Ankal Asalaam Aleikhum, Mie langu ni hii iPhone yangu ya 16GB yenye kava nyeupe ambayo kuna msamaria mwema aliniletea kama zawadi toka Marekani. Huwa ina kwikwi ya kukata mawasiliano na haiwaki kabisa endapo chaji inakuwa imekwisha. Software ya BlackraIn ninayo na huwa naizibuaga ikikata. Sasa cha ajabu leo baada ya kwikwi nilipojaribu kuibinjua nakuta hayo maandishi kama mnavyoiona.
Naomba wadau wa Globu ya Jamii walio wataalamu msaada tutani wa kunisidia nijue tatizo nini na nifanyeje izibuke tena. Ina namba kibao za maana nami hadi nimechanganyikiwa wallahi. Msaada tutani wadau wataalam ambao najua mpo kibao kila pembe ya dunia.
Mdau wa Chang'ombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2010

    iweke jalalani

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    ukweli ni kwamba iphone ukiwa nayo africa hutaifaidi kabisa,kama mtu ankuja nimshauri simu gani ya kununua nitamshauri anunue simu nyingine kwa africa kuliko iphone, technology africa bado sana,hasa ya internet ambayo inahitaji update kila mara.wa tz kuna simu kali sana, kuwa na simu kali sio lazima iphone kuna simu nyingine iphone mavi tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2010

    KILICHOFANYIKA HAPO NDUGU YANGU HUYO JAMAA ALIYEKULETEA HAKUKUAMBIA UKWELI WA UPATIKANAJI WA SIMU HIYO: NI HIVI JAMAA WA MAJUU HUO WANAPATA HIZO SIMU KWA CONTRACT HUWA HAWALIPI HATA SENTI TANO NI BURE KABISA PROVIDED UTAKUWA KWENYE CONTRACT NA HUYO SERVICE PROVIDER WA NETWORK NA CONTRACT ZINATOFAUTIANA KUANZIA MWAKA MMOJA HADI MITATU: NA PAMOJA NA KULIPIA BILL ZAKE KILA MWEZI PIA KUNA INSURANCE UNALIPA KWA AJILI YA SIMU AMA IKI-IBIWA AU KUPOTEA UNAPEWA MPYA BUREEEEE, SASA JAMAA WANACHOFANYA NI KUZUSHA KUWA SIMU YANGU AMA IMEPOTEA AU KUIBIWA NA WANAPEWA MPYA NA HIYO YA ZAMANI NDO HIZO WANALETA HUKO KAMA ZAWADI KWA JAMAA ZAO KWANI HUWEZI KUTUMIA TENA KATIKA NCHI HUSIKA WATAKUSHIKA NA HATA HIVYO UKISHAPELEKA HABARI YA KUPOTEA AU KUIBIWA WANA-DISABLE MTU YOYOTE AKIWA NAYO HAIFANYI KAZI TENA: NA SASA WAMEGUNDUWA KUWA WATU WAKIRIPOTI IMEPOTEA HUZISAFIRISHA NJE YA NJE, KWA HIVYO BASI WAMEGUNDUWA JINSI YA KUZI-DIABLE GLOBALLY, KWA MANTIKI HIYO BASI HIYO YA KWAKO KAMA ILIPATIKANA KWA MTINDO HUO IMESHAKUWA PERMANENTLY DISABLED HAIWEZI KUFANYA KAZI TENA HATA KAMA MTU ATAIFUFUA KULE ITAWA-ALERT NA WATAIUA TENA KWA VILE WANA SERIAL NUMBER YAKE KWENYE MTANDAO WAO. HIYO NI TECHNICAL KUIELEZEA HAPA KI-UTAALAMU NI NDEFU MNO.

