Ankal, pole na kazi.
Shida yangu ni kwamba nna ndugu yangu anatumia madawa ya kulevya, nataka kumsaidia aache. Tatizo sijui pa kuanzia. Huyu mgonjwa yuko Dar. Ningependa kupata ushauri kwa wadau kama kuna kituo chochote (rehab) kinachoshughulika na kutibu watumiaji wa madawa ya kulevya. Nashukuru kwa maoni in advance maana hii imekuwa shida kwa familia.
Wako,
Mdau mtiifu.


hata kama wewe ni teja anza kwa kumuona dr kwa ushauri
ReplyDeleteHujui pa kuanzia??
ReplyDeleteWell mwambie, kaka acha kubwia unga unadhurika kiafya na kifikra.
Kwa uzoefu wangu kwa 'mateja' hata umpeleke 'rehab centre' ya Amerika kama mwenyewe hajasema na nafsi yake kuamua kuacha unga basi kamwe hawezi kuacha kwa kupelekwa huko, nina ushahidi wa hilo wengi wamerudia uteja. Cha kwanza mpe counseling asipoacha kuwa mkatili tengeneza mchongo mpeleke Segerea akikaa kama miezi miwili mi3 bila kuvuta atakuwa amepona kiasi fulani lakini hakikisha mnampelekea msosi daily manake sembe maharage ya segerea kama mtoto wa mama atapata kipindupindu na utapiamlo. Then akitoka Segerea ongeeni nae vizuri kwa kumuelimisha na kumpa counseling ya nguvu huku mkim-monitor nyendo zake na kuhakikisha hapati nafasi ya kukaa karibu na marafiki zake mateja. Kama akiwasikiliza na uhakika ataacha mi nina kaka yangu tulimfanyia hivyo kaacha na ukimuona ukiambia alikuwa teja lazima ukatae!!
ReplyDeletehili ni tatizo kweli pole sana, ebwana ushauri wangu mimi ni kwamba kama uezo upo mpeleke nje ya nchi atatibiwa na ataacha lkn si bongo.
ReplyDeletenakwambia hivi kwasababu tatizo hili lishatukumba sana ktk familia yetu, tulikuwa na ndugu watumiaji na kituo pekee kikubwa cha uhakika ni milembe dodoma, hapo gharama ni kubwa sana kwa watu hawa na pia rushwa kwa sana. yule ndugu alilazwa pale alikuwa anachukua vitu hapo yaani mahitaji ya kibinadamu hlf familia inalipa gharama. tukienda kuulizia mgonjwa tunaambiwa anaendelea vizuri kbs na atapona mda si mrefu.
bwana weee hizo bill za mahitaji zikawa juu kidogo kuja kugundua kumbe wale manesi wa hospitalini hapo hapo walikuwa wanauza unga kwa wagonjwa na kwa ndugu yetu pia, tukaona ni bora arudi tu nyumbani kwani mtu mwenyewe hajihurumii na hana nia.na hapo alishakaa miezi zaidi ya mitatu mamilioni yalipotea bureeee... yaani alikuwa anakula raha, unga tunamlipia sisi
Kuna kituo kipo Korogwe kinaitwa Lutindi. Kinasaidia si unga tu hata wenye ulevi wa kupindukia.
ReplyDeleteNi rehab centre nzuri sana na miezi mitatu tu utaona mabadiliko makubwa ila cha muhimu zaidi ni mhusika mwenyewe kuwa na nia na kuepuka makundi yanayomsukuma kufanya hivyo mara anapomaliza tiba.
Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na madaktari wa huko, namba zao ninazo maana wako milimani Korogwe lakini wana kituo chao Korogwe mjini wanafika mara moja kwa wiki, kuchukua na kupeleka wenye matatizo waliopewa ruhusa.
Kama utahitaji maelezo zaidi unaweza kwenda korogwe au post contacts email au simu yako nitakupigia.
Kuna gharama kidogo unalipia kumweka mgonjwa kwa siku zote na pia pamoja na matibabu wanafundihwa ujuzi wa kazi mbalimbali za mikono.
Pole sana, naelewa ukubwa wa tatizo lako kwa kuwa na mimi nilikuwa na ndugu kama huyo lakini nilimpeleka Korogwe na walimsaidia.
Mpelekeni RUTINDI - kituo kilichopo milimani Korongwe, huduma nzuri, makini na gharama nafuu. Kama huwezi kumpeleka Rutindi, mhamisheni hapo anapokaa sasa hivi, mpelekeni mahali tofauti ikiwezekana iwe nje ya mji ambapo atapata mahitaji ya msingi kama chakula na maji lakini tengenezeni mazingira asionane na watu wengi hasa marafiki zake wa karibu, kwa miezi kadhaa kama mitatu hivi. Iwe ni operesheni maalumu inayoongozwa na watu/ndugu wenye moyo na mapenzi na huyo ndugu yenu, maana ni zoezi gumu na linalotaka dhamira ya kweli, kwani ni rahisi sana kukata tamaa.
ReplyDeleteYes, Kituo cha Lutindi kimewasaidia ma-addicts wengi sana. Ukimwona Psychiatrist au psychologist yeyote anaweza kukupa contacts za Lutindi. Pole sana.
ReplyDeletemtowa maoni wa Mon May 03, 10:34:00 PM wacha utoto, watu wako serious hapa, kama huna la kufanya kwa nini huendi nje ukacheze foliti na wadogo zako?
ReplyDeletemtu alokwisha fika kutaka kutafuta reharb ya mdogo wake unadhani hakuwahi kumuweka chini? na unadhani mbwia unga atasikiliza haya maneno uliyosema? GROW UP
naungana na mdau hapo juu jaribu kumpeka segerea miezi mitatu atasahau hayo maunga akitoka hapo ndio mumpeleke huko rutindi ili akapate ushauri na hakika ataacha kabisa pole sana ndugu kweli huu unga umeua wengi
ReplyDelete