Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2010

    Sirikali ni kwamba maji yalikuwa yameshafika shingoni kwa mheshimiwa Rais ndo maana aliamua kujitutumua na kusema lolote kuzuia ule mgomo, kwani kama asingesimama na kutoa mkwara mkali mambo wandugu yangekuwa mabaya sana. Mgomo sio mzuri kwa taifa nafikiri mnaona nini kinachoendelea Anthens sasa hivi! ni uharibifu wa hali ya juu. Kwa ujumla hatuba aliyoitoa mheshimiwa Rais ilikuwa ya kibabe na kiimla lakini ilimbidi afanye hivyo kwa kuwa mawaziri aliowachagua mwenyewe inaonekana uwezo wao ni mdogo kutatua matatizo ya taifa ni mawaziri jina tu na wasanii.
    Uchaguzi ujao kama atafanikiwa kurudi madarakani ahakikishe anachagua mawaziri walio na uwezo wa kuongoza wizara stahili. Akifanya hivyo atajikuta hachemshi. Kwa ujumla hatuba yake alichemsha na ni hatari sana kwa kiongozi kuwa kusema kwamba hahitaji kura za wafanyakazi! Hapo busara ilimtoka kidogo akiwa kama kiongozi wa nchi anayetegemea kuchaghuliwa tena kurudi madarakani.
    Watanzania sasa hivi sio wale wa miaka 45 iliyopita, wengi tunaangalia mambo kwa undani sio wajinga wajinga tena.
    Majibu ya TUCTA yana uzito mkubwa sana ndani yake na mheshimiwa rais anatakiwa akutane na hao wajamaa na waongee kwa undani kwani namna ya kukabiliana na tatizo hili.
    Ndimi Mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2010

    Haya sasa nyumba tunajenga sote kwanini tupiganie fito?Haya wadau tupitie mchanganuo wa TUCTA.Nahisi hapa kuna hoja kwa madhamana wetu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2010

    Mdau wa kwanza hapo juu, ukichagua mtu akashindwa kazi si unamtoa/fukuza na sio kumuhamisha wizara. Hii lazima ibadilike au wewe kama kiongozi unabeba lawama zote. Ukweli ndio huo. Michuzi usibanie hii plse.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2010

    Pole mh. Rais kwa majibu haya. Kwa kweli TUCTA wamekuwa wakitoa hoja za msingi wakati kwa upande mwingine mh. amekuwa akionyesha upungufu wa busara. Huwezi sema hauhitaji kura za wafanyakazi, je unamaanisha wewe watakaokupigia kura ni wazururaji tuu au wafanyakazi siyo wanaokuwezesha kufikisha malengo ya nchi? Nimepata moyo lakini pia nimekuwa na masikitiko, ninaogopeshwa nikiangalia upeo wa awamu ya pili ya Mh. kama sasa hivi kabla ya uchaguzi anaonekana hivi. Ni kweli kuna watanzania wengi sana wanaoamini ni bora kuwa watumwa nje kuliko kurudi nyumbani na kukuta mambo yanayoudhi kama haya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2010

    Ingekua nchi zilizoendelea uu ufafanuzi ni tosha kwa rais kuachia ngazi.

    Pili TUCTA wameonyesha rais uwezo wake ni mdogo, mpaka wameamua kumpa somo la namna ya kuongeza mapato ya ndani.Bahati mbaya sana Rais na serikali yake hawana uo uwezo....Haya mambo ya kuongeza mapato ya ndani anayaweza Mkapa.

    Hawe muungwana kuwaomba radhi wafanyakazi kwa kuja na story za "mbayuwayu na Kingong'ota" wakati watu wanadai haki yao za msingi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2010

    Mimi bado ni mwanafunzi, na ninahimizwa kusoma kwa bidii sana. Kwa kweli sifanyi vibaya shuleni. Ila ninakoelekea sasa baada ya kumaliza shule kunanitia shaka. Nadhani itabidi niangalie njia mbadala.

