Hiyo ndiyo hali halisi kama nilivyoshuhudia leo asubuhi majira ya saa tatu nikiwa njiani kuelekea nje ya mji wa Mahenge wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, katika shughuli zangu za kikazi. Unaona jinsi gani magari yanavyokata viuno kwenye miundombinu yetu. Kwa kweli inakera kwani basi limefunga njia katika kijiji cha MSOGEZI kama kilometa saba hivi kutoka mji wa MAHENGE.
Limetuchelewesha kwa takriban saa tatu mpaka trekta ya Halmashauri ya Ulanga ilipowasili kuondoa karaha hiyo. Mvua ilikuwa inanyesha, kwa ujumla wengi wamekereka. Unaona na gari yenye namba za kiserikali, nadhani aliyekuwamo atafikisha ujumbe kwa waheshimiwa wenzake kwani alikuwa miongoni mwetu tuliochelewa katika safari zetu.
Ni mimi Mdau
Emmanuel R. Manyanga
emmanyanga@yahoo.co.uk
{Safarini Kikazi-Mahenge (Ulanga)
Ni mimi Mdau
Emmanuel R. Manyanga
emmanyanga@yahoo.co.uk
{Safarini Kikazi-Mahenge (Ulanga)
Bongo tambarare. Safari ni safari tu utafika mdau. Usihofu ndiyo maisha. Usitegemee mtelemko tu. Kuna milima, mabonde, utelezi na kila aina ya ghasia ili mradi tu ikaitwa safari.
ReplyDeleteMdauzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
Bara bara nyingi za kuunganisha Miji mikuu ya mikoa na wilaya au vitongoji ndio ziko hivyo.
ReplyDeleteWatanzania wa kawaida (wanaoishi mikoani) wamezoea hali hii, ni kawaida kwao. (Hivyo hawaoni kama ni tatizo au wamekata tamaa ya maisha)
Kwa wale waliozaliwa na kukulia mijini, hili ni tatizo lisolowahusu. (hivyo si juu yao)
Kwa wale waliopata nafasi ya kwenda nchi zilizoendelea kama huko Amerika ama Ulaya.. hawataki kurudi (wanaona sisi waTz tumechoka, na wajinga)
Viongozi walioko madarakani. (Wengi hawajui wanafanya nini hapo walipo.. waligombea nafasi wakidhani ni piknik)
Na listi inaendelea....
Ilo shangigi linakwenda kuomba kura kwa wanakijiji, sijui mbunge vwa uko anajiskiaje anavyo ona ali kama iyo.
ReplyDeleteMsijali kiangazi si mbali!! After all hayo si ndiyo maisha bora mliyoahidiwa jamaniii!
ReplyDeleteHalafu angalia lile basi. Sijui kwa nin i lilikua linatumia njia za mkato nalo. Likianguka hapo si watu wanakufa.
ReplyDeleteHalafu linajua nji hizo hazina traffic police ndio maana linakatiza huko.
Hiyo ni hatari sana.
Mbunge wa hili jimbo ana gari la Mill 90, tena hilo ni lakuendea kwa nyumba ndogo tu,acha lile la mama watoto, na hause boy. teh teh teh
ReplyDeleteHivi mtanzania wa kawaida ni yupi? na asiye wa kawaida ni yupi? tafadhali naomba ufafanuzi ili tuende sawa!
ReplyDeleteNdio wadau,kama huyu mheshimiwa anaenda huko kwa shughuli za kila siku big up sana but kama ndo anenda kuomba kura alaaniwe.Serikali inanunua magari ya gharama na yenye nguvu ili wabunge na watumishi wengine wa wilayani na majimboni wafanye kazi bila shida lakini cha kushangaza ndugu wabunge siku zote wako mijini na hayo mashangingi!kama unajua jimboni kwako hutokaa kwanini usiombe corolla tu ili kupunguza gharama za uendeshaji? au ndo haikuhusu!laana si lazima uuwe mtu!
