Mpiganaji Athumani Hamisi ambaye alikuwa matibabu sauzi kufuatia ajali ya gari mwaka jana akipokea maua toka kwa Bi. Mwanakombo Jumaa, mpiga picha na afisa habari mwandamizi wa MAELEZO alipotua jijini Dar leo jioni na kupokelewa na umati mkubwa wa wapiga picha wa habari, ndugu jamaa na marafiki wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu, Kaimu Mhariri mkuu wa Daily News na HabariLeo Mkumbwa Ally, Mhariri Isaac Mruma, baba yake Athumani, Mzee Hamisi Msengi na wadau wengine kibao.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamuakimpokea Athumani Hamisi kwa furaha
Athumani Hamisi akiwa na Baiskeli ya umeme anayotumia akiongoza umati uliojitokeza kumpokea
Mhariri Isaac Mruma akimpokea maua Athumaniambaye kaja na nesi maalumu (wa pili shoto)
Mwenyekiti wa Chama cha Wapiga picha za habari Mwanzo Millinga akimkabidhi Athumani Hamisi kadi maalumu iliyosainiwa na wapiga picha wote kumkaribisha nyumbani
Baba Mzazi wa Athumani Hamisi mzee Msengi akimpokea mwanaekumtia machoni rafiki yakeMatina Nkurlu wa Vodacom na dada yake (shoto)
Mpiga picha mkuu wa Globu ya Jamii Francis Dande akimpokea Athumani Hamisi
Ankal akirekodi ujio wa Athumani Hamisi akitumia FlipVideo
athumani akielekea kupanda ambulance iliyokuja kumpokea
Mpiga picha mkuu wa Globu ya Jamii Francis Dande akimpokea Athumani Hamisi
Ankal akirekodi ujio wa Athumani Hamisi akitumia FlipVideo
athumani akielekea kupanda ambulance iliyokuja kumpokea..
Athumani akiingizwa kwenye ambulance kabla ya kuelekea nyumbani kwake ambako atahudumiwa na nesi maalumu aliyekuja naye kutoa mafunzo yamwezi mmoja kwa mtu atakayemhudumia wakati wote. Mpiganaji Athumani Hamisi, pamoja na kuwa amepooza mwili mzima, ameonesha ushujaa wa aina yake kwa kuweza kumtambua kila aaliyemuona na kuongea naye kwa ucheshi wake wa kawaida. Globu ya Jamii inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kumuombea apate nafuu na kurejea katika ulingo wa mapambano ya habari.
Athumani akiingizwa kwenye ambulance kabla ya kuelekea nyumbani kwake ambako atahudumiwa na nesi maalumu aliyekuja naye kutoa mafunzo yamwezi mmoja kwa mtu atakayemhudumia wakati wote. Mpiganaji Athumani Hamisi, pamoja na kuwa amepooza mwili mzima, ameonesha ushujaa wa aina yake kwa kuweza kumtambua kila aaliyemuona na kuongea naye kwa ucheshi wake wa kawaida. Globu ya Jamii inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kumuombea apate nafuu na kurejea katika ulingo wa mapambano ya habari.Habari ya Ajali hiyo
BOFYA HAPAAisee Michuzi,
==============================================
==============================================
Da! Ndugu yetu anasikitisha.
Nakumbuka maneno ya muuguzi mmoja wa Muhimbili, Sept. 2008, nilipokwenda kumwangailia wakati nikiwa mjini hapo, akaniuliza, ni ndugu yako, nikamwambia ndiyo. Akasema hali hii kubadilika itakuwa vigumu kwa kweli. Yaani mshikaji anaonekana hawezi hata kuegemea mwenyewe kwenye kiti? Ehe! Hii adhabu sijui amepewa ya nini? Huwa tunayaona haya lakini likimfika unayemjua, da! Linauma.
Hivi yule dada uliyemtoa mara ya kwanza mshikaji alipolazwa hospitali, kwamba ni mchumba wake, amepotelea wapi jamani?