    ReplyDelete
  7. Mdau, GenevaMay 07, 2010

    Mimi naona kama Mhe. Rais anaweza kwenda kwa wazee na kutamka maneno kama hayo yenye vitisho, basi kwenye uchaguzi mkuu ujao, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Na sisi vijana hatutadanganyika!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2010

    SAFIII SANA TUCTA,UNAPOKUWA UNATOA HOJA AU KUJIBU HOJA NI LAZIMA UWE NA VIELELEZO VYA KUTOSHA JUU YA HOJA YAKO,HAPA TUCTA WAMEONYESHA NIA NA NJIA YA VIPI JK ANATAKIWA AFANYE ILI AWEZE KUKIDHI MAHITAJI YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI.PRES NI LAZIMA AWE A BIG THINKING TANK KWA NATION,NI LAZIMA AWEZE KUNG'AMUA VYANZO MBALIMBALI VYA MAPATO NA KUDHIBITI MATUMIZI YA PESA HASA KWA MARUPURUPU YA SAFARI AMBAYO KWA ASLIMIA 90 WANAPATA WALE MAWAZIRI NA WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA NA SIO WATENDAJI MUHIMU WA SHUGHULI ZA KILA SIKU ZA TAASISI. MHESHIMIWA NI LAZIMA AJUE KWAMBA HILI NI TAIFA LA WAVUJA JASHO HIVYO KUONGEZA KIMA CHA CHINI NI LAZIMA...MAANA MAISHA YAMEPANDA SANA...HEBU ANGALIA SHILLING INAVYOPOROMOKA UKILINGANISHA NA US $...LAZIMA AJUE MAISHA YA WAFANYAKAZI WENGI NI YA KUBAHATISHA LABDA MPAKA APATE DILI NDO AANZISHE MRADI WA KUPIGA JEKI BAJETI YA HOME...PIA PRES. AANGALIE MARALI YA WAFANYAKAZI JE ITAPANDA AU ITASHUKA MAANA UNAPOMKATIZA MTU TAMAAA MAANA YAKE NINI?WATU WANAWEZA KWENDA KAZINI KWELI LAKINI UFANISI UKAWA CHINI NA DUNI KABISA WALA USILETE TIJA KWA TAIFA HIVYO MH. AOMBE MSAMAHA KWA WAFANYAKAZI NA KUWAONGEZEA MSHAHARA KAMA ANATAKA UFANISI WA KAZI UENDELEE 100% MHE AACHE MADOIDO YA KUWAITA HAO WAZEE WANAOJIITA WA DSM KWANI WENGI WAO NI KUPIGA FIKSI MITAANI NA SI WALA WATENDAJI WA KAZI WA KILA SIKU.......USIIIIBANE MICHUZI PLIIIIIIIZI

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2010

    HII NI TAARIFA YA SAHIHI NA IMEGUSA MAMBO MUHIMU.

    PIA KUTOA MAONI JINSI YA KUONGEZA PATO LA TAIFA NI JAMBO JEMA SANA.

    VYAZO VYA MAPATO SERIKALINI VIPI VINGI SANA, ACHA NA MISAMAHA YA KODI. KAMA MWEKEZAJI HATAKI KUWEKEZA NCHI AONDOKE.

    MBONA KUNA WATANZANIA WAZALENDO WANAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO AMBAZO NDIYO ZINASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KUENDESHA MAISHA YA WATANZANIA WENGI HAWAJAPEWA HIYO MISAMAHA YA KODI?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2010

    kaka kima cha chini tzs 315,000/=
    wanapigania wapate wakati huohuo Mh Liyumba alikuwa analipwa tzs milioni 10,000,000/= kwa mwezi ebu cheki hilo gap

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2010

    asante mithupu kwa kutuletea copies hizi! Lakini ingekuwa jambo la busara zaidi kutoa copies zote in full na sio segments amabazo weye binafsi unaona ndio points za TUCTA.Let us see the press release in wholesome, so we can form own versions of whats going there kwa sie tulio mbali na huko.
    ASANTE.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2010

    Mdau hapa juu nakubaliana na wewe 100%.
    Huku nilipo tumejazana kibao and ukiuliza kila mtu nyumbani unarudi lini utasikia nikafanyeje....
    Kuna mzungu mmoja nilikutana nae office moja huku, kwenye mazungumzo akaniuliza unatokea wapi nikamwambia Tz...kumbe amewai kufika Tanzania and akazunguka mikoani na akakaa dar kidogo.... akasema,,,, " Thank God everyday, you are very lucky to be here." akasema kwa yeye binafsi ni heli awe maskini wa kuombaomba marekani kuliko kuwa tajiri Tanzania. So ata angekuwa maskini angebaki tu US than kwenda kuwa tajiri TZ...!
    Anyways, God Bless Tanzania na Ubabe wa Viongozi...! Watu wana akili nowadays hawataki kuibiwa ibiwa kama serikali inavyofikiri..
    Stay Blessed you all.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2010

    Uongozi wa TUCTA vis a vis Mkuu wa Nchi/Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

    Natamani ingelikuwa enzi ya Benjamin Mkapa ungeona kama hao TUCTA wana kiherehere cha kujibishana na Jemedari Mkuu. Nakumbuka Tanesco walivyopelekewa FFU kurudishwa ofisini, wazanzibari wlivyopigwa mabomu Unguja na Pemba, watu wote tulishika adabu na wengine wakawa wakimbizi huko Kenya leo hii watu tunaandika barua ndefu na waraka mbali mbali kujibishana na mkuu wa nchi. Ingekuwa enzi ya Nyerere hao wangepelekwa vijijini wakakae huko huko bila kutoka tena majumbani mwao!

