TV CHANNEL GANI BORA KWA HABARI?
Brother Michuzi,
Ratiba ya wana-dar es salaam tulio wengi tulioajiriwa ni ngumu sana sasa hivi kutokana na tatizo donda ndugu la foleni za magari barabarani. Taarifa za habari vituo mbalimbali vya TV vilivyozoeleka huanza kati ya saa 1 hadi 2 muda ambao wengine tunakuwa hatujafika majumbani.
Vituo mbalimbali mida hii vinagongana kutangaza taarifa, huwezi ukaangalia channel zaidi ya moja kwa wakati. Matokeo yake unakosa 'balanced reporting', kuna taarifa zingine unazozitarajia hazionyeshwi au kutangazwa na baadhi ya vituo kutokana na maslahi ya mmiliki, kwa mfano nimegundua ITV haitangazi habari mbaya zinazoihusu CCM kutokana labda na itikadi ya mmiliki, taarifa muhimu ya kikao cha jumuia ya umoja wa vijana kinachoendelea Iringa haijawahi kutangazwa kwa sababu ya sakata zilizotokea huko.
TBC nayo kwa sababu inamilikiwa na serikali haitatangaza kwa undani habari negative za serikali na chama tawala, na haitangazi kwa kina kizuri kinachohusu vyama vya upinzani, vitu kama hivyo. Wangekuwa wanapishana mida ya kutangaza, mmoja taarifa saa 1, mwingine saa 2, mwingine saa 3, tungeweza kuangalia kotekote kwa zamu, sasa wote wameng'ang'ania muda niliotaja hapo juu.
Mimi siku zote ni huwa natazama ITV habari saa 2 nikikosa naangalia marudio saa 4:30 jioni au saa 12 na saa 1 asubuhi siku inayofuata. Tatizo la ITV ni kama nilivyosema hapo juu, nafikiri wanamuogopa sana mmiliki. Kitu chochote kinachohusu chama chake, biashara zake, familia yake, yeye binafsi, ni habari kama tu ni nzuri, itatangazwa sana bila kujali ni muhimu au la, ina maslahi kwa taifa au la, lakini kama ni mbaya, hutaiona.
Pia vipaumbele vyao havieleweki, habari nyeti kama za vikao vya UVCCM, mauaji ya kijana pale Victoria yaliyofanywa na polisi, jaribio la mtoto kulipua ubalozi wa Marekani, imagine haziko kwenye taarifa za jana na juzi!
Naomba wadau wanisaidie kujua ni
channel gani ambayo wengi wanaona ina sifa zifuatazo:
- Inasikika vizuri na kupatikana kirahisi maeneo yote ya Dar
- Inazingatia uhuru wa habari- ina-ripoti bila upendeleo wala uoga na haiweki maslahi na itikadi ya mmiliki kama agenda ya kuzingatiwa katika habari.
- Ina wanahabari wanye utambuzi wa habari muhimu kwa maslahi ya taifa na wanaifuatilia kwa undani na kuipa uzito unaostahili na kwa wakati ikiwa motomoto.
·-Inatangaza taarifa zake muda muafaka kwa watu mbalimbali hasa wafanyakazi (saa 2 usiku na kuendelea)
Asanteni.
MDAU CHRISTOPHER M.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    wee mdau, channel iliyo bora kwa habari ni TBC1.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Ni kweli kabisa mdau. Pia utakuta vituo vingine kama ITV wanapokuwa na COMMERCIAL BREAK katikati ya taarifa ya habari, basi wanaweka matangazo mengi hadi mtu unasahau unaangalia taarifa ya habari au matangazo ya biashara. Kwa kukusaidia:
    Channel 10 taarifa ni saa moja, Mlimani TV taarifa saa 1 na nusu, zingine nyingi saa mbili na marudio saa nne usiku. Itabidi tu upange muda vizuri vinginevyo uwe msomaji mzuri wa magazeti...

