Dear Uncle Michuzi,
Ninakitu kinanitatiza na hili swala la Jumuiya ya Afrika Mashariki: naomba ulifuatilie au kama kuna wadau unafahamu juu ya malipo ya dolla kwa wazawa kwa huduma ndani ya nchi na kwa wageni wanapokuja hapa kwetu.
Ni kuhusu chuo cha Kampala international University…. Wameanziasha campus hapa Dar es Salaam - Tanzania. Lakini cha cha kushangaza Wanawalipisha Watanzania kwa DOLLA za Kimarekani..... huu sio Ujanja wa kupata faida mara mbili... wakati Waganda wanaosoma chuo hicho hicho nchini Uganda wanalipa kwa pesa ya Uganda na sio kwa Dolla.
Ninahisi kama kunakitu hakiendi sawa hapa...... Tafadhali wadau wanaofahamu mambo haya tunaomba maoni na pia kujua suluhisho la shida hii.
Asante sana
Mtanzania halisi.
Ninakitu kinanitatiza na hili swala la Jumuiya ya Afrika Mashariki: naomba ulifuatilie au kama kuna wadau unafahamu juu ya malipo ya dolla kwa wazawa kwa huduma ndani ya nchi na kwa wageni wanapokuja hapa kwetu.
Ni kuhusu chuo cha Kampala international University…. Wameanziasha campus hapa Dar es Salaam - Tanzania. Lakini cha cha kushangaza Wanawalipisha Watanzania kwa DOLLA za Kimarekani..... huu sio Ujanja wa kupata faida mara mbili... wakati Waganda wanaosoma chuo hicho hicho nchini Uganda wanalipa kwa pesa ya Uganda na sio kwa Dolla.
Ninahisi kama kunakitu hakiendi sawa hapa...... Tafadhali wadau wanaofahamu mambo haya tunaomba maoni na pia kujua suluhisho la shida hii.
Asante sana
Mtanzania halisi.
Jibu ni rahisi! Nenda kamwone mzee Mwinyi atakwambia Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunza kunyoa.
ReplyDeleteIle ni takataka nyingine nchini kwetu. Yaani mkakimbilia kusoma tu hata bila kuvifanyia uchunguzi vyuo. Hebu amkeni na ndio maana wanakula pesa zenu.
ReplyDeleteWajanja hao wanajua fika kuwa Tanzania ni nchi ya waliwao ambao hawaoni tabu kuliwa!!! Acha kushangaashangaaa ndugu au wewe ndo kwanza umepewa uraia wa bongo juzi???? Hapa bongo ni tambarare no problem hata raia wa kigeni Akita kiwa mbunge Leo anaupata tu no problem!!! Sasa cha ajabu ni nini mbona kempisky unalipishwa dola na inachajiwa dola kwa saa unayospendi hulalamiki?? Acheni lawama fanyeni kazi kwa vitendo sio somjo ty kila siku na maswali Kama hayo kamuulize benno ndulu au mustapha mkulo!!! Intentional irregularalities are so immense and undealable in tz!! Kaeni msubiri tshirts na kanga oktoba si huwa mnaona mmeyapatia maisha mkipewa tshrts na kanga zikisindikizwa na porojo na ahadi ambazo unaona kabisa mtoaji haziwezi zaidi ya usanii??? Bongo bwana!!! Haya kanyageni twende titafika tu!!!
ReplyDeleteWatanzania bwana...taabu kwelikweli..!,kila kitu kigeni mnakimbili na mkipigwa changa la macho ndo mnarudi kutafuta ushauri,acheni ushamba na kudharau vitu vyenu.
ReplyDeleteMdau Mbagala.
aghh wamejua watanzania hawathamini vya kwao mpaka wakaamua kuwaleteana na vyuo kuwachezea akili zaidi. Wanajua kunamarket kubwa sana la sivyo wasingefungua hapo. Ati ili aseme nimesoma Kampala...LOL...kama unataka kusoma chuo cha nje ya nchi na ulipe mahela yote hayo toka nje ya nchi ukasomee huko huko kwao. Kusoma nje ya nchi unajifunza mengi zaidi ya kukaa tu darasani..
ReplyDeleteUtakuta vyuo vyetu vingi vinatoa elimu bora sana kuliko hicho lakini kwa vile watu wanataka waonekane wanasoma Kampala University basi watakimbilia hapo..