    Rais wa nchi akisema ni amri

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2010

    IT IS AN ELECTION YEAR. KAMA HATAMBUI HAKI ZA MSINGI ZA WANACHAMA WENU JUST VOTE HIM(THEM) OUT. ANAWATISHA NA KUWATUKANA NA BADO APATE KURA ZENU!! THESE PEOPLE ALL THEY KNOW IS RULING, NOT LEADING.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2010

    Kwa mujibu wa mawazo yangu nafikiri wakti umefika wa Tz kusima kidetekuhusu haki zao bila kufanya hivyo kila siku itakuwa mambo ya kijinga yanafanyika tuu...Mimi wakati mwingine nashindwa hata kuelewa nia na dhamira ya Rais wetu... amekuwa siyo mtu serious.. hotuba yake ilikuwa chukozo kwa waTz.. na pia unamwona hakiwa anacheka.... sasa umashindwa hata kuelewa, nikama vile mtu yuko kwa mazishi,kuna kifo halafu unakuta mtu mwingine unafuarahi ancheka... lazima ujiulize huyo mtu anamatizo au laa>>
    Kuna mawaziri wawili kuacha hao wengine nafikiri wote wana uprofessor nashindwa hat kuelewa uprefosor wao ni wanini, kwa sababu wamekuwa mzigo na hata mwananch wa kawaida anaweza kuwangamua kwamba hakuna kitu kabisaa.. mmoja ni huyu wa minstry ya labour na huyu wa elimu..
    wabongo tusimame tusiangalie chama tuangalie watu wa kutusaidia inchi hii iendelee mbele
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 07, 2010

    Nakiri sasa tunaona sura kamili ya Mkulu... na ni kiburi cha Redet, lakini aelewe hizo reaserch ndogo hata sample size is not represenattive.,Watz siyo wajinga watampa hiki kipindi cha pili lakini hatambue kuwa ni kwa sababu hakuna alternative(mbadala).. lakini kipimo chake angalie asilimia aliyopta kipindi cha kwanza na hiki cha pili, na hikiwa kwa amepata chini asimilia 10 ya kipindi kilichopita ajue hilo ni pigo kubwa sana kwake... ajue kwamba imani kubwa waTz walikuwa nayo kwake imepungua kwa kiasi kikibwa.. tuangalie awamu ya tatu alipongia kipindi cha kwanza watu walikuwa hawana imani naye walikuwa hawamfahamu lakini kwa sababu ya kujenga uchumu aliweza ku-win trust kutoka kwa WaTz na kipindi cha pili tuliona asilimia ya ushiindi wake uliongezeka.
    haya ni mawazo yangu, najua mkulu ni mtoto wa mjini pia kwenye blog atakuwa anatembelea so apate tuu mtizamo wa wananchi anaowaongoza
    Thanks#

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 07, 2010

    kwa kweli inasikitisha sana! hiyo ndio dhamira hasa ya ubinafsi,maana hatupendani na kutokujali watu wanaishi vipi kwenye janga la umasikin! hebu mh.jaribu kidog kuwaangalia hao jamaa kweli yana msingi!? au tayar Ridhiwan na nduguze in another next level? pia wakwetu wanahitaj pia elimu bora,usitukumbushe ubabe wa bw. ben mkapa. zama hizi zimebadilika people are mature for their what they need hasa kwenye maisha haya ya ubinafsi! kwenye maepa yenu,marich yenu, migodin kwenu...aka! sisi basi hata jasho letu la alfajir kwenye daladala na usiku kugombania daladla wakt tunarudi,tunaomba aman mh. na busara itumike.mdau japan

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 07, 2010

    Wewe Anonymous wa Tarehe Fri May 07, 05:55:00 PM, ni mmoja wa wale wazee mheshimiwa rais alikuwa akiwahutubia.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 07, 2010

    Lakini raisi alisema wewe umetia sahihi kwenye documents za makubaliano...mbona hilo hujalijibu?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 07, 2010