Ila, labda uzungumze na vijana wako kwenye chama, kwamba ifanywe harambee mjini hapo ya kumchangia fedha walau ajengewe nyumba itakayokuwa na mpangilio mzuri wa yeye kuishi, yaani milango mipana, sakafu iliyonyooka, choo maalum, sehemu za kupumzikia, n.k. Hata ikiwa Salasala sawa tu. Kiwe kitu kikubwa cha kuwa na mgeni rasmi kama JK au Pinda na watu nguvu wenye vijisento vyao.
Lakini ili asionekane kama anapendelewa peke yake, itolewe mifano ya wengine ambao jamii iliwahi kuwasaidia, mfano yule dada wa Tabora asiyekuwa na mikono na yule mama aliyezaa watoto watatu wenye vichwa (ashakumu si matusi) vya kipanya.
Jingine, huyu awe Balozi wetu wa kitaifa wa kupambana na ajali za barabarani (ingawa nasikia ishu ilikuwa sms - isije kuwa na huyo Martina Nkurlu - hili ni jungu au kweli?). Anahitaji ushauri kwa kweli.
Shukurani, wasalimie washikaji.
Matinyi.
Nakumbuka maneno ya muuguzi mmoja wa Muhimbili, Sept. 2008, nilipokwenda kumwangailia wakati nikiwa mjini hapo, akaniuliza, ni ndugu yako, nikamwambia ndiyo. Akasema hali hii kubadilika itakuwa vigumu kwa kweli. Yaani mshikaji anaonekana hawezi hata kuegemea mwenyewe kwenye kiti? Ehe! Hii adhabu sijui amepewa ya nini? Huwa tunayaona haya lakini likimfika unayemjua, da! Linauma.
Hivi yule dada uliyemtoa mara ya kwanza mshikaji alipolazwa hospitali, kwamba ni mchumba wake, amepotelea wapi jamani?
Ila, labda uzungumze na vijana wako kwenye chama, kwamba ifanywe harambee mjini hapo ya kumchangia fedha walau ajengewe nyumba itakayokuwa na mpangilio mzuri wa yeye kuishi, yaani milango mipana, sakafu iliyonyooka, choo maalum, sehemu za kupumzikia, n.k. Hata ikiwa Salasala sawa tu. Kiwe kitu kikubwa cha kuwa na mgeni rasmi kama JK au Pinda na watu nguvu wenye vijisento vyao.
Lakini ili asionekane kama anapendelewa peke yake, itolewe mifano ya wengine ambao jamii iliwahi kuwasaidia, mfano yule dada wa Tabora asiyekuwa na mikono na yule mama aliyezaa watoto watatu wenye vichwa (ashakumu si matusi) vya kipanya.
Jingine, huyu awe Balozi wetu wa kitaifa wa kupambana na ajali za barabarani (ingawa nasikia ishu ilikuwa sms - isije kuwa na huyo Martina Nkurlu - hili ni jungu au kweli?). Anahitaji ushauri kwa kweli.
Shukurani, wasalimie washikaji.
Matinyi.



MICHUZI saa ingine kama una tongotongo machoni,wewemtu umesafiri sana lakini saa ingine bana,sasa flip video ndio nini si useme tu video tungekuelewa
ReplyDeletePole sana kaka yetu kwa kweli nimesikitika kaka michuzi kwanini hiyo video clip usingeiposti? simfahamu kaka yangu huyu ila nimesikitishwa na habari zake. Kama sijasahau siku za nyuma uliweka stori yake yeye pamoja na FRANCO MTUI ambae nilikuwa nae pamoja tukienda pati tofauti wakati wa likizo mwezi wa sita. Tafadhali endelea kutupa maelezo ya ndugu zetu tujue wanaendeleaje. Halafu huyo nesi ni msauzi je hapo nyumbani hatuwezi kufundisha manesi wetu wenyewe badala ya kuleta hao wa nje? Uko karibu na JK kamichu hebu ingiza hili swala tafadhali.
ReplyDeleteThanks, mdau massachussets.
Get well soon, bro. ama kweli watu wakikujia hivi machozi lazima yatakutoka manake unapatwa na moyo wa maisha. Simfahamu huyu kaka ila kwa kweli nimetokwa na machozi.