Wameona mafisadi wana dollar waganda watoe wapi dollar...Bongo zipo dollars za kumwaga....waache wajanja wachote tu
we wa kwanza ndo bwege nenda kachunguze vyuo vyatakiwa kuzidi na kuwa vingi kama nchi za jirani,nenda TCU uone kama iko chuo hakipo adi kwenye vitabu vyakuchagua chuo kipo..Swala hapa sio chuo nihayo malipo yao ya kijinga tulipe kwa hela zetu yani TZS kama wanavyowafanyia Waganda.
ReplyDeleteBig up kwa TZ naona vyuo vinazidi kidogokidogo sio kama enzi zetu..ila gharama zishushwe.we wa kwanza nenda kachunguze kwanza ndoutoe comments..Mie BINAFSI NILIENDA TCU ndonikapata data zote.sasa wewe nani kusema chuo cha ajabu?wao wamekiregister,nyie ndo mnaoshusha elimu za watoto.
Mbaya zaidi nilienda extra miles kwa kucheki kwa mtandao best universities in africa nanikakikuta..Tanzania vipo 2 kama si 3..naicho unachokiita chakijinga kipo..Haya ivyo vya maana kwako nikipi kilichoingia..?Watanzania lets do rwesearch kwa nza na tusome sana,tusiongee ongee..Kama unaitaji chuo nenda kwa mamlaka husika kama TCU
Ni kweli ni kichwa cha mwendawazimu! Wapo watu wa serikalini wengi wanasoma pale, lakini hakuna mtu analitilia maanani. Yale yale ya "Squre root" kila kitu ndivyo sivyo na hakuna anaye jali. Ankal hii issue unaweza kuituma "tume ya vyou vikuu?" Tafadhali hili lisiishie hapa!
ReplyDeletenyooo, ki chuo chenye kimeeeechoooooka eti dollar....na ninawaonea huruma wanafunzi wa kitanzania wanaosomea hapo..videgree vyenu na qaulifications vitaishia u-cashier ubungo buss terminor n vi dollar vyenu hiiiiiiivyooo, mmeliwa...labda ka vi dollar vya zimbabwe, hapo nitaenda kusomea hicho chuo kupoteza tu mda...njoooni tu, tumaini au mzumbe university!
ReplyDeletewatanzania amkeni, acheni kukimbilia kimbilia vi vyuo vya kigeni visivyo na vichwa wala miguu, kasomeni vyuo vya kitanzania UD/IFM/UDOM nk. kama unataka kulipishwa dollar na vyuo uchwara, basi tumbukia hapo "kampala Innternational University". Tanzania OYEEEEEE
ReplyDeletemimi ninachoona tukazanie walipishwe kwa TZS kuhusu chuo kipi kizuri nendeni Tanzania Commission for universities pale wanamajibu yote.Watanzania waajabu sana leo kimekuja kipya makelele,wakati ata icho mnachokiona cha maana nacho kimeanzia hukohuko chini.Halafu mbaya zaidi ata ivi vya ndani ya nchi pia mnasemaga vingine vya kipuuzi..ninachosema ukitaka chuo nenda TCU watakwambia vyuo gani wanavikubali hilo 1,pili watu someni jamani msianze kuzarau vyuo..pigeni kitabu na mfanye uchunguzi kwanza.NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK
ReplyDeleteMi ninachojua ni kwamba, kwa mtu yoyote ambaye anaelimu kidogo ya finance anao upeo mkubwa wa madhara ya kufanya hivi na sio suala la uganda tu kuna sehemu nyingi sana hapa tanzania huwezi kupata huduma kama hauna dollar za kimarekani, hivi hawa tuliowapa dhamana ya kukontrol pesa zetu (BOT) wako weapi na wanafanya nini?nahis hawa watu wana ki2 wanachofaidi make wametugeuza ndondocha siku nyingi ila mwisho upo tu kwani tumechoka sana tena sana,kwnini tudevalue pesa ye2 na kuvalue pesa za kigeni?au ni conditions za donnors? if yes let us know then,
ReplyDeleteWaTz ulalamishi. nchi yenu haina mwenyewe. Acha wa uganda wafungue vyuo vya juu. na sisi tuki nyuma yao.Kamau alisema ukweli.
ReplyDeleteSisi tuko hapa gongo la mboto tunachapa kitabu na kula dola. shlingi ya TZ ziii haijulikani hata kwa watanzania wenyewe
Tatizo la watanzania ndio hilo hapo mtu anauliza swali badala ya kujibiwa anaongezewa mzigo wa maswali. Je chuo hiki kinatambulika na TCU na kama ndivyo kwanini TCU wasiweke msimamo wa fedha inayo lipwa katika vyuo vikuu kwa wanachuo ambao ni wazawa kuwa fedha yetu wenyewe? tusaidiane jamani ndio tutafika
ReplyDeleteWATANZANIA TUMEZOEA KUSEMA BILA KUFANYA UCHUNGUZ HUYO ANAYESEMA CHUO CHA KIBABAISHAJI YEYE KAFANYA UCHUNGUZ WAPI
ReplyDeleteKAZOEA KUSIKIA KUNA ud, udom ifm NA VYENGINE VICHACHE HATAKI MABADILIKO HATA KIDOGO.
