANZANIA HATUHITAJI TUME YA MAADILI KWANI HAIJALETA TOFAUTI YOYOTE YA KIUTENDAJI KWA VIONGOZI, HEBU TUANGALIE NYUMA, WAZIRI MKUU ILIMCHUKUA ZAIDI YA MIAKA KUTANGAZA MALI ZAKE KITENDO AMBACHO KILIKUWA NI UKOSEFU WA MAADILI LICHA YA VYOMBO VYA HABARI KUMSIFU BADALA YA KUHOJI ALIKUWA WAPI MUDA WOTE; SASA HUYO NI KIONGOZI WA JUU SERIKALINI AMBAYE ANGEKUWA NI MFANO KWA WENGINE. TUKIANGALIA MAWAZIRI NA VIONGOZI WENGINE UTENDAJI WAO NI UNAOTIA MASHAKA WENGI WAO HUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUENDESHA SERIKALI! NA MAMBO MENGINE MENGI TU YANAYOONESHA UDHAIFU KIUTENDAJI KWENYE VYOMBO VYOTE SERIKALINI.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    RECYCLING!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2010

    Tume ya maadili inachaguliwa mwishoni kabisa mwa awamu ya utawala wa raisi ili ifanye!!!!!!???????

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2010

    Wazee tu na majina ni yale yale tu yanachosha, ndio maana tunarudi nyuma. Mfano mzuri ni Bodi za ATC na TANESCO ziliwekwa watu walioharibu siku za nyuma, basi wakaendeleza kuyaua mashirika haya muhimu. Tuwe tunaangalia damu mpya mawazo mapya, mbinu mpya na mikakati mipya.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2010

    mzee Tibakwitira enzi ya mwalimu.wapi Jovin na Edgar ?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2010

    Reclycling!!! Daaah nimelipenda hili neno. The same old politics.Wastaafuu tuuuu. No future for new generation....

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2010

    NCHI HII BWABNA...HEBU WAC=HEKI HAO WAZEE ,HIVI WATAFANYA NINI??

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2010

    recycling ni nzuri ila si kwa akili na kazi za watu.Daaah hii inaitwa "Ulaji"

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2010

    Ndugu zangu watanzania, huu ni utamaduni wetu, na tutaendelea kuudumisha! Wawe wazee au picha hayo yapo nje ya katiba.

    JayK.

    ReplyDelete
  11. jovin yuko Pennslyvania na Edgar Washington DC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...