ReplyDelete"Ni vibaya sana kumfanya mtu mijinga ambaye hajui kama unamfanya mjinga".kama ndugu wabunge mngekuwa mkiishi na wapigakura wenu siku zote mnazotakiwa kuwa nao na kuwasikiliza shida zao kusingekuwa na shiad wakati wa uchaguzi kama sasa!cha ajabu mmegeuka manyang'au.
KWELI HIYO NI BARABARA YA WILAYA, NI BARABARAYA KUPITA GARI KAMA BASI KATIKA KARNE HII YA 21 NA BAADA YA UHURU TAKRIBANI MIAKA 50? WE NEED TO RE-THINK OUR DEVELOPMENT STRATEGIES AS WELL AS THINKING OUTSIDE THE BOX, WE NEED NEW BRAINS IN OUR DECISION MAKING ORGANS. HII GENERATION YA VIONGOZI WA UHURU IONDOKE TUJE NA WAPI AMBAO HAWAKUHUSIKA KABISA NA MASWALA YA UHURU,WENGI WAO WAMEAMBUKIZWA HUU UGONJWA WA KUTOFIKIRIA MAENDELEO YA NCHI. EBU TUIPE USUKANI GENERATION YA KILEO AMBAYO HAIKUAMBUKIZWA UGONJWA HUU
ReplyDeletejaribu kulinganisha hiyo barabara na twin tower,nyumba ya mkuu wetu wa fweza,vijisenti, epa n.k utapata jibu ya bongo za watanzania hapo maamuzi ndo yanapoonekana.sioni adhabu ya kuwafaa wafanya maamuzi wetu mbali na viboko vya matako tena hadharani.
ReplyDeleteNdugu watanzania. Huu ni uchochezi, acheni uchochezi kabisa. Hivi hamuoni aibu kuanza kulaumu werikali na wabunge sijui kuhusu barabara hiyo ya mwituni wakati mnajua fika kuwa wakaazi wa Dar hupoteza karibu masaa sita (6) kila siku kwa ajili ya kwenda na kurudi kazini (au shughuli)?
ReplyDeleteHamjui kuwa huo ni upotevu wa mabilioni ya pesa kila siku iendayo?
Inabidi mfikirie kwanza kabla ya kufungua vinywa vyenu. Hivi mpaka leo hii nani asiyejua kuwa Dar ndiyo moyo wa uchumi wa Tanzania? Halafu mnaanza kulalamika eti barabara mbaya, ... ooh nini sijui, mara basilimeziba barabara! Jamani jamani jamaniii!
Serikali ya nchi yetu ina mipango mizuri kabisa. Inafanya kazi kwa kutegemea kipato na bajeti iliyopo! Hatuwezi kufanya kila kitu kwa mara moja. Serikali inatia kipaumbele katika miundombinu muhimu kwanza, tukianzia na barabara za Dar kwanza.
Dar ni lazima ikombolewe katika huu utumwa wa kusota barabarani ndipo nguvu itaelekezwa huko kwingine hatimaye.
Lakini kitu muhimu ni kuwa pamoja na barabara za nje ya Dar kutokuwa katika levo inayotakiwa, hutumia muda mfupi kusafiri kulinganisha na Dar. Inabidi mutuhurumie wakaazi wa Dar!
Ahsante
Nilisoma Kasita seminary miaka ya 90 na hii barabara ilitengenezwa na kampuni toka thailand ili kuchimba madini ya rubi na sio serikali kabla ya hapo wanavijiji walikuwa wakitembea mpaka mahenge mjini ma walimu pia ilikuwa hivyo.baaba ya kumaliza madini ndo wanavijiji wamebaki na barabara.Lakini ni sehemu iliyokuwa na utajili sana hasa madini.muulizeni Liyumba anakujua sana huko.pole sana kaka.
ReplyDeleteHaya ni matunda ya kuendelea kuwatukuza viongozi waliotufikisha hapa.Ukiona vyaelea vimeundwa na ukiona vimezama.....
ReplyDeleteViongozi wetu waerevu sana. Badala ya kujenga barabara ziwe nzuri na kununua gari za bei nzuri, wao wananunua mashangingi ya bei mbaya ili waweze kupita kwenye hizo barabara mbaya.
ReplyDelete