Mwanamuziki mkongwe, Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi, na kikosi chake kikali watashambulia jukwaa katika miji ya Beirut na Cairo kwenye tamasha la Spring Festival 2010 tarehe 14 na 15 mwezi huu.
Bendera ya bongo itapeperushwa ipasavyo, na kama wahenga walivyonena, asiye na mwana itabidi aelekee jiwe!
Safu ya Ras Nas ina wanamuziki Uriel Seri (Ivory Coast), Chuck Frazier (USA), Karlos Rotsen (Martinique), Larry Skogheim (Norway) na Dag Pierre (Sweden). Wadau habari ndiyo hiyo!


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...