Sean Kingston
Msanii maarufu kutoka Jamaica Sean Kingston anatarajia kuwasili nchini leo saa 4 usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Sean Kingston ataingia nchini akiwa na kundi la watu 13 ambao ni sehemu ya bendi yake itakayotumbuiza jijini Dar es Salaam usiku wa tarehe 15 Mei 2010 katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye Onesho la washindi wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

Ratiba Yake ya Sean Kingston kwa ufupi:
Sean Kingston atatoa salaam fupi akitoka nje ya uwanja wa ndege kwa watakaokuwa wamekuja kumlaki kabla hajaelekea kupumzika katika hoteli ya Double Tree by Hilton iliopo Masaki Dar es Salaam.
Alhamisi anatarajia kuzungumza rasmi na wana habari katika hoteli ya Double Tree by Hilton kuanzia saa 5:30 (tano na nusu asubuhi).
Atakwenda kwenye vituo kadhaa vya radio na Televisheni kwa ajili ya mahojiano ya moja kwa moja na baada ya hapo atatembelea kampuni ya bia Tanzania (TBL).
Ijumaa msanii Sean Kingston anatarajia kuendelea kufanya mahojiano ya moja kwa moja na baadhi ya vyombo vya habari na mazoezi ya nafasi yake ya utoaji Tunzo katika halfa yake usiku huo.

Usiku wa utoaji Tunzo ambao utafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubliee tarehe 14 Mei 2010, Sean Kingston hatotumbuiza bali atashiriki kama mgeni mwaalikwa na atatoa Tunzo kwa mshindi wa kinyang’anyiro cha WIMBO BORA WA RAGGA. Usiku huu ni kwa waalikwa tu.

Tarehe 15. Mei. 2010, Sean Kingston atafanya onyesho kamili katika ukumbi wa Diamond akiwasindikiza washindi wote wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010 ijulikanayo kama Winners Concert. Ticket zinauzwa shs 15,000 kabla na shs 20,000 mlangoni.

Kwa taarifa zaidi kuhusu ujio wa Sean Kingston tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa namba za simu hapo chini.

Biography
Sean Anderson (amezaliwa tar.
3 Februari, 1990 mjini Miami, Florida, Marekani) anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Sean Kingston, ni rapa na mwimbaji wa raggae wa Kijamaika-Marekani. Japokuwa, Sean alizaliwa Marekani, lakini makuzi yake yote yalikuwa mjini Kingston, Jamaika, aliondoka Marekani akiwa na umri wa miaka sita. Jina hilo analo tumia la "Sean Kingston" amemaanisha kuwa kama anatoa heshima kwa Kingston, Jamaika. Sean vile vIle ana urafiki mkubwa na baadhi ya waimba Reggae maarufu nchini Jamaika (Buju Banton) ambaye pia ndiye aliyemshauri Sean kujiusisha na maswala ya muziki.

Nyimbo maarufu
2007: "Beautiful Girls"
2007: "Me Love"
2007: "Take You There"
2007: "There's Nothin'" (featuring Paula DeAnda)
2007: "Gotta Move Faster"
2008 Fire Burning
2009 Face Drop
AWARDS
Image Awards
2008, Outstanding New Artist (Nominated)
MOBO Awards
2007: Best Reggae Acts
Teen Choice Awards
2007: Choice R&B Track "Beautiful Girls"
2007: Choice Summer Track "Beautiful Girls" (Nominated)
2009: Choice Summer Song "Fire Burning" (Won)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    Ndugu hivi hizi tuzo haziwezi zikafana bila ya hao wasanii wa kimtaifa? mbona mziki wetu upo juu ni sisi kujitangaza au ndio mambo ya kupeana deals kwa style hiyo? waandaaji wanatakiwa kujiamini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...