AENDE KWANZA TCU AKAFANYE UCHUNGUZ KWANZA WANAFUNZI WA KIU HATUKUVAMIA TU TUMEFANYA UCHUNGUZ KWANZA.
YEYE ALALAMIKIE SUALA HILO LA KULIPIA KWA DOLLAR TU SIYO VYENGINE
ACHA USHAMBA
Mimi binafsi nimesoma pale Postgraduate,sasa huyo jamaa asiite chuo cha kibabaishaji,pale kuna watu wamemaliza na wengine waendelea mpaka Master,ni serikali gani ambayo itaruhusu hali hiyo kama kuna ubabaishaji.Halafu kama mchangiaji hapo juu alivvosema hicho ni chuo best katika Afrika kuliko hivyo ulivyovikuta wakati unazaliwa,soma zaidi utaelewa tu.Mwisho rafiki ww lipa tu hizo dola kwa sababu wanaweza kuruhusu ulipe za KITANZANIA lakini kwa rate ya Dola utasemaje?Nakushauri usome tu,kwani ulipo ji-register si uliona masharti?kwa nini uskatae?Hiyo ni biashara ya watu,hutaki nenda kwenye hivyo vyuo vyako vya bure,waache waliokubali walipe.
ReplyDeleteNdio maana Tanzania hatufanikiwi katika mambo mengi yanayohitaji utaalam, hii ni kwasababu, katika suala zima la elimu na katika mpango mzima wa kutafuta elimu, tunafikiria gharama, elimu bila gharama sio elimu na huwezi kupata elimu ya bure, bila kulipia gharama, sasa hivi ukichangisha mchango wa harusi ndani ya wiki mbili, utapata mamilioni ya pesa, ila ukipitisha tangazo la harambee kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kusomesha watoto wetu, hata kwa mwaka laki hupati, ipi nafuu kulipa hizo dola KIU, au kununua mcreti ya bia na kunywa halafu ukakojoe na huku afya imeshaaribika, tatizo ni ufinyu na umasikini wa mawazo. Elimu ni kitu muhimu sana. Sio kizazi hiki kinachoishi Tanzania, labda baada ya miaka hamsini, hii product ya tanzania ya std seven, ina matatizo sana. Kuna rafiki yangu nilimaliza naye pale IFM, sasa hivi anamalizia postgrduate yake ya Computer Science pale KIU, mambo yake shwari, na si tu akimaliza ataajiriwa bali atakuwa na uwezo wa kujiajiri, mtaalam mzuri wa web design, database design, na pia ni computer programmer mzuri. Mimi mwenyewe nipo mbioni kwenda kuchukua master ya computer pale. Halafu inatakiwa kufanya uchunguzi wa kutosha, sio kuropoka tu, nenda TCU, katafute data, wewe ulizaliwa ukakuta chuo kimoja UDSM, na vingine vya MZUMBE, SUA, IFM n.k Ila unashindwa kuelewa kitu kimoja elimu, sio ukuu wa majengo, umaarufu, pale KIU, walimu wengi wanaofundisha wamesoma nchi mbalimbali za ulaya hasa nchi za Scandnavia, wana PHD, wapo watanzania, waganda na wengine kutoka Ulaya. Kwa mfano kuna mwalimu mmoja kasoma Sweden, ni mtaalamu ktk fani ya kompyuta na kasomea mambo ya automation operating systems. Ni mtaalam katika mifumo ya kiroboti. Ni mtanzania anahitajika sana Ulaya. Uganda wanamfaidi kwenye vyuo vyao sisi wenyewe na vyuo vyetu vya ada nafuu tumeshindwa kumtumia. Au wewe unapenda akalipe ada pale mlimani (UDSM) YA LAKI SITA, ndio unaona umepata elimu, wenzako wanaenda kutafuta degree ulaya kwa mamilioni ya pesa, wakirudi tanzania, wakipata kazi nzuri unasema, mafisadi, wakati wao wanasoma kwa ada kubwa wewe ukaona gharama, ukaenda mlimani kuchukua SOSHOLOJI, sasa hivi unahangaika kazi hupati. HAYA BWANA KAMA ELIMU NI GHARAMA JARIBU UJINGA
ReplyDeleteMambo mengine tunajitakia wenyewe. Tusiwabeze wanaokwenda kusoma pale. Si rahisi upata chuo cha serikali au watu binafsi hapa TZ.