    ReplyDelete
  4. Mume Wangu, Mikanjuni TangaMay 23, 2010

    Hizo minutes ulizoambiwa siyo nyingi, kuwa mpole na usubiri zimalizike na u-try again.
    Zawadi nyingine zina gharama vilevile, tujifunze kununua kwa jasho letu badala ya kuomba omba zawadi kila kukicha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2010

    YA KICHINA HIYO!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2010

    kaka nenda kwa fundi koroboi akubadilie serial number.kama yeye alivokufungia. mafundi modification wengi wapo ikishindikana . basi waone wachina watakusaidia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2010

    Iphone Tanzania ni kama mapambo tu. Too much money for nothing. Huwezi kuinenjoy simu yako bongo kabisa. Utamu wa iphone ni hizo apps...You want to sleep, there is an app for that" Love it...

    Kwanini hukuwa una sync hiyo simu before?

    Jailbroken and openssh Iphones unaweza kuaccess data kutoka user/library folder. Try to do that and then restore back the phone. Sidhani kuwa wameshaweza kudisable phone nje ya nchi.

    Kama hujui kurestore iphone google online utaona na kama ukirestore bado inaafanya hivyo basi motherboard imeharibika beyond the repair.

    Pia kuna software inaitwa phoneview. Unaweza kuitafuta online hiyo unaweza kuitumia kuaccess your data.

    Goodluck lakini kumbuka vitu vya bure always cost more.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2010

    1. Ipeleke kwa mafundi wa simu ambao hutumia njia za kisasa kutengeneza simu, wao wataicheck hiyo simu serial number yake kutoka kwa watengenezaji wa hiyo simu,na kuweza kuitengeneza. Hii itawezekana kama simu yako sio conterfeit product, yaani ni geneuine product ya manufacturers wa iphones na siyo imitation.

    2. Kama imeshindikana kuitengeneza na shida yako ni hizo number za simu ama contacts, nadhani unaweza kwenda kwa service provider wako yaani Zain, ambao nauhakika wataweza kukupatia tena contacts zako zote kutoka kwenye hiyo sim card yako, wape tu namba yako ya simu na uwaelezee tatizo lako. Kuna service providers wana uwezo wa kufanya hivyo pale ambapo sim cards zinablock au mtu akiibiwa simu. Wanakupa sim card nyingine ya namba ile ile ya zamani yenye contacts zako zote.

    3.Kama na hilo limeshindikana, pole sana. Kaikomboe number yako toka zain, na uanze zoezi la ku-save number moja moja pale utapokuwa ukipigiwa simu, ama unaweza kupata contacts baadhi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kuwaomba tena namba zao, waelezee tu simu imepata dhoruba.

    4. Mwambie huyo aliyekuletea hiyo zawadi toka huko marekani, aache kukuletea zawadi mara moja! Vijizawadi gani hivyo feki? Mmzzzz!

    ReplyDelete
  9. wewe anoyi uliyeandika maandishi mengi acha kumdanganya mwenzio nimekuwa na ipod 32gb for 3 years na sasa hivi nipo na iphone niko na uzoefu mkubwa sana ni hilo problem kilicho tokea ni kwamba jamaa amekosea password mara kumi,ndo maana imekuwa hivo sasa wewe subiri hizo dakika simu yako itakuwa fresh kabisa,ila nenda kwenywe setting na ubadilishe setting yako,yaani kama ukikosea pass word isifute data. ni hayo tu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2010

    ulikosea pin mara kadhaa sasa imejifunga. Na kila utakapojaribu kfungua minutes zitaongezeka. Muulize jamaa aliyekuletea

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2010

    Ndugu yangu Kama una laptop au computer nyumbani na Internet download program inayoitwa Itune halafu connect simu yako na laptop au computer yako moja kwa moja simu yako utakuwa lazma huyo jamaa yako kashairegister na hiyo program ya Itune sasa hiyo program inakuambia Kama simu yako inataka kuupdate software yake la Kama itakwambia haihitaji kuupdate basi kuna option pia ya kuirudisha simu kwenye orginal setting yake lakini yote hayo ninafikiri pia itakubidi uwasiliane na huyo jamaa yako akupatie login details zake za hiyo itune . All the best

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2010

    aliyekuletea hakukuambia ukweli kwamba hiyo simu ni fake version ya i phone,najua sababu ninayo