ReplyDeleteKamichu tupostie pia habari za pascal mayala, franco mtui na kaka yetu huyu tujue anaendeleaje. Ingekuwa vizuri pia ungetuwekea email au anuani yake kusudi tumtumie japo kadi za kumpa moyo. Kama sioni vizuri nahisi kaka yangu huyu kapooza mwili, ila nimeona kama anaweza kugeuka lakini mikono na miguu ndio haifanyi kazi. Kamichu eleza kwa kirefu habari zake.
Ni muda mrefu sana nilisubiri habari za kaka yangu hamisi kwa kweli leo nimefurahi kuona yuko mzima asante kamichuzi. Ila hujatueleza kama ni anaenda hospitali au amerudi nyumbani, mi ni nesi huku marekani najua ukipatwa na spinal cord injury huwa unahitaji vitu vingi sana, haswa msaada wa mtu kuwa nawe masaa 24. ungemfungulia accounti tukamwekea pesa kaka yetu manake msaada atahitaji kila kona.
ReplyDeleteGet well soon, and please dont give up, hang in there.
Pole sana Athumani, kweli hujafa bado hujaumbika. Mungu akutie nguvu. Mkewe mbona haonekani hapo kwenye picha?
ReplyDeleteKaka Mithupu mpe pole sana huyu jamaa Yetu. Mungu awe naye daima katika kipindi hiki kigumu kwake na familia yake.
ReplyDeleteWewe mdau wa Massachassutes unayeandika kwamba tu-train manesi wetu..umenifurahisha na wazo lako lakini vile vile nadhani wewe ni mnafiki. Kwani unadhani manesi hatunao? Wako wengi sana..ila ndo kama huyo mdau wangu hapo juu..wote ni manesi huko majuu.maana wanasema Mhimbili hakulipi. Na wala sina uhakika hao hao ambao ni manesi huko..ukiwaleta huku bongo watakubali kuwa manesi. So manesi wapo wengi..ila wanabeba box na kuhudumia wagonjwa wa kidhungu huko majuu.
Huyo anayeomba na. ya account eti atume pesa...hapo sina comment..lakini najua fika Michuzi ungeweka hiyo ukaunti hapa ungetukanwa..watu mnakataa kuchangia ndugu zenu waliokufa warudishwe home..ndo mtachangia jamaa huyu? Mdau kunradhi..siongelei wewe specifically..(perhaps you mean well) lakini in general..watanzania sisi tunapenda sana unafiki wa kujifanya na huruma...when we dont. perhaps cha muhimu..soma...kama una la kusaidia..fanya kimya..siyo kuleta hadithi zako hapa kwa Mithupu.
Namuombea ndugu Athuman apate nafuu.
Bongo zaidi ya uijuavyo wewe...
Mwenyezi Mungu yupo na kila mwenye kusubiri, kabla hujafa hujaumbika. Athumani ulikuwa na nguvu zako leo hii unatembelea bike,.Mwenyezi akupe nguvu na imani uweze shinda mitihan hii ya Ulimwengu.Umati mkubwa umekuja kukupokea, naomba msiishie hapo uwanjani, kwa hali na mali endeleeni kumsaidia Athumani, msije mkachoka, Athumani ana safari ndefu ya kushinda majaribu yaliyomfika.
ReplyDeleteRehema na Amani ziwe juu yako Athumani.
Bro,
ReplyDeleteMwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Yu Pamoja Nawe.
Fidelis M Tungaraza.
Kwanza kabisa napenda kutoa pole kwa familia na Bwana Athumani, Mungu ampe umahiri, ushujaa na uvumulivu juu ya hili.
ReplyDeleteAwe mwenye kujikubadilisha na INEVITABLES. AMEN,
One point i want to suggest to him and his family, he has to take his life on new direction, of being an advocate and champion of ROAD SAFETY AWARENESS, given his high profile, he will be a perfect candidate for that purpose.
Meeting thousands of victims, who have been crippled by road accidents, who have no same profile and backings financially to aleviate the pains, they are suffering.
As Journalist bringing in the stories ya mayatima na broken families as a result of road accidents, I am sure there are lot of stories, on which the general public deserve to know.
and Hopefully setting up a just an organisation, taking on leading role with other victims on FIGHTING THIS JUST CAUSE,(ROAD ACCIDENTS).
