Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bwana Mushi (wa tatu koshoto) akiwa na vingozi waArusha Press Club akiwemo Bw. Claud Gwandu (wapili kushoto) ambaye nimwenyekiti wa Klabu hiyo na Eliya Mbonea (wa pili kulia) katibu. Viongoziwanne waliopita waliotunukiwa ni waliosimama kutoka kulia, AngeloMwombela,M/kiti 2007- 2010; Nicodemus Ikonko,M/kiti 2003 - 2007; NoelThomas, Katibu 1993-2003 na Danford Mpumilwa, M/kiti 1993-2003.
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari tarehe 3 May 2010 iliadhimishwa kwa namna yake Mkoani Arusha ambapo wanahabari karibu mia moja walikusanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli mpya ya Stereo na kufanya kongamano juu ya siku hiyo pamoja na kuwatunuku vingunge wa habari mkoani hapo ambao walianzisha na kuiendesha Arusha Press Club yapata miaka ishirini iliyopita.
Klabu ya Arusha ndiyo iliyokuwa ya kwanza kabisa kwa Klabu za Mikoani kuanzishwa nchini na ilikuwa mistari wa mbele kuanzisha the Union of Tanzania Press Clubs nchini. Ingawa hapo katikati ilikuja kuyumba lakini hivi majuzi uongozi mpya umeteuliwa ambao umeahidi kuipaisha Klabu hiyo kurudia anga zake. Siku hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Mushi ambaye alikuwa mgeni wa heshima.
Mwenyekiti mwanzilishi wa APC, ambaye sasa ni Afisa Habari wa UN - Mahakamaya Rwanda na vilevile alikuwa Mwenyekiti Mwanzilishi wa Umoja wa Klabu zaHabari za Mikoa ya Tanzania, Danford Mpumilwa akitunukiwa cheti maalumu chakushukuliwa na Mhe. Mushi Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Viongozi wa enzi hizo wa Klabu hiyo wakifuatilia mada mojawapo ukumbinihapo. Kutoka kushoto, Noel Thomas, Danford Mpumilwa, Nicodemus Ikonko na Angelo Mwoleka.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...