Mtanzania wa kabila la kisukuma mwenye umri wa miaka 36 ambaye tarehe 26 Oktober 2009 aliua mkewe Bi Anne Holmstrom umri wa miaka 27 wa Denmark ambaye walikutana Tanzania na kuoana mwaka 2003.
Katika mauaji hayo yasemekana alitumia njia ya kumnyonga mke wake kwa waya za umeme na baadaye kutumia "machate/mapanga" kwa kuukata kata mwili wake vipande vipande, amepata hukumu ya miaka 14 kuwepo jela na atakapomaliza kifungo chake atarudishwa Tanzania moja kwa moja kutokea jela.
Hii ni kufuatana na habari zilizotolewa kwamba mtanzania huyo alihamaki baada ya mke kuomba waachane kufuatana na kitendo cha mume kujihusisha na mwanamke mwingine akiwa likizo Tanzania, kitu ambacho Scandinavien ni makosa makubwa hata kusababishwa watu kupeana taraka za kuachana.
Huku wanakuwa na mtazamo wa ndoa ni za milele kifo ndiyo huwatenganisha na kama mtu hajapata makaratasi ya kudumu ya kuishi nchini kufuatana na sheria huwepo katika mipangilio ya kurudishwa nchini kwake huyu mtanzania ilikuwa arudishwe siku ya pili yake mara tuu baada ya kuachana na mkewe.
haya yalimchanganya kichwani na kufanya uamuzi wa mauaji kwa mkewe watoto zake wakiwa wapo shule ya vidigi-digi
Habari zimetafasiriwa kwa kifupi kwa jamii ya watanzania
na Mdau Mickey Jones
Global Advance Tanzanian Network

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2010

    aibu kweli!! yaani acha tu na atakuwa kichaa maaana tunaamini kuuwa kwa kisukuma unageuka kuwa kichaa. na atarudi kuchota maji ktk kisima cha kisesa kinaitwa kwa nyalali atafanya kazi na nani muuwaji???? kajihalibia maisha mwenyewe

    ReplyDelete
  2. Baba UbayaMay 05, 2010

    well,kabila wala haikuwa muhimu kutaja.pia suala la ngono nje ya ndoa ni kosa hata bongo si huko Ulaya tu.raia wengi tu wameshapoteza maisha au kujeruhiwa vibaya hapa bongo sababu ya fumanizi.
    next time just write in short na sio blah blah za kumwaga.

    lakini tunashukuru kwa habari.kama kweli katenda kosa hilo basi anastahiri adhabu. matter of fact,14 yrs wasn't enough kwa ukatiri alioufanya.

    ReplyDelete
  3. Mtoa maoni wa Wed May 05, 06:41:00 PM umenikumbusha mbali sana...(kwa nyalali)...ila nasikia kisima kimekauka, kwa hiyo atakuja kuchota maji kanyama au nyamuhongoro...damn, nina miss sana kisesa

    ReplyDelete
  4. bhoke serengetiMay 05, 2010

    Hivi wale si wakrito safi sasa talaka zitoka wapi kwa wazungu si haramu ila mswahili ni haramu watch out ni haki ya mwanamke kudai talaka panapo kuwa na sababu za msingi wanawake wa africa sio mtu mapaka akuue kama ndugu zangu wakurya kule ukonga mombasa ee mungu tunusuru.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2010

    Kanda ya ziwaaaaa!
    Anyway ukabila siyo fresh ila ndugu zangu tupunguze nje plus wake wenza even if dini hairuhusu(kama si mwislam).
    Mdau The Dreamer

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2010

    Kama ni msukuma basi itakuwa alimfananisha mkewe na albino,kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2010

    Kapone akweli huko hawana kitanzi. Na sisi wabongo tujifanye kama nchi za uarabuni, Hazipokei wahalifu...Wakirudi nyumbani tunanyinga...Mtu kama huyo abaki huko huko...Kama aliweza kuua akirudi si ataua tena huku kwetu...Abaki huko huko


    JK tunakuomba ufuatilie hili...Hatutaki wahalifu nchini...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2010

    yaani you had to add kabila eti msukuma. yaani lazima wewe utakuwa una agenda na wasukuma....au kuna msukuma alikupiga kibuti....wasukuma scarce commonidity wewe ohoo!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2010

    (1) Watanzania wenzangu; tukubali kuwa sisi ni Watanzania na kwa kuwa tuna rangi, dini na makabila mengi huo ni utajiri wetu HATA HIVYO: TUWACHE KUSEMA "ooh...huyu kabila hili au lile au dini hii au ile..." Katika kila rangi, dini, nchi na kabila duniani kuna watu wema na watu waovu.(2) Tukubali kuwa kwa wanaume wengi hapa TZ na Afrika kwa jumla, ukatili (violence) dhidi ya wanawake ni kitu cha kawaida. Kila mwaka TZ kuna wanawake wengi wanauliwa au kuumizwa na waume au mabwana zao; na majority ya kesi hizo hazifiki mahakamani. Wanaume wengine wakienda nchi za nje wanaendeleza unyama wao and they pay for it. Tujirekebishe: wanawake ni mama, mabibi (nyanya), shangazi, dada na mabinti wetu. (Uungwana sio kuvaa tai na jeans tu: ni mtazamo wako wa maisha na watu na viumbe wenzako). Siku njema yo'll!!!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2010

    Watanzania mnapenda kukuza mambo, huyo bwana akukosea kutoa habari hiyo na wala hana kosa kabisa kutaja kabila! kwani hapa bongo uwa wakati mwingine muhalifu anapojulikana kabila lake atajwi?
    mara ngapi kwenye magazeti tunasoma habari kuwa mtu kamwibia tajili wake na kunakuwa na kabila lake na dini yake? acheni kumjia juu pasipo kichwa wala miguu!!
    Mdau, nakupongeza kwa kutu habarisha!!! mwenye hasira na ajinyonge.

    ReplyDelete
  11. Mbona mnatilia maanani mambo yasiyo na umuhimu?....The real issue ni kuwa mume Mtanganyika kamnyonga na kumkatakata mkewe kikatili....anafungwa miaka 15 tu!! kisha anarudishwa Tanzania.

    What a shame!! Kwanza walipaswa kumnyonga huko huko, but nasikia Sweden wanafata sana "haki za binadamu"

    I say akitua tu Tanzania apelekwe kwenye kichiguu cha SIAFU kisha afungwe kamba wamle taratibu mpaka wammalize.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2010

    na wewe mtoa maoni wa thu may 06.08:00:00 pm umechemka vilevile wangesema mwafrika kutoka east afrika kamuuwa mkewe kikatili inge leeta maana. kwani sisi wote vyakula na maji na hewa tunavyotumia ni sawa hivyo kunauwezekano kabisa samaki mmoja akioza anaweza kuambukiza na alio nao karibu yahe!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2010

    Huyo bwana yuko Denmark na siyo Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...