Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
Tamko kwa Vyombo vya Habari
Mei 20, 2010


Siku ya Jumapili, tarehe 16 Mei, mnamo saa 2.30 usiku, mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikimbia na kumpita mlinzi aliyekuwa mbele ya Ubalozi wa Marekani, akawasha moto kwenye chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na kisha kuirusha chini ya moja ya malori mawili ya kubebea maji yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ukuta wa Ubalozi.
Chupa hiyo ilivunjika lakini haikuweza kulipua moto. Walinzi wa Kampuni ya KK wanaolinda ubalozini hapo walimkamata mara moja kijana huyo kabla hajaweza kurusha chupa ya pili. Hakukuwa na mtu yeyote aliyejeruhiwa wala mali yoyote iliyoharibiwa katika tukio hilo. Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania aliwasili sehemu ya tukio sekunde chache baadaye na kumkamata mtuhumiwa. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.
Baadhi ya maelezo yanayotolewa kuhusu tukio hili si sahihi, yamekuzwa na kutiwa chumvi mno na yasiyo ya kweli, yakidai kuwa mvulana huyo aliingia ndani ya ubalozi. Hii si kweli. Hakukuwa na mtu yeyote aliyeweza kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.
Taratibu zetu za kiusalama za kuzuia wahalifu kuingia ubalozini zilidhihirisha ufanisi wake hapo Mei 16. Walinzi wa kampuni ya KK na Polisi wa Tanzania walishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa. Tunawashukuru sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    Huyo mtoto alikuwa na nia ya kwenda kufunguliwa mashitaka nchi Marekani na kutegemea afungwe ktk magereza ya Marekani, maana maisha ya Bongo anayaona magumu sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Huu ni ugaidi ule ule wa siku zote. Jamani wafundisheni watoto mambo yanayojenga badala ya itikadi za kulipua na kuuwa wengine. Hawa ni wale wale ambao dini yao hawataki iguswe badala ya kuwakemea na kuwarekebisha. Kwa maoni haya najua nimefungulia bomba la matusi kutoka kwa wahusika

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Taarifa imetolewa na afisi ya nani? Michuzi? Au...nani sasa? Tuwe makini sana katika kuandika na kutoa taarifa hasa zile zinazoisemea serikali. Kwa nini mtu asipotoshe kwa taarifa kama hii isiyo na mwenye? Nina wakumbusha maafisa wetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    Wewe mtoa maoni wa thu,may 20,04:18:00 pm.unaposema hawa ni wale wale una maana gani ni nani hao ambao hawataki dini yao iguswe na dini gani hiyo inayowafundisha waumini wake waue watu wengine?unapotoa maoni kuwa mwangalifu.
    BY MREKEBISHAJI

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    At least in this intance, it makes sense kuhusu hii habari. Maana yake ilivyoripotiwa hapo mwanzao ilikuwa inaonyesha uzushi mtupu.
    Haiwezekani mtoto wa miaka 14-15 aingie ndani ya ubalozi huo (tena unaolindwa kuliko balozi zote duniani)na silaha kama vile anaingia kwenye nyumba ya jirani.
    Labda hili litakuwa fundisho kwa waandishi wetu wenye kurukia stori bila ya kuzifanyia utafiti wa kina.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2010

    Huyo mtoto hao polisi waliomkamata walimshuhudia akifanya hayo anayotuhumiwa kayafanya, au wameamini moja kwa moja hayo waliyoambiwa na hao walinzi wa KK? Ikumbukwe kuwa hao walinzi kuna uwezekano mkubwa sana kuwa wata-side upande wa 'boss' wao, yaani Ubalozi wa Marekani, hicho ndicho kinachowaweka mjini ati, tena usikute hata 'statement' yao huko polisi, iliongezwa chumvi, ili pengine wapate hata kupandishwa vyeo na hao KK!
    Au pengine kuna ushahidi wa CCTV Cameras.

    Pili, huyo 'mtuhumiwa' ni mtoto ama kijana mdogo, hivyo tunatumai kuwa taratibu zinazohusu watoto na vijana wadogo walio na 'mgogoro' na sheria zitafuatwa, siyo kwa vile ni marekani inahusika basi tutetereke. Hapana.

    Mwisho, muitikio ambao jeshi la polisi linasemekana kuutoa kwa hili tukio, nadhani ulikuwa unahitajika zaidi (na nadhani bado unahitajika) kwa tukio kama lile la kule kwetu Moshi, ambapo yule mtoto wa miaka nane alitekwa nyara na watu 'wasiojulikana' na kupelekwa Uganda na baadae watekaji nyara hao kudai pesa kama kigezo cha mtoto huyo kurejeshwa kwa wazazi wake. Polisi sijui wamefikia wapu kuhusiana na wale watoto wengine wawili ambao inasemekana kuwa bado wako Uganda.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2010

    huyo atakua amenyimwa visa ya marekani tu,sas anataka kulipiza kisasi,teh,teh

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    mpuuzi sana huyo,hana akili,akafie mbele na sheria zichukue mkondo wake.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    season finale...the cover up!