    Kuomba radhi si lazima atangaze ama manataka sasa akatangaze mbele ya wazee kama alivyofanya? nadhani sasa ni wakati wa Rais kupamabana na ushauri potovu na makofi ya kijinga na hata maandamano yasiyo na kichwa kama yaliyofanyika kuunga mkono hotuba yake. Sasa ni wakati wa kwakemea na kuwapa ukweli wale wot wanaojifanya wanamsapoti ama kumshauri kumbe wanampotosha, Rais ni muelewa ana ila kuna watu wanamtakia mabaya kwa kumshauri vibaya ama kumletea mambo ambayo yeyte kutokana na kuwaamini watu wake anajikuta anasababishiwa hali kama hizi, mfano kuna nini mkoa wa Arusha? alafu kusaini muswada wa sheria? yote haya utaona siyo makosa yake bali wale walioandaa mazngira hayo.Any way, kila siku ni shule lamaana kujifunza kuwa accurate na pia precise, vinginevyo ni kushuka kwa credibility!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 07, 2010

    Bwana Mkubwa alipoongea kwenye ile hotuba nilidhani nasikiliza wimbo wa Khadija Kopa.
    Mipasho kwa kwenda mbele. Bado kutiana masingi tu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 07, 2010

    Ndiye mimi niliyesema kuwa ni ukosefu wa adabu, hebu huyo Mgaya akajibishane na Jongwe wa Zimbabwe, M7 wa Uganda, Kagame, au hata Rais wa Burundi ajione ataishia wapi kama sio kufutiliwa mbali na hiyo TUCTA yenu.

    Nampa changamoto akajibizane na Kagame tuone kama mwanaume kweli. Narudia tena Rais akitoa tamko ni amri, mnamchezea huyo JK lakini si kwa Nyerere wala Mkapa waulizeni kina Mapalala na Kasela Bantu, wengine na elimu zao waliozea vijijini.

    Mheshimiwa Rais mpeleke huyo Mgaya kijijini akakae huko halafu uone kama wengine watakuchezea hovyo.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 07, 2010

    True nirudi Tanzania nikafanye nini? Kama mambo yenye ndio haya. Viongozi wasiofanya kazi wanalipwa kuliko wafanyakazi wa chini wanaofanya kazi kwa bidii.

    Na huyo anayesema enzi za huyu na enzu za huyu...hizo ni zilipendwa....hata angekua nyerere au mkapa sasa hivi enzi za utanda wazi afanye hivyo hawajipendi....Mkikalia uoga mtaishia kufa na njaa.....Heri ufe umesimama ukidai haki yako kuliko kufa umelala kwa njaa...

    True ni heri kuwa maskini nchi za wenzetu kuliko kuwa tajiri tanzania...matajiri wenyewe njaa tupu sijui utajiri wao ni wa cash flow au majumba na magari ambayo vyote hata hawavifaidi...wakitoka nje ya nchi kazi kushukia kwa watu kila siku..Mnatubana na vijumba vyetu huku...Tajiri unashindwa kushukia hotelini??????Ukiwaona matajiri wenyewe wa bongo wamechoka kuliko miye mwenyewe mbeba box...

    TUCTA tupo nyuma yenu...tukiona watu wanashikamana hivi na kuongea ukweli penye ukweli ....myaongeza changamoto kwa vijana kutaka kurudi home

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 07, 2010

    kwakweli ni aibu sana rais wa nchi kutunga na kuongea uongo. Aombe msamaha mapema

    ReplyDelete
  25. Mdau ughaibuniMay 07, 2010

    Mimi nilifanya kazi serikalini na sasa niko Ughaibuni. Pesa za kulipa KCC Ths.315,000 zipo. Kwa kuongezea tu point za TUCTA ktk kufanikisha hilo ni kuzibana bajeti za mawizara kwenye mambo ya warsha, semina, safari, kusomeshana nje bila kujali mahitaji, wafanyakazi hewa etc.

    ReplyDelete
  26. Mdau HazinaMay 07, 2010

    Tucta wameongea kweli, Nimeona hili kwa macho yangu ikifika mwisho mwaka wa bajeti yaani June, watu mawizarani hutadhani wamechanganyikiwa wanafuja pesa eti kumalizia vifungu pesa zisirudishwe hazina. Hapo ndio manunuzi hewa, ufisadi wa kupindukia.Wasipozimaliza wanahamishia kwenye akaunti moja inaitwa DEPOSIT hapo ndio wanajichotea taratibu tu, kwa kusingizia chochote tu visafari, fenicha, etc. Pesa ipo ila ubinafsi na ufisadi ndio tatizo.

