Mwenyekiti wa timu ya Azam Fc,Said Muhammad Said akiwa na mchezaji mpya wa timu hiyo,Mrisho Ngasa alietokea Yanga wakati akikabidhiwa uzi wake mpya leo katika makao makuu ya klabu hiyo.
Nyanda mpya wa timu ya Azam FC,Jackson Chove akionyesha uzi wake mpya mara baada ya kukabidhiwa leo na Mwenyekiti wa timu hiyo,Said Muhammad Said.Nyanda Njovu alikuwa akiidakia timu ya JKT Ruvu.
Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC,Said Muhammad Said (kati) akiwa na wachezaji wake wapya,kushoto ni Mrisho Ngasa na kulia ni Jackson Chove.

Wakati mchezaji Mrisho Ngasa akiamishwa kwa ada ya shilingi milioni 58 kutoka timu yake ya zamani ya Dar Young African, timu ya Azam imemnyakuwa kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove aliyekuwa amebakisha miezi sita kumaliza mkataba wake na JKT Ruvu ambapo timu hiyo imeshamalizana na uonozi wa JKT kwa kulipa kiasi cha shilingi milioni tatu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa wachezaji hao wapya Mwenekiti wa Azam Fc, Said Muhammad Said alisema kuwa baada ya kuwapata wachezaji hao lengo la klabu hiyo ambalo ni kuchukua Ubingwa wa ligi Kuu ya Vodacom katika msimu ujao.alisema "Wachezaji wazuri tunao hatuna sababu ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2010-2011".

Nae mchezaji mpya wa timu hiyo,Mrisho Ngasa alisema "Nitahakikisha timu yangu mpya inafanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,Najua kuna kila aina ya ushindani huko niendako lakini nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kiwango changu hakishuki na kuipatia Ubingwa wa Ligi Luu ya msimu ujao timu yangu mpya". aliongeza Ngasa.

Naye golikipa mpya wa timu hiyo aliyehamishwa kwa kitita cha shilingi milioni tatu kutoka JKT Ruvu, Jackson Chove alisema kuwa,baada ya kukosa kusajiliwa na timu hiyo katika msimu uliopita sasa amefika katika timu ambayo alikuwa anaipenda kutokana na kuwa na mapenzi na klabu hiyo tajiri hapa Tanzania. "Najua kama kuna ushindani mkubwa katika timu yetu lakini nitahakikisha nafanya mazoezi na kuongeza juhudi zaidi ili kiwango changu kisishuke" alisema Chove.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    Inaonesha Kilichobakia ni Rushwa tu ila hilo Halimzuii Simba kutowa Ubingwa tena. Seif.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2010

    Yaani Mrisho Ngasa kanunuliwa kwa hilo dau for what? Mrisho si mchezaji na hana kipaji chochote. Najuwa wengi mtakasirika lakini ndivyo tulivyo watanzania hatupendi kuambiwa ukweli, hivyo sitanshangaa. Huyu yanki (Ngasa) ukisoma humu kwa Michuzi ama magazeti ya TZ utamuona ni bonge la mchezaji. Nilipokwenda Bongo mwaka jana nilibahatika kumuona katika lile kombe la challenge. Yaani, it's a pitty...jamaa ni kukimbia tu na hana any talent. If anybody knows soccer, huyu yanki namfananisha na Filipo Inzaghi wa AC Milan (ila Inzaghi kidogo anastahili sifa) but not this dude. Then we wonder why Taifa Stars haifiki mbali mashindanoni, you can never win with players like Ngasa, he is simply useless na ndiyo maana alishindwa kupata namba West-Ham.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2010

    Wewe hapo juu acha chuki binafsi hizo, Ngasa ni bonge la mchezaji ndiyo maana kachaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi, wewe inavyoonyesha ni mbumbumbu wa soka umejaa chuki binafsi tu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Utasemaje Ngassa si mchezaji wakati ushindi wa Taifa Stars always unamtegemea yeye! That is the best we have in Tanzania utake usitake. Acha chuki Binafsi mnazi wa Simba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...