ReplyDeleteNi vijana wangapi wamekimbilia nje si kwa sabb ya pesa bali kukosa kukubaliwa ktk vyuo vya TZ.na kule wanafaulu na kuwa wafanyakazi wazuri hapa tz.
Acha tunyolewe kiwendawazimu. Watz sijui tulirogwa na nani! kila mtu mbinafsi, hata wale waliopewa dhamana kuongoza wananchi.
Nawashukuru sana wadau mnaohimiza kuhusu umuhimu wa kufanya research kabla ya kusema. binafsi nachukia watu wanaoropoka bila kufanya utafiti wa kina juu ya kile wanachokisema. Hao watu wanaosema chuo ni feki, waende vyuo vipya kama UDOM wajionee. Ubora wa chuo ni facilities, kama vitabu, walimu na ratio kati ya mwalimu mmoja na wanafunzi. Lets be scientific and stop speaking like laymen! Kuhusu kulipa kwa dola nakubali ni vema tulipe kwa Tsh, hata hivyo kuna vyuo kama New Horizon ambavyo kozi ya IT kama Cisco tu unalipa dola 800, na ada ya mtihani dola 400. Na hiyo ni kozi ya miezi sita tu!...Lets find facts guys!!
ReplyDeletesamahanini wadau,nilikua naomba kupata ukweli,je chuo hiki cha Kiu kinatamabulika na tcu?
ReplyDeleteWatanzania tuache kulalama bwana hamjui kuwa sisi tupo nyuma sana kielimu ata vyuo vyetu ni havipo kwenye standard za kimataifa ndo maana watanzania waliowengi wanakimbilia kusoma nje ya nchi.Na kuhusu KIU acheni kama kilivyo kwani kipo kwenye ranki za kimataifa and well known around africa,swala la kulipa kwa dollar si kitu cha kushangaza sana kwani ata mahoteli makubwa hapa tz tunalipa kwa dollar Na kama uiwezi garama za ni bora ukasome vyuo vyetu vya kayamba vya sh laki tano,
ReplyDeletejaman mi np njia panda, nimechaguliwa kwnd kusoma pl sa kutokana na mchango wenu nashindwa kujielewa
ReplyDeleteWadau nimekubali kuna watanzania mandondocha tena mazuzu. na wengine wana upeo wa hali ya juu jiulizeni kwa nn baadhi ya viongozi au maprofesa pamoja na wakufunzi wapeleka watoto wao kwenda kusoma nje ya Tanzania? ELIMU NI GHARAMA. tumezoea kulundikana darasan hata mwalimu akufundisha humsikii na usahihishaji wake nao niwataabu jiulize lecturer ana fundisha wanafunzi mia sita course mbili je huwa anasahihisha kiuhakika? Pumbafu yenu mnaokikandia KIU. OK nina taka kusoma Masters of Arts in Conflict Resolution and Peace Building chuo gani kina fundisha hapa Tanzania? Amka wewe jitume na acha kulala mika. wewe na ka dgr chako cha UDSM IFM UDOM unabakia kuwa customer service kwenye makampuni ya sim na unalipwa mshahaa kulingana na ada uliyo isomea. Guys wake up. tumeona hivyo vyuo unavyo visema eti Tumaini Mzumbe sindio mnafundishwa na Ma tutorial waliofaulu kwa kukuibia tuna wafaham sana leo hii unakandio chuo che PhD holders wakutosha na maprof. Mdau hapahapa TZ.
ReplyDeleteelimu ya watanzania wengi waliomaliza vyuo vikuu ni ndogo hawawezi kutumia akili kutatua matatizo ndiyo maana wageni wanafaidika hapa nchini mwao kama msomi jaribu kuwa na sababu kwanini hivi alafu toa ufafanuzi sio kuwa mropokaji tu pole sana ndiyo maana nimesepa bogo
ReplyDeletejamani mimi sioni cha ajabu na ni vizuri vyuovya aina hii vije ili kushtua elemu yetu na wakuu wa vyuo vyetu wawe wabunifu na kuweza kusoma alama za nyakati. Nafurahishwa kwa challange hii na ni fursa kwa UD, UDOM na vingine kuangalia njia na kujiongeza mpaka kenya UG na shm nyingine. Watanzania msiwe waoga na pendeni changamoto kwani zitawasaidia mnataka mbaki na vyuo vyenu amabavyo havishindani globaly mtafika vipi na mtapambana vipi na masoko ya kimataifa?????????
ReplyDelete