    ReplyDelete
  27. Candid ScopeMay 07, 2010

    Mgomo kazini humwadhiri zaidi mgomaji na umma na wala si serikali na viongozi wake. Viongozi wataendelea kupozi kwenye majumba ya kifahari wakiburudishwa na viyoyozi wakati mgomaji yuko mitaani na mabango akivuja jasho.

    Tunapofikiria kuhusu mishahara tusifikiri tu kujaza mifukoni mapesa bali tuwe na upembuzi yakinifu katika mambo ya uchumi wa taifa na majukumu yote ya mapato ya serikali kwa matumizi ya watumishi na taifa kwa ujumla. Serikali hiyo hiyo tunahitaji itengeneze barabara, kusaidia wakulima, kusaidia elimu, huduma za afya, nk. Kwa upande wa wafanyakazi utendaji kazini ni duni kwa vile wakishafika kazini ni kusimuliana habari za jana vikaoni kwenye vilabu au bar, michezo ya simba na yanga, kuongelea mambo ya mabibi na mabwana, kutumia muda mwingi kuchati kwenye computer nk. Kisha wanaoaga kwenda lunch inayochukua masaa matatu hadi kupitia bank, na kupita kule kupata moja moto moja baridi baada ya kufaidi kitimoto. Anaporudi sehemu yake ya kazi ndo muda wa kwenda nyumbani umewadia.

    Hata nchi zilizoendelea kiuchumi hawana utaratibu wa kuongea mishahara ya wafanyakazi kila mwaka, ila nimeshuhudia mara moja baada ya miaka zaidi ya kumi. Ninyi ndo mnasababisha hata pesa iwe na thamani ndogo. Hakuna unafuu wa ongezeko la mishahara kwani kila kitu kitapanda hakuna salio litakalobaki.

    Wafanyakazi tafuteni njia nyingine za kujiongezea pato kama kulima mashamba kwani ardhi tunayo. Hata nchi zilizoendelea mshahara wa kazi moja hautoshi na inabidi wafanye kazi mbili, sembuse Tanzania>

    Viongozi wa wafanyakazi wawe na juhudi za maksudi kuwaelimisha wafanya kazi utendaji kazini badala ya kuhangaikia tu kuomba nyongeza za mishahara wakati uzalishaji makazini hauwiani na nyongeza tunayotaka kazini. Nenda we kashike uongozi ndo hapo utaona halihalisi ilivyo kwani kwa sasa unafikiri ndani ya chungu kumejaa chakula kumbe ni ukubwa tu wa chungu ndani umebaki ukoko tu wa ugali tuliopika jana.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 07, 2010

    TUCTA, mmeweza kwa kiwango cha hali ya juu kutuonyesha sisi wafanyakazi na watanzania nini pumba na nini mchele. Mmebainisha wazi wazi pumba alizomwaga hadhara mheshimiwa rais. na hii sasa ni ufunuo wa jinsi gani kiongozi wa nchi wa timu take jinsi wasivyokua makini.
    Na shauri sasa TUCTA mtuorganise sisi wafanyakazi ili tufanye maandamano inchi nzima kupinga hotuba yake iliyojaa dharau, kashfa, matusi(kuwaita viongozi wetu wanafiki,wachochezi).. na kuwaita majina ya kejeli kama ndege kong'ota sijui ndo ndege gani.
    Ni maandamano ndio yatafikisha ujumbe. na kama alivyosema mwenyewe hategemei kura za wafanyakazi katika nchi ya wakulima na wafanyakazi... haya ni maajabu. wafanyakazi tumuonyeshe nguvu ya wafanyakazi.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 07, 2010

    WORLD ECONOMIC FORUM! inahamasisha kuhusu serikali kuthamini na kuutambua na kuuwezesha mchango wa mwananchi mzawa na mwekezaji wa ndani. Ili uweze kuwekeza lazima uweze kuzalisha ziada.Profesa A.Tibaijuka anasema ili kumkomboa mwananchi mzawa lazima serikali iwekeze kwenye makazi mijini na vijijini. Kama wafanyakazi kupitia makato yao ya PSPF,PPF,NSSF wangekua wanajengewa makazi bora, na uhakika wangeweza kusave kiasi kikubwa cha pesa kwa mwezi( sio wa kima cha chini)Hali hii ingeweza kuleta mawazo mapya ya uwekezaji na watu wangeweza kukusanya mitaji na kufanya uwekezaji. hali hii inaweza kuchochea ukuaji wa uzalishaji na kuongeza ushindani kwenye ajira, yaani man power ingekua inahitajika zaidi,hivyo maslahi kuboreshwa zaidi kwani uzalishaji ungeongezeka, mapato ya serilkali yangeongezeka, serikali ingekua na uwezo mkubwa wa kuajiri na kulipa mishahara. Hili suala la kuitana MBAYUWAYU uenda likawa limefutika katika namna hiyo.
    TUCTA tupo pamoja kama kucha na kidole.Siku zote wafanyakazi ni waleta mapinduzi ya kiuchumi na kifikra, hivyo bira wafanyakazi kusingekua na Tanzania huru leo.Na bila wafanyakazi hakuna Tanzania bora yenye neema