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Tafuta kazi ya U-House boy! Wakati wenye nyumba wamekwama kwenye foleni, wewe utapata nafasi ya kujinafasi kwenye Bonge la Sofa ukiangalia ukitakacho bila presha ya kufikiria foleni ya kesho!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    Kwa conditions unazotaka, sidhani kama kuna TV channel inayotimiza vigezo kama hivyo. Kwa Ujumla local channel zote za hapa kwetu TZ, zinafuata masharti na mwelekeo wa mwenye hiyo channel. Ilipoanza Mlimani TV nilidhani kuwa itajipambanua na kuwa ya kiana yake, lakini hadi hivi leo sijaweza kuitofautisha na hizo channel nyingine.So angalia hivyo hivyo hizo Channel na ukijaziajazia na habari za magazeti na za vijiweni, huenda ukapata mseto mzuri. Wajua kuna habari nyingine huzipati kwenye TV, au Magazeti, isipokuwa utazipata vijiweni na zikiwa bado hot kabisa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    Anon wa 3 umenivunja mbavu jaribu kujiunga navikundi vya vichekesho may be you go make more money

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2010

    we mdau unaesema atafute kazi ya u h.girl huna akili kabisa,huyo mtu anachoongelea ni kweli lakini wewe unafanya jokes.nikweli kabisa anachozungumza.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2010

    Inakera sana unapoona mtu anajibiwa vibaya katika hoja ya msingi. we Anon na 3 umechafua hari ya hewa katika kujadili jambo la msingi sana.
    Nikweli mdau kuwa kuna mapungufu sana katika taarifa za habari ya baadhi ya mashirika ya habari. wewe umetaja mapungufu machache tu, yapo mengine katika michezo, mfano timu kama ya simba ikicheza ni kazi kubwa kupata habari zake kwenye kituo kama ITV. kwa sasa kwa mtazamo wangu, pamoja na kuwa kinamilikiwa na serikali kituo cha television cha TBC1 walau kuna uhakika wa kupata habari sahihi. Tido mhando anajitaidi kwakweli kukiweka kituo hiki katika hari bora zaidi. kingine ni channel ten. ukikosa habari ya vituo hivi viwili basi kuliko bakia tegemea kupata habari ya upande mmoja zaidi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    Mdau wewe Christopher..kweli umefulia hahahahah...yaani vikao vya UVCCM ni kitu nyeti? Au I am missing something?

    Harafu swala la mda..hilo hata huko ulaya lipo...inamanisha kwamba..hizi media house..zina ushindani..kwa hiyo media inayoweza kuattract watazamaji ndo hiyo iliyobora. Mfano kama unaiamini TBC..ni hakika utaiangalia hata kama ITV itakuwa hewani..na kinyume chake.

    Kwa hiyo mdau..ni wewe kuamua..kwangu mimi naona ndo utaratibu mzuri kushindana. kizuri chajiuza. Kibaya chajitembeza. Kama ITV ni nzuri/inaaminika..watu wataiangalia hiyo..kama ni kinyume..watu wataswichi kwingine...After all wakiweka mda tofauti..watakosa watazamaji..maana wengine watakuwa wameshanaglia habari kwingineko..ndo soko la biashara hilo..

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    Binafsi huwa naangalia TBC1 coverage yao ni nzuri na kila siku huwa wanajaribu kubuni vita vipya..

    ReplyDelete
  10. Labda mi niwaambie tu kuwa mimi binsafsi nilishachoshwa na taarifa za habari za Local TV's, kwani unaweza kusikia habari imetokea asubuhi hii au pengine usiku wa kuamkia siku sawia(kwa mfano saa 10usku hadi saa 1 asubuhi) lakini taarifa hiyo usiipate kwa muda muafaka eti mpaka saa mbili usiku,na mbaya zaidi ni kuwa unaweza kuskia habari imetokea saa kati ya saa kumi na moja jioni na mida ambayo taarifa husika inasomwa lakini utakuta taarifa hiyo haijai include hiyo habari,taarifa zimejaa maigizo tuuuuu,kwa kweli nimeshindwa!Utaambiwa sasa ni muda wa taarifa za habari za kimataifa,unachokikuta huko ni ujinga mtupu,hivi kweli inawezekana kuwa muda wote wa makusanyo ya taarifa za kimataifa ukatuwekea habari moja ya sekunde 60 au dk 2,na huipati habari kwa uzuri uunaotakiwa! Ndo maana nimestack kwa DSTV,kule unaipata habari live toka CNN,BBC,Aljaazira na kadhalika,angalia channel kama KBC,Citizen ni tofauti na hapa!Mi bwana nikiitaka habari ya nyumbani nafungua michuzi blog,japo naye siku hizi amekuwa senior,anapost habari mbili au tatu kwa siku na matangazo kibaoooo,na pia nasikiliza habari ya EA Radio,au kama vipi msikize kibonde jioni katika clouds fm,huwa habakisi habari za siku hiyo!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2010