Mungu atulinde na MAAJALI YA KILA LEO KWENYE MABARABARA YETU. AMEN.
machozi yamenitoka amenikumbusha baba yangu kipenzi na yy alipooza na kufunga kauli nikiwa darasa la5 na kipindi kile miaka ya 86na 87 huduma zilikuwa hafifu sana akatangulia mbele za haki but kwa sasa huduma zipo namuombea lisilo wezekana kwa binadam kwa muumba linawezekana nampa pole na wauguzi wote.
ReplyDeleteankal bwana yani umeshindwa kutumia camera ya maana ukaona utumie kisim chako hayo mambo ya visim ni yakitoto achana nayo mtu mzima tumia mitambo ya uhakika
ReplyDeletepole sana mpiganaji wa habari mungu yupo nawe
hujafa hujaumbika
god bless u.
Kamichu ulivyoongeza hayo maneno ni vizuri mno, manake pale alipo jamaa ni atachanganyikiwa sana kama hatapata msaada toka kwetu. Binafsi simjui huyu kaka ila nimesikitishwa mno na nilijaribu kutoa maoni yangu kuwa tupromote manesi wetu na kumchangia ila kuna mdau mmoja aliniponda hapo juu.
ReplyDeleteMANENO YAKE:
Kaka Mithupu mpe pole sana huyu jamaa Yetu. Mungu awe naye daima katika kipindi hiki kigumu kwake na familia yake.
Wewe mdau wa Massachassutes unayeandika kwamba tu-train manesi wetu..umenifurahisha na wazo lako lakini vile vile nadhani wewe ni mnafiki.
---------------
inayonyesha ni wazi huyu mdau mwenzangu ni kachanganyikiwa na maisha (nenda shule achana na maboksi ulaya pls) manake badala ya muda kama huu tushirikiane yeye ananiita mie mnafiki.
Kama utatoa anuani au simu itakuwa vizuri. Mi ni nesi najua watu wa hivi huwa wanaumia sana na kuwa na hasira (inaeleweka manake hata ingekuwa ni wewe, leo unaweza kujishugulikia mwenyewe kesho unafanyiwa kila kitu, kwa kweli inauma). Anahitaji si tu nyumba ya milango mipana anahitaji mtu wa kuwa nae masaa yote, wa kumlea kama mtoto. Jamaa tuache dharau tushirikiane kwenye swala hili.
Mungu ibariki africa, Mungu mbariki JK.
Maongezo.....
ReplyDeletena pia anahitaji sana mazoezi kwa huku huwa wanatiwa kwenye maji manake bila ya hivyo huwa wanashikwa na pathological fracture ambayo ni mifupa inavunjika yenyewe, na hupatwa pia na decubitus ulcer ambazo ni vidonda vinavyotoka sababu ya kukaa kwa aina moja. so kuzuia hivi vidonda inabidi mtu amgeuze kila baada ya masaa 2 na mara nyingi huwa vinapona kwa tabu sana. Jamani tuungane kumsaidia kaka yetu. Nimeona huruma sana kuona hata baba yake ni ana nguvu zake ila ndio hivyo tena.
Pole sana kaka yangu usihuzunike sana mungu atakusaidia.
Mdau massachusets.
NB: hiyo stori uliyoongeza ya dada aliyesukumwa?? ni nani hebu tutolee pls michuzi. manake kuna watu ni afadhali waende motoni tu moja kwa moja. Hata huruma hawana.
Franco mtui nae vipi kuna habari zake zozote ?? Najua pascal mayalla anaendelea vizuri na vipi mzee apiyo? nakumbuka walilazwa wote.
ReplyDeletenimebofya hapa mpaka nilijuta manake nilifikiri ni video yake kumbe ni gari walilopatia ajali na pia sijaelewa kaka yangu huyu ni mwandishi wa habari au ni mpiganaji ngumi?
ReplyDeleteKuna mtu katoa wazo la choo maalum ila kwa taarifa watu waliokuwa na spina cord injuries huwa wanapata choo hapo hapo mkojo ni wanawekewa catheters nk sipendi kwenda ndani zaidi ila fanyeni uchunguzi na nyie ndio mtaelewa zaidi.
Pole kama yangu, Hugs and kisses from the netherlands
mnifafanulie wadau pls
ina mana kaka yangu huyu hajaoa? basi huyo mwanamke kama kaishia alikuwa sio mke mtu gani anafanya unyama kama huu?? Lakini sishangai wako watu wa namna hii.