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 08, 2010

    Nafikiri huyu mheshimiwa angatuke mwenyewe kabla watu, pamoja na wafanyakazi wa njji hii hawajaamua kumg'atua ifikapo october 2010!

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 08, 2010

    TUCTA waache malumbano ya kijinga na nyie wadau wengine acheni ku-support ujinga...

    Raisi kasema very straight forward, hajatisha mtu... Raisi alichokuwa anafanya ni ku-avoid mgomo ambao utapoteza tu muda. Hata mkigoma serikali haina hela. ni kama mtu ambaye anamawazo badala ya kuyatatua anaenda kulewa, kulewa hakutasaidia coz ukiwa sober mawazo yanabaki palepale.

    Kama mtu hataki kazi aondoke, wangapi wapo mtaani wanatafuta kazi? Uchumi wa dunia ni mbaya hata USA watu sasa wana-struggle kutafuta kazi.

    Kima cha chini USA ni 6.75/hour, Kazi ngumu kama nini but watu bado wanafanya. Dunia ya sasa ni jitiada, Unakazana kujitahidi hili utoke other than kulalamika.

    Kama mwanafunzi"its not your degree that will give u a job but its a combination of both ur natural brain and a degree plus jitihada".

    Watanzania, kwanini msiige mfano wa Lady Jay deee or Asha Baraka? msione wapo pale ni wame-struggle, life is all about struggling. Ukifanya juhudi utapata reward yako.

    Kama hupendi mshahara wa 80000, think of plan B...think namna ya kupanda ngazi kwa kuangaika.
    Huwezi mtu ukatoka tu hlf unatangaza mshahara wa kima cha chini flani wkt hujui huwezo wa mwajiri wako...

    Serikali ya Tanzania kama serikali nyingi duniani naamini haina huwezo, but ikiwa na huwezo itajitahidi na yenyewe kufanya inachoweza.

    Najua maisha magumu, but kama tunataka kitu tusitake kwa shari...tuombe, inabidi kuomba kama hatutapata basiiiiii.

    JAMANI WATU HAWANA KAZI si TANZANIA tu bali all over the world. Shukuru unachopata, Kazana na Mungu atakuongezea.

    ReplyDelete
  32. MTZWADARMay 08, 2010

    Usiibane Michuzi, mjumbe auwawi!

    Ili kuwaongezea kima cha chini wafanyakazi serikali inaweza kufanya yafuatayo:

    -Kila mtanzania alipwaye, hata housegirl, anatikiwa kulipa kodi, biashara zote hata ndogo kuanzia kima fulani, vyakula, magari, maji, umeme, barabara, magari, mkaa, namaanisha kila kitu wazee lazima serikali ipate mshiko wake.
    -Kupunguza matumizi ya serikali ikiwemo safari zisizo za lazima, kuambatana delegation kubwa, cabinet nayo ni kubwa mno ipunguzwe.
    -Serikali bila kusimamia assesment, utozaji na ukusanyaji kodi haitaweza kufika popote pale, maana ndo chanzo chake kikubwa cha kutusnisha mfuko wake wa fedha.
    -Kubuni njia zingine za kujipatia hela, hasa serikali za mitaa, kama vile, parking system, congestion charges kwa kila gari iingiao mjini, internet cafes, libraries, maduka na supermarkets/masoko, maduka ya kuuza vifaa vya nyumbani, mashambani, kilimo, maofisini, elimu na afya, kutoza kodi za majumba yaliojengwa (propery tax).