    Naona angalau Chanel 10

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2010

    Channel Ten tu ndo huwa wanaonesha habari kwa undani zaidi angalia sakata la ndugu zetu kule mara walivoathiriwa na uchafuzi wa mazingira wa migodi ya barrick..ITV ndio walewale kama TBC habari za chama tawala kama harambee kuchangia CCM ishinde zitaoneshwa kwa kina sana...tuache ubaguzi...

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2010

    Usijihangaishe mdau hutapata jibu miongoni vya vituo hivyo vya TV.

    Sisi wenye kiu za habari tunakuja hapa ktk blogu ya jamii au JamiiForums, ambako angalau kuna nafasi ya kupumua kusema jambo au kuchambua jambo.

    Hata Mh. Mstaafu mmoja alisema hakuna 'investigative journalism' na 'serious researched questions' toka kwa waandishi, iwe wa TV, Radio au Magazeti ndani ya Bongo.

    Hivyo sasa habari za uhakika zinapatikana ktk citizens owned blogs na forums. Ukitegemea hivyo vyombo vinavyomilikiwa na wafanyabiashara na serikali hupati kitu.

    Na Hali hiyo siyo kwa Tanzania tu, hata USA, UK, Italy n.k wananchi washastuka na kuelewa kutotegemea 'vyombo rasmi' vya habari vinavyomilikiwa na serikali, wafanyabiashara au 'makundi' yenye agenda 'fulani' kwa mfano 'kushinda uchaguzi kwa mbinde'.


    Ukweli ndio huo.

    Mdau
    Shimoni Kariakoo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2010

    TBC1 ndo naweza kupendekeza sababu mfano ukiangalia habari za michezo ITV utaambulia mechi za mchezo wa bao, kufukuza kuku na mipira ya vijiweni. Labda kwa wakazi wa Dar waliowengi mnakuwa barabarani lakini habari za michezo TBC1 pale sa 12.30 na 1.30 asubuhi ni tamu balaa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2010

    Mchuzi hii usiibanie tafadhali!
    Nawashangaaa hamlijui soko huria ninyiii? ebo mnanishangaza sana wenye tv station walipokuwa wanaanzisha hizo station kama chanzo chao cha mapato nyie mlikuwa wapi? au pengine mngeliingilia kati kuwahoji ili kuweza kuweka hizo interest zenu manzozisema leo, guys, mambo yako hivi, mmiliki wa chombo cha habari chochote lazima ana interest zake, kwanza anaangalia mrengo wa kupata zaidi, kwa sababu hiyo ni biashara, na yamkini pia inawezekana anahofia kuweka habari amabzo ama hana uhakika nazo au zinazoweza kuharibu biashara yake kwa namna moja au nyingine, namaanisha kuwa kwa kawaida mtazamaji wa tv station yeyote, wewe ni kukubaliana na unachokiona kwenye hiyo station tu, kwa sababu huna nafasi ya kushawishi kubadilisha even ratiba ya kipindi hata kimoja, kama unaona haikufai wewe chapa mwendo au usiangalie tv kabisa, eee wewe umenishangaza soko huria limeharibu kila kitu, na kumbuka kuwa si kila unachofikiri kuwa ni muhimu, kinakuwa muhimu kwa kila mtu, ndio maana unaona habari nyingine zinaoneshwa kutokana na jicho la umuhiomu lilivyoona. ukishindwa hamia kule TBC manake walinifurahisha kuonesha malumbano fulani kati ya mbuge na mkuu wa mkoa fulani, hii ilikuwa nyeti na ilirushwa laivu.

    ushauri: usitegeemee kupata habari timilifu kwa kutegemea tv station tu, soma magazeti, tembelea blog, zungumza na watu nk.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2010

    Switch kwenye channel zotezote. Ikifika saa mbili we anza na muhtasari wa ITV, then nenda TBC. Habari za michezo nenda Star TV.