    Kitendo cha huyu dogo kuwapita walinzi wakiwa wamelala, kwenda hadi kwenye tanki la mafuta bila kustukiwa na kupasua chupa ya kwanza juu ya tanki iliyowaamsha walinzi kinaonesha ni jinsi gani ulinzi wa hapo ulivyo lege lege!

    Mimi nlipata bahati ya kuwa mmoja ya wapita njia. Sote tulihaha kutokana na mpasuko ule, gari zetu zilisimamishwa na walinzi walikimbilia upande wetu wa barabara wakijua ni bomu.

    Sasa wanajidai eti aliwapita akikimbia! ilikuaje hawakumsimamisha usiku wote huo hadi awapite na kwenda kutupa chupa!

    Wao wakubali udhaifu na kuufanyia kazi denial haisaidii wakati wananchi tumeshuhudia

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2010

    Jamaa hapo juu ansema ukweli mtupu. Watu wanafundishwa chuki na matkeo yake ndio kama kwemye hii habari. Amini unacho amini lakini usijaribu.Chuki ya Marekani na nchi nyingine za Ulaya itatufikisha pabaya.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2010

    Maoni yangu yatolewe, msiyatie kapuni.


    Hebu Acheni maneno ya uongo. Huyo ni
    Alkaida na ni gaidi kama wale wooote wa Imani ya Kujilipua.

    Ingekuwa dini nyingine ungesikia maoni na matusi. Nabii Tito hapa alitolewa na watu wakamtukana mitusi tani yao. Lakini mtoto huyu hata jina la mtoto limefichwaa. Halafu leo wametangaza jina huku wakimtetea eti ni yatima.

    Huu ni ugaidi wa kawaida kwa dini yenu. Siitaji Dini lakini wote mnaijua. Kwani ndiyo Dini pekee inayojilipua karne hii ya 21. Na sijawahi viongozi wa dini hii wakikosoa tabia za namna hii. Woote wako kimyaaaaaaaaa.

    Hata siamini kama michuzi atayatoa maoni yangu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2010

    If you want to be a Cellebrity nowadays....NJIA NDIO HII....mfanyie chochote Marekani hata japo kuongea kwa sauti kwenye simu kwa lugha yako.....tamka nenoi BOM....Ushakuwa Cellebrity!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2010

    mh jamani tanzania yetu hatutaki walipuaji wa kujitoa mhanga!!

    shindwa ktk jina la Yesu

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2010

    waseme tuu walikuwa wamelala mbona tunawaonaga wakila mbonji kila leo?? wanajiamini sana kwamba hakuna mtu atasogelea pale hivyo wanajilalia tuu fukuza kazi hao hamna kitu hasa hao kk sekyuriti wanajionaga sana tukienda kuomba visa utadhani wao ndio makansela nyodo nyingiii na wale wa ubalozi wa uingereza punguzeni njaa ukipata visa wanakuzongaa uwakatie kitu kidogo utadhani wao ndo wamekupa visa shwain sana labda hizo kamera nazo ziwe zilikuwa zimelala vinginevyo job kwishney!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2010

    SASA HATA TUKITENGENEZA PROFILE YA WALE WENYE DINI YETU ILEEEE.....BADO NITABU! KWANI HUYU KAJA GHAFLA TU KWA NJE. iLA NINGEPENDA NIJUE ANA ABUDU WAPI?

    NB: HII ITATUSAIDIA SANA, KUONYESHA HIYO JAMII HATUILAUMU BILA MISINGI!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 21, 2010

    wame edit hao walinzi walilala

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2010

    mnaogopa nini kumtaja jina?? ati mvulana wa miaka blah blah tajeni jina kama yule aliyetaka kulipua time skwea new york namna hii " faisal shahzad" kwani kuna tatizo gani hapo kwenye jina?? kama ni john au george wekeni wazi hata kama ni mashaka semeni eboo inaelekea ile story ya mwanzo ina ukweli zaidi WALINZI MLIKUWA MMELALA FULL STOP!! ndio mtajua supu ya mbwa ni dawa ya ukimwi!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2010

    mi naungana mkono na mtoa maoni hapo juu kwamba huyo kanyimwa visa , analipiza kisasi, magaidi wangelipua hapo maana wanakuw ana plan zao za muda mrefu wakipiga wanafanikiwa aslimia kubwa , na isitoshe kama magaidi wakitaka kupapiga hapo sidhani kama watashindwa ... achana nao hao ...

    huyo mtoa maoni may 20,04:18:00 pm
    akili zake hazina akili

    alitaka kusema waislam ndo wanafundisha kuua watu.

    mpuuzi na hana akili tumuogope kama ukoma huyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...