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2010

    JAMANI ULIMWENGU UMEKUA MDOGO. NILIWAHI KUMSIKIA RAISI WA MAREKANI WAKATI ULE REAGAN AKIWAAMBIA terrorist "You can run, but you can't hide." sasa msemo huo unaonesha wako mbali na wamefika mbali.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 23, 2010

    Hey isskuumize kichwa ni tatizo dogo sana inaonekana kua kama hunguingiza wrong password basi iphone imecrash kwa sababu ya jailbrake.kwa sababu hilo tatizo linatokea kam umeingiza wrong password.lakini inaonekana kua iphone yako ni jailbroken kutumia blackrain(inamanisha unaweza kuinstal downloaded games from internet bila kununua kupitia itunes,na pia labda hio iphone ilikua ni ya contract kwa hio inaweza kua imezuiliwa kutumika kwa line moja tu ya subscriber aliye iuza hio iphone sasa ikiwa jailbroken na black rain unaweza kutumia kadinyingine pia) actually kwa hizo minutes zote ni kama masaa 353773.6,

    solution inabiidi uamue kujaribu kui restore kwenda original firmware lakini caution inawezekana baada ya hapo ukashindwa kuitumia endapo kama hio simu ni ya contract to certain subscriber,kama sio hivyo you can be lucky to use it again.
    how to do it
    lazima uwe na computer with internet
    USB cable (charging cable)
    Itunes software installed.
    you have to know which version is your iphone.2g,2g,3gs,etc
    THEN
    open itunes
    plug the cable from iphone to computer USBport
    START DFU MODE and for that fallow this link

    Sijawaza jua which iphone model unatumia lakini kama unajua a litle basics of computer go to internet and seach in yu tube videos how to restore ya iphone firmware but u have to know ya iphone version..
    hope i have answered ya qn.
    but please wasiliana na aliye kupa kujua kama ni contract phone na ina specelia subscriber because hata kama utarestore u cant use it after that because jailbrake(blackrain) will be lost so choose ya options wisely.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2010

    sikia kaka..iphone inahitaji updates kila mara kwani hiyo kampuni kila kukicha kuna technolojia wanaziongeza katika products zao..sasa kutokana na uhaba wa internet nchini kwetu ndo inapelekea matatizo kama hayo..pia hizo simu huko ulaya zinauzwa kwa mikataba maalum so mkataba ukiisha na kama kuna deni halijalipwa basi wataalam wanaidisable simu yako..cha kufanya jaribu kuiflash ambayo hiyo nayo ni hatari coz ndo unaiua kabisa..iphone kwa bongo sio conducive kaka...tutumie hizi hizi nokia zetu tu..

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2010

    Restaore the firm ware but you will loose your jailbrake(blackrain)na kama ni contract phone u can still not use it because even after restoring the software it will be locked to special subscriber. so contact jamam aliyekupa then know those details.
    after that u can choose to restore.
    u need internet computer and itunes installed use ya charging usb to connect to iphone and computer using usb port.set ya iphone to DFU mode her is the link
    but before u do this know the version of your iphone.http://limitededitioniphone.com/how-to-put-the-iphone-into-dfu-mode/
    hope it will help ya.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2010

    Ni kweli kama walivyosema hapo wadau!! sasa cha kufanya kwa sasa download software moja hivi inaitwa (rebt) katika www.iphone.com au nenda moja kwa moja google andika driverrebt kisha tumia cable kupitia katika hicho kimeo chako then run itazibuka tu!!! ila sio solution ya moja kwa moja inaweza kujirudia na ikijirudia na we rudia tena itazibuka tu. Pia jaribu kuunga net mara kwa mara kwani huwa inajiaptdat yenyewe direct & automatic

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 23, 2010

    Call Muna 0754233355 ataimaliza ila uwe na 40,000/

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 23, 2010

    Kuna maneno hapo juu kwenye simu yameandikwa: "Solo emergenze" = Emergency only. Hayo yaliyoelezwa hapo juu yasipokusaidia, basi itunze iphone kwa kupiga simu za dharura tu (SOS).

