Na Veronica Kazimoto – MAELEZO.
Dar es Salaam 

Rasilimali za misitu zinakadiriwa kuchangia asilimia 2 hadi 3 kwenye pato la Taifa na zina umuhimu mkubwa sana hapa nchini kwa kuwa ni chanzo muhimu cha nishati inayotumika katika makazi yetu.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Shamsa Mwangunga wakati akizindua kamati ya kitaifa ya ushauri ya misitu iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa misitu ni chanzo muhimu cha nishati, kwani asilimia 95 ya nishati hiyo hutokana na miti.

”Shughuli mbalimbali zinazofanywa katika maeneo mbalimbali ya misitu huchangia katika kuondoa umaskini miongoni mwa jamii ya Watanzania, iwapo haya yote yangeingizwa katika mahesabu ya pato la taifa mchango wa sekta ndogo ya misitu ungekuwa mkubwa kuliko kiwango kilichoainishwa hapo juu” Amesisitiza waziri Mwangunga.

Waziri Mwangunga amezindua kamati ya kitaifa ya ushauri ya misitu ambayo inaundwa na wajumbe 15 kutoka serikalini, vyuo vikuu, taasisi zisizo za kiserikali na sekta binafsi.

Uzinduzi huo umeenda sambamba na uteuzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ambapo Profesa Said Idd ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ameteuliwa kuwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti ni Bi Anna Maembe kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Kamati ya Kitaifa ya Ushauri ya Misitu inaundwa kwa mujibu wa Sheria ya Misitu Na 14 ya mwaka 2002 kifungu cha 10. Kazi za kamati kwa mujibu wa sheria hiyo ni kumshauri Waziri juu ya mambo yote yanayohusiana na ukodishwaji wa misitu, kutangazwa kwa hifadhi za misitu, usimamizi wa misitu ya hifadhi na mapitio ya sera ya misitu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2010

    Veronica, asante kwa taarifa hii. Ni vizuri kuwa inachangia kwa asilimia 2 hadi 3 kwenye pato la taifa, ila tunapoteza asilimia ngapi pia kila mwaka (hasara)? Tafadhali usiache kunijibu.

    Thanks Veronica.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2010

    HAPO WAZIRI MWANGUNGA HAJAELEZA KUWA NI MISITU GANI?[YA ASILI AU TUNAYOPANDA ?.NA KAMA NI MITI YA ASILI KWA KWELI HAINGII AKILINI.KILA MTU ANAONA NA AMEONA TUMEKATA MITI KIASI GANI NA TUTAISHIA WAPI?.TUTAFUTE SOURCE NYINGINE YA KUONDOA UMASKINI SIO MITI YA ASILI?.NA KAMA NI MITI YA KUPANDA ITAKUWA SAFI NA SAWA.LAZIMA TUANGALIE UMUHIMU WA MITI KATIKA UCHUMI WA NCHI KWA UJUMLA.TUNATAKIWA KUANGALIA THAMANI YA MISITU KWA UJUMLA SIO TU KUKATA NA KUPATA PESA.MISITU INA REGULATE CLIMATE.MVUA NI MATOKEO YA MISITU,MISITU INATUMIKA KAMA CARBON DIOXIDE ABSORBERS.MISITU NI MAKAZI YA SPECIES WENGINE[WADUDU,WANYAMA WA PORINI,NA MISITU NI DAWA KWA WANYAMA WA POLINI NA BINADAMU.SASA IMPACT YA KUKATA MITI NI TUTAKOSA MAJI KATIKA MITO,MIFEREJI NA HATIMAE HATA KUKOSA UMEME.KWANI TANZANIA INATEGEMEA UMEME UNAOTOKANA NA MAJI KWA ASILIMIA 99.IMPACT NYINGINE NI HATUTAKUWA NA MAVUNO[DROUGHT],NA IMPACT NYINGINE CLIMATE CHANGE AND GLOBAL WARMING,HAPO KUTATOKEA VIMBUNGA,WANYAMA WATAKUFA KUTOKANA KUWA HAWAWEZI KUHIMILI HALI YA HEWA,WANAYAMA WATAKUFA KUTOKANA HAKUTAKUWEPO NA MAJI NA CHAKULA CHAO[MAJANI].MFANO MMOJA TUMEONA MWAKA JUZI HUKO KENYA WANYAMA WA PORINI WALIKUWA WANAKUFA.SASA KUTOKANA NA HAYO YOTE NILIANDIKA HAPO JUU,NI KWAMBA UMASIKINI UTAONGEZEKA KWA KIWANGO KIKUBWA NA NI BALAA KAMA MISITU YOTE
    IKIMALIZIKA.NA NAOMBA NIMWELEZE WAZIRI KUWA KUNA ALTERNATIVE NYINGI ZA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI NA SIO KUKATA MAGOGO KWA AJILI YA KUINGIZA PESA.HII NI SAWA NA KIPOFU ANATEMBEA NA HAJUI KAMA HAPO MBELE KUNA SHIMO.TUWEKE SERA YA KUHAMASISHA WANANCHI KUPANDA MITI ILI WAVUNE KWA MAITAJI YAO NA SIO MITI YA ASILI.MITI YA ASILI IPO HIPO HAPO KWA SABABU YA KIJIOGRAFIA NA ENDAPO UTAITOA INA MAANA KUNA VITU VINGI VITAADHIRIKA.HATUJAIJUA NA KUISOMA ENVIRONMENT VIZURI NA KUJUA UHUSIANO WAKE KWA MAISHA YA BINADAMU.LET US BE SMART AND WISE ON THIS MATTER."MUNGU IBALIKI TANZANIA NA WATU WENYE MAWAZO MAZURI YA KUENDELEZA NCHI.AMINA
    MDAU USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...