ReplyDeleteThanks kamichu
simjui kabisa uyu kaka ila nilikua nafatilia hizi newz
ReplyDeleteameniuma machozi yamenitoka eeh Mungu umtie nguvu na umpe moyo mkuu na wote wanaompa huduma!
aisee me nilijua amepata japo nafuu baadhi ya viungo vyafanya kazi?
Yaa Uthman, Hakika hujafa hujaumbika,
ReplyDeleteALLAH amepitisha rehema yake, ni jambo la kushukuru kwani lina kheri nyingi ndani yake.
Kikubwa ni lkuwa mtu wa subira...Stainuu biswabr...wa.salaat..japo kwa kuaa waweza kusali pia.
Inshaalah ALLAH akujaalie wepesi.
kuna watu mnaboa mnaleta mada sizo kabisa..kwenye issue kama hizi very sensitive mtu unaleta pumba zako msonyoo! kuweni na adabu basi..
ReplyDeletePole Brother..Usikate tamaa, yote yatapita!
Oh pole sana Kaka. Hujafa hujaumbika! usikate tamaa..Mungu kakujaalia uzima mpaka dakika hii mshukuru sana Mungu..apangalo Mungu halina makosa..kaka jipe moyo utashinda!Napenda kukupa pole sana wewe pamoja na familia ndugu na marafiki kwa wakati huu mgumu, believe me u will be alright. Hang on there..sio mwisho wa maisha kaka yangu. Pole sana!
ReplyDeletemdau flani
Pole sana Athumani jamani ndugu zangu sijui nisemeje, kweli kama hujafa hujaumbika. Kule Moshi niliwahi kuona NGO inaitwa KASI kwa ajili ya watu waliopata matatizo kama haya ya Athumani wapo wengi na wanaumoja mzuri sana. kama dar es salaam hakuna mimi nashauri waende Moshi pale opposite na Stanbic zipo hizo ofisi. Athumani akikutana na watu kama hao wakaulizana matatizo nk. atakuwa na faraja sana.
ReplyDeleteWazo la kujengewa mimi naafiki tena itengwe hata akaunti kwa mdau yoyote atumbukize, hii sio upendeleo ila bahati wazo limeangukia kwa Athumani...
FARAJA PEKEE NDIO ITAMFANYA AWE ANAJIONA BADO YUPO NASI VINGINEVYO ATAKATA TAMAA KABISA...
ULEMAVU WA UKUBWANI NI TATIZO MAUMIVU YASIOISHA
Jamani Pole sana my bro athumani, imeniuma hata mimi nimeshindwa kuyazuia machozi yangu kutoka.Mungu ni mwema -Tunakuombea upone haraka.Ni kweli wadau, athumani anahitaji kuchangiwa kidogo.
ReplyDeleteMama Dastan Msengi.
KAKA MICHUZI
ReplyDeleteNIMEPENDA SANA HUU MOYO AMBAO MWENYEZI MUNGU AMEKUJALIA (UBARIKIWE)
KI UKWELI SISI KAMA NDUGU/JAMAA/WACHA MUNGU / MARAFIKI NA WALE WENYE MAPENZI MEMA KWA NDUGU YETU HAMISI TUNAHITAJI KUFANYA KITU AMBACHO SI TU KWA AJILI YA HAYO YALIYOMPATA BALI NI KWA AJILI YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWA JAMII, PIA MBALI NA HAYO YOTE TUNAYO KILA SABABU YA KUMSAIDI KWA SABABU KI UKWELI YEYE (HAMISI) NI BABA WA FAMILIA SASA HIYO FAMILIA INA MWELEKEO GANI
NINAYO MENGI SANA YA KUSEMA KWA SABABU MOYO WANGU UMEJAWA NA HURUMA NYONGI SANA NA NIMEGUSWA SANA NA HUYU BWANA
MAONI
WADAU TUACHE KUTUKANANA HAPA KWENYE BLOG NI SEHEMU YA KUTOA MAONI YENYE KUJENGA MALIMBANO SIO KWAKE
KAKA HAMISI MUNGU YUKO NA WEWE HAWEZI KUKUCHA
AMEN