    Hebu wafanye haya pia na mengine yaliotajwa na wengine, halafu wataona jinsi kutavyokua na mahela serikalini ya kutuhudumia wananchi.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 08, 2010

    "You can fool some people sometimes,but you can't fool all the people all the time".Bob Marley
    Mr.President wakati watanzania wanaonekana wanasonga mbele kimawazo wewe na timu yako mnaonekana kuwa mnarudi nyuma.Maelezo ya hizi documents za TUCTA yana represent upeo wa Watanzania wa karne ya leo. Kama hautotilia maanani, Kalaghabao.Labda kama unafikiria kuwa Dictator kama Mugabe.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 08, 2010

    halafu nina mfano..Dada mkubwa anaduka yeye analipa kodi kama nini na wala haingizi hela nyingi kabisa. dada mwingine anapamba kwenye harusi na hata mikutano ya kiserikali. Na serikali inamuajiri kila siku lakini halipi hata senti kwenye kodi....Hii ni mfano mchache tu inayoonyesha wapi hela zinapotea. mabiashara ya kwenye breafcase hawalipi kodi kabisa...

    Na hawa watu wamesema kweli posho , safari sizizo na mbele wala nyuma, Viongozi waliozeeka wanapelekwa kusoma nje ya nchi sijui ili warudi bongo wakafanye kazi miaka mingapi wakati wanastafuu in less than 5 years wengine wao.....

    TUCTA TUPO NYUMA YENU VIJANA TUMEAMKA NA TUNAONA

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 08, 2010

    MI NADHANI MH.RAIS AKA "MWAJIRI MKUU" WAKATI UMEFIKA SASA AKATUMIA BUSARA ZA KIPWANI KUKAA NA HAWA JAMAA AKAWASIKILIZA HOJA ZAO,ASIWAONE KAMA NI MAADUI WA UONGOZI AMA NISEME UTAWALA WAKE,NO MR PRESIDENT,HAWA WANATAKA KUKUSAIDIA KATIKA AZMA YAKO YA KULETA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA TUKIANZA NA MFANYAKAZI AMBAE HIZO PESA ANAZODAI ATAZITUMIA HAPA TANZANIA NA KUSTIMULATE UCHUMI.

    TX MOSHI R.I.P.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 08, 2010

    Wewe anony wa May,08th 12:19:00 hapo juu naomba usipotoshe watu...kwanza kabisa kima cha chini cha US siyo hicho unachokitaja hapo...Kima cha chini cha huku in terms of federal ni $7:25...still ina depend from state to state.
    Pili,tunajua kwamba economy kwa sasa imekuwa mbaya but siyo chanzo cha Mheshimiwa JK kutoa kauli ambazo haieleweki kwa watu waliowahi kubahatika kwenda shule...Unaongelea kwamba even US watu wana-struggle kutafuta kazi...ni kweli watu wanatafuta kasi but hivi umewahi kusikia kuhusu unemployment benefits...food stamps nk??Basi naomba usifananishe kifo na usingizi...huku hata kama uko kwenye kima cha chini but still ukipata mtoto wanakupa maziwa,diapers etc...sasa hiyo Tanzania tunayo??
    So my point ni kwamba hao watu wanatafuta haki zao...kama hata shule mtoto anatakiwa alipie and all that hivi hiyo nchi tutafika wapi kama tutashindwa hata kuwasomesha watoto...Kweli kazi ipo.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 08, 2010

    NAOMBA NIWAULIZE WAFANYAKAZI SWALI.

    HIVI MNADAI KULIPWA PESA HIYO KWA SABABU MNA MAHITAJI MENGI? AU MNAFANYA KAZI YA KUZALISHA INAYOSTAHILI KULIPWA HIZO PESA? KWA SABABU HATA KAMA PESA ZIPO, MTU HALIPWI KWA SABABU PESA ZIPO TU. NI LAZIMA AFANYE KAZI INAYOLINGANA NA MALIPO HAYO. WAFANYAKAZI WENGI WA SERIKALINI NI WAVIVU, WAKOROFI, WANA LUGHA MBAYA NA WENGI WANAPENDA RUSHWA. NENDA ARDHI, MAHAKAMANI, POLISI, MANISPAA, UHAMIAJI, NENDA UJIONEE.

    ULAYA WATU WANALIPWA VIZURI LAKINI WANAFANYA KAZI SIYO MZAHA.

    KWA HIYO MSIFIKIRI KUWA SERIKALI KAZI YAKE NI KUGAWA PESA BILA TIJA.