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 23, 2010

    Njoo uchukue ya kwangu Nokia 3310, sina kazi nayo

    ReplyDelete
  21. Kama utarestore hiyo simu (bila shaka ni 3gs) itaupdate filmware kuwa 3.1.3 na baseband kuwa 5.12.01 .mpaka sasa hakuna unlock solution ya baseband 5.12.01. So utaweza kuitumia hiyo iphone kama ipod. Blackra1n ni kwa baseband chini ya 5.12.01. Sasa kuna Spirit but ni kwa kujailbreak tu na si Unlock. Wataalam wa kuhack iphone wanasubiri Apple watoe iphone 4G hapo june ila waweze release unlock ya 4G,3GS etc. So lets wait. Nakushauri kwa sasa jaribu tu kuizindua kwa blackra1n wala usirestore ampapo utaupdate baseband na kutoitumia unless new unlock imekuwa released.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 23, 2010

    ina tochi?
    kwanza: kama inatochi; zima.
    halafu update. no itajiapdate automatically. then... no no noo.
    sorry zima tochi.. halafu washa mara mbili kwa haraka haraka. halafu chukua simu nyingine lakini iwe ya nokia yenye tochi, then iunganishe kwa USB halafu iboost kama unavyoboost betri ya gari.
    IPELEKE DT DOBIE.
    mkome na ubishoo...

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 23, 2010

    mimi nilishawahi kuja nayo iphone kutoka USA, kwanza unatakiwa kutoa lock simu yako ili ifanye kazi popote pale inapotumika simcard,ikiwa haitaki kufanya kazi hapo kuna mambo mawili,inawezekana simu yako ipo lock unatakiwa kuifungua au inawezekana simu hiyo ni feki kutoka china haiwezi kuji-update maana wenyewe kampuni ya apple wameishtukia kuwa ni feki,mimi nimetumia huko bongo iphone 3gs na imefanya kazi na tigo huko bongo.kwahiyo ndugu yangu jaribu kuitoa loki au itakuwa simu yako feki siyo iphone.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 23, 2010

    Kuna mshikaji software ya iphone yake ildata, akaipeleka kwa mafundi wakaiweka sawa. Kama una namba ya simu anaweza kukuelekeza kwa huyo fundi fanya iweke hapa ili akusaidie. Au tumwambie michuzi?

    Pole

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 23, 2010

    ATI MMOJA ANASEMA SUBIRI HAYO MA-DAKIKA ITAKUWA FRESH, HIVI UNAJUWA DAKIKA HIZO NI SAWA NA MIAKA MINGAPI KAMA SIKOSEI NI ZAIDI YA MIAKA 15000 SASA NANI ATAKUWEPO HAPA DUNIANI? NO ONE AMONG US WILL BE ALIVE AND EVEN THOUSANDS OF GENERATION TO COME THEY WILL NOT BE HERE. IKISHINDIKANA KABISA WEKA UKUTANI KAMA PAMBO.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 23, 2010

    Subiri kwa siku 14740.56667 itakua poa. Ni hayo tu

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 23, 2010

    Nunue nyingine.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 23, 2010

    wewe anon unayeema simu zinatolewa buire huko majuu ni nani? Unfaikir monthly bills unazolipa katika kipindi cha miaka miwili unapokuwa na kontact na hao jamaa ni pesa kidogo?

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 24, 2010

    Hamna Iphone inatolewa bure

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 24, 2010

    Downgrade au upgrade kwenda higher version kwa kutumia firmware za 3g version 3.0 ndio lock inatoka kiurahisi hata bila ya kuwa na wireless internet

    Then Jailbreak kabla huja unlock

    Then tumia kwa Raha zako

    Ikikuzingua nitafute kwenye
    mwenze@hotmail.com
    0786-070762

    Dont worry that is a silly problem linatatulika kiurahisi

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 24, 2010

    hivi wewe unaundugu na yule kaka wa kanyingo nini???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...