    Mdau... Tengeru

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 20, 2010

    Ukweli TBC wanakuja juu, nionavyo mimi, hata taarifa habari yao ya saa mbili usiku inanivutia sana. sio huko upande wa pili kila siku kipimajoto ksichokuwa na kichwa wala miguu, mara wahojiwe watu wawili mara siku nyingine wahojiwe wanaume tu, where are you guys? na swali la kipimajoto la yes, no, na sijui will not take us far, hiyo ni close ended question, sio explanatory enough to know the reasons for a certain existing problem. manake hata mtu akitaka kufanya intervention kwa kutumia majibu ya yes, no na sijui haitasaidia.

    ReplyDelete
  18. dimba-dimbaMay 20, 2010

    ni sawa kabisa kwa maoni hapo juu yaliyotangulia isipokuwa mmoja alitaka kuleta mambo ya dharau huwa hawakosi mkumbo 2 TBC1 wako juu kwa habari za michezo kuliko channel yeyoye hapa nchini vinginevyo kama una dishi angalia channel za nje hapa kwetu miyeyusho 2

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 20, 2010

    gazeti la mwananchi ndio suluhisho lkn hawa wengine IPP media, michuzi blogi,tbc1 wote ni ccm maslahi yao mbele kwa mjengwa pia hakuna matatizo
    niliacha star tv habari ilukuwa inaanza saa 2:15 usiku na ndio ilkuwa chaguo langu la kwanza

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 20, 2010

    Taarifa za kina hutazipata kwa kutegemea 'sound bites'. Ikija kwenye luninga hata iweje tayari imewekwa 'hisia' za mhariri husika. Ili kukidhi kiu yako soma magazeti, mtandao, sikiza redio, SOMA vitabu n.k. Usikubali kubweteka na vitu ambavyo tayari umetafuniwa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 20, 2010

    kwa redio nakushauri sikiliza MICHUZI FM, ama runinga wewe ng'amua MICHUZI TV. matangazo yake ni moja kwa moja na yanakuwa updated kila baada ya dakika 30 .

    vyote hivyo utavipata .michuzi dot com

    hi hi hi hi hi hi hi
    mdau no 5 .

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 20, 2010

    TBC1 oyeeee kwa kila kitu ITV muozo haswaa kipindi cha michezo ndo zero kabisa kweli ni habari za bao tu !

    ReplyDelete
  23. PETER NALITOLELAMay 20, 2010

    I THINK ARE HASHEEM THABIT WHILE IS ON DAR TOUR AND ARE LEAVING EUROPE OF USA THEREFORE HE CAN OPENED THE STATION OF TV LIKE CNN HERE IN HER HOME GROUND OF TZ DAR FIRST BECAUSE ARE THE SON OF AFRICA AND LATER IS THE YOUNGEST EVER BILLIONAIRE TO BE KNOWN IN AFRICA CENTRAL AND EAST UNDER 24 YEARS HE WAS TO SHARE NEWS LIKE CNN WITHOUTING HELPING OTHER SIDE SO PRAY THAT ARE MISSION IS GONNA WORK FRESH HASHEEM IS THE ONLY ANSWERED MAN IN THAT CASE OF NEWS AND ALSO ARE YOU READING MICHUZI BLOGS? THERE IS ALL NEWS YOU NEEDN`T ACTUALLY TV HE DOES NOT BIAS ANY BODY EVEN HER OWN T SHIRT THE FULANAZI SO GO TRY TO READ MICHUZI ALL THE STAFF YOU SAY DIDN`T SHOWED IN TV WERE ON MICHUZI WORLD NUMBER ONE BLOGS OF AFRICANS THANKS NO THANK YOU FOR MY COMMENTS OF WISE AND BRAVES,

