Ankal,
Naomba wajuzi wa sheria wanijuze juu sheria ya kazi ya Tanzania inavyosema juu ya mfanyakazi anaeumia kazini au kuugua muda mrefe pasi kufanya kazi! Compensation zake zikoje na ni wajibu wa nani mifuko ya hifadhi like NSSF au muajiri? Nataka kusaini mkataba wa kazi lakini swala hili silielewi kidogo.
Many thanks

Mdau Edwin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2010

    bongo sheria zipo ila zipo kwenye vitabu tu , we ingia huo mkataba ufie kazini....

    unacheza na bongo

    uliza kwanini inaitwa bongo ?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Nakushauri umuulize muajiri wako mtarajiwa, kwani naamini sera zinatofautiana kutoka kampuni moja hadi nyingine. Wengine ukiugua unafutwa kazi (na bosi wala haji kukujulia hali) na wengine (kama kampuni ya Athumani mpiga picha) ukiugua wanathamini jinsi unavyohitaji msaada na hivyo hawakutupi. Ongea na wafanyakazi wa hiyo kampuni kama ni ngumu kumuuliza muajiri. Usiangalie sana sheria ya nchi, watekelezaji wananunulika na mabosi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Wewe umepata kazi tena Bongo halafu unaanza kuulizia masuala ya kuumwa au kuumia kazini.

    Mtu wangu wewe ingia kazini na sign mkataba. Kwa vyoyote vile kama alivyosema jamaa hapo juu kwamba likitokea tatizo kama hilo basi tena inabidi tu ushukuru Mungu kwani watekelezaji wa sheria wanakula sahani moja na boss wako.

    Piga mzigo jibaba, kazi njema.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    Kuna ofisi za serikali pale UWT na Morogoro Road, Junction. Nilipofunga biashara yangu miaka ya nyuma niliwachukua wafanyakazi na kwenda nao huko ili wajue haki zao. Ni ofisi zinazohusika na haki za wafanyakazi. Niliambiwa kama sikosei kama mgonjwa basi alipwe kama kawaida (mmoja wa wafanyakazi alikuwa mgonjwa muda mrefu). Ni mshahara wa mwezi mmoja kwa kila mwaka aliyofanya kazi. Pili, alipwe nauli ya kwenda nyumbani. Ni hayo tu. Nikamlipia gharama za hospitali ingawa sihitajiki kulipa. Muhimu ni kwa mfanyakazi kulipiwa pensheni (NPF) kila mwezi ili aweze kupata pesa akimaliza kazi. Bado serikali haina program yoyote ya kumsaidia mfanyakazi ambae anaumwa ghafla na kupoteza mshahara. (unemployment benefits).

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    watakiwa kutumia akili yako na kama ulivyo andikishiana mkataba na mwajiri wako. alafu Shshshshwaaaaaaaa kama mbayuwayu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...