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 20, 2010

    Wewe sio mtafiti makini. Halafu mwisho wa siku unatoa matokeo kuwa "kwa mujibu wa utafiti, channel xxx inaongoza kwa ubora katika vigezo vifuatavyo....". Kuna cons nyingi kuliko prons katika kufanya utafiti kupitia internet (emails and blogs), bado ufumbuzi wa matatizo yake haujapatikana kisawasawa. Sasa unaona watu wanajibu kwa kusema wao ni "Anons", then utajuaje kama hawajarudia kujibu mara mbili au zaidi? Hata wangetaja majina inawezekana yasiwe ya kweli. Na kama majibu yanatolewa na watendaji wa chombo cha habari husika? Unatumia haphazard sample? etc. etc. STOP THIS EXERCISE IMMEDIATELY, YOU ARE FOOLING NOT ONLY YOUSELF BUT THE ENTIRE COMMUNITY INVOLVED!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 20, 2010

    Nampongeza Christopher ambaye ni mtoa Mada kwa observation makini.

    ITV imeshakuwa ni kama TV ya Chama Cha Mapinduzi. Utashangaa kuona hata TBC1 ambayo ni ya serikali inakuwa "bold" kutangaza mambo ambayo ITV inayakimbia kabisaaa. Inaonekana vile vitisho alivyopewa bwana Mengi wakati wa sakata la mafisadi papa ilifanikiwa.

    Nakumbuka Nyerere alisema CCM siyo mama yake. Akimaanisha kuwa alikuwa akiongozwa na "values" fulani siyo ufuasi kipofu.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 20, 2010

    Hakuna chombo cha habari bora Tanzania wala duniani zaidi ya globu binafsi hivi sasa. Kila chombo cha habari kinawakilisha maslahi na utashi wa mmiliki, ikiwemo blogu. Uzuri wa blogu hazifichi maslahi na utashi wake, wakati vyombo vingine vinajifanya viko 'fair', 'objective', 'balanced' wakati ni wizi mtupu.
    Siku hizi hata habari zilizokuwa zinaripotiwa kwa usahihi za michezo nazo zinaripotiwa kwa ushabiki.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 20, 2010

    Mwananchi Communication Limited, Wanajiandaa kuoanzisha TV tusubiri tuone.

    Kwa sasa the only proffesional and fair balance TV station is National TV... i.e. TBC through Channnel TBC1... and soon they are launching second channel TBC2

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 21, 2010

    Duniani kote hakuna chombo cha habari kisicho na malengo wala mwelekeo hakuna hata CNN,BBC,ALJAZEERA na wengine kikubwa ni maslahi ya mmiliki na nchi zao kwanza ndiyo maana wanalipaka matope bara letu Afrika,Iran na nchi zinazopingana na nchi yao kimaslahi chumvi zaidi kuliko ukweli halisi,cha muhimu usizubae kwenye channel moja jijuze kutoka vyanzo mbali mbali vya habari magazeti,blogs,radio na TV ndiyo utaipata habari kwa kina.Mtafute Jenerali Ulimwengu atakupa kilichompata kwa magazeti yake kuwa fair wakati wa awamu ya tatu ndiyo uje ulaume mmiliki ama SIRIkali ukizingatia wengi wanadaiwa KODI kibao

    ReplyDelete
  29. Mimi naona ni bora kuangalia Channel 10 na TBC1 halafu uwe unasoma magazeti na kutembelea tovuti mablimbali zikiwemo blogu.

    Halafu wewe PETER NALITOLELA kama hujui KINGEREZA naomba utumie lugha unayoifahamu ni aibu sana kuandika KINGEREZA KIBOVU unapotoa maoni.

    Ni bora wewe PETER NALITOLELA uandike kwa KUTUMIA KISWAHILI AU KIFARANSA FASAHA kuliko KINGEREZA CHAKO CHA KUUNGANISHA MANENO YASIYO LETA MAANA HALISI AU UMETUMIA GOOGLE TRANSLATE????

    OK ,wadau wote muangalie TBC1 na CHANNEL 10. Daniel

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 21, 2010

    Chris, kama ung'enge unapanda jaribu BBC utaniambia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...