    NI MAONI TU.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 08, 2010

    walipwe mshaharahuo kwa kazi gani hasa wanazofanya? Na sisi wachangiaji wengi ni wanafiki wakubwa kutwa tunalalamika humu bloguni kuhusu utendaji mbovu, uzembe na uvivu uliokithiri kwa wafanyakazi TZ.Hebu tuone serikali igome kutoa ruzuku halafu watu kama Tanesco, Dawasco walipwe kutokana na mapato halisi ya shirika kama inawezekana, na watu wote walipe gharama halisi za maji na umeme. Kama hamjaandamana tena.

    MNATAKA KWENDA PEPONI HUKU KUFA HAMTAKI, MTAFIKAJE MBINGUNI?

    FANYENI KAZI KWA BIDII, KILA MTU ALIPE KODI HALISI, ACHENI WIZI NYIE WENYEWE HUKO KWENYE MASHIRIKA NA SERIKALINI, ACHENI KUIBIA SERIKALI PESA NA MUDA, FANYENI KAZI KAMA WATU WA ULAYA NA AMERICA (HUKO NDIKO KUFA), MUONE PEPO ITAKAVYOKUJA.

    Aliyedata

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 08, 2010

    ANONY HAPO JUU YANGU MAY O8 09.50,NAKUJIBU WEWE,HATUDAI NYONGEZA KWA KUWA PESA ZIPO TU LA HASHA BALI NDUGU YETU WEWE AMBAE NADHANI UTAKUWA MFANYABIASHARA SISI NDUGU ZAKO TUNADAI HAKO KA NYONGEZA KWANZA ILI KUMSAIDIA "MWAJIRI MKUU" KUTEKELEZA AHADI YAKE YA KULETA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA PILI GHARAMA ZA MAISHA ZINAPANDA KILA KUKICHA HUKU SERIKALI IKIWA HAITUONYESHI DALILI ZA KUWA NA MIPANGO YA KUSHUSHA GHARAMA ZA MAISHA,MBONA BIG BEN KATIKA UTAWALA WAKE HATUKUMSUMBUA SANA KUHUSU NYONGEZA ZA MISHAHARA?TAFAKARI NA UTAPATA JIBU KWAMBA ALIDHIBITI KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA NA KUFANYA HUO MSHAHARA ANGALAU UTOSHE KIDOGO,TSHS 10,000 YA MKAPA(BLUE) NA YA "MWAJIRI MKUU"(WEKUNDU WA...)IPI ILIWEZA KUNUNUA VITU VINGI?

    EDWARD MORINGE SOKOINE R.I.P.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 08, 2010

    Nyie ndugu zetu mlioko huko majuu msifikirie hayo mliyoyakuta huko yalijileta tu, kuna watu waliyapigania wakapoteza maisha, hakuna asiyejua namna gani mtu mweusi alivyopigania haki huko marekani na kwengineko, historia inaonyesha sikukuu ya mei mosi ilianzia marekani baada ya vurugu kubwa za wafanyakazi waliokuwa wakinyonywa miaka hiyoo ya 1800 sa sa leo nyie mnaona mambo yako safi mnawashangaa wafanyakazi wa TZ wanaodai haki zao za msingi SIWAELEWI.
    Sidhani kama saa hizi mngekuwepo huko kama watetezi wa haki za mtu mweusi wangekuwa kama mlivyo nyie.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 08, 2010

    huyu aliyesema ni rushwa tupu namuunga mkono kama hujawahi kwenda wizara ya aridhi tema mate chini pale sio pana rushwa bali balaaa rushwa utakyotajiwa utoe utatamani aridhi ipasuke upotee kwenye uso wa hii dunia maana kama umeenda kununua chakula hutaki kafe njaa.wapunguze rushwa sio binadam kabisa kwa helaaa.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 08, 2010

    HAKI ITAPATIKANA TUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 08, 2010

    Anony wa sat May 08, 09:39:00 AM.
    YEs!according to federal in USA kima cha chini ni 07:25/hour.

    But nakuomba mdau zunguka other states, Wafanyakazi wa Mcdolnads or Burger King ktk other states wanalipwa btn 6dollars to 7dollars.

    Pia abt food stamps, huwezi kulinganisha uwezo wa serikali ya Tanzania na USA...USA ni muungano wa STates or Nchi....State moja ndogo ya USA, tena not state but a city ina GDP sawa na Tanzania...ebu imagine???

    Tunajua maisha magumu, tunahitaji tuongezewe mishahara but kwa sasa serikali haina...ikaibe??? tusiwe kama watoto, tuwe tuna-akili. Kikwete kasema hela serikali haina hata mfanye nini, mbona inakuwa ngumu kuelewa??? tunapoteza tu muda kuongelea kitu hiko hiko badala kutafuta solution na mambo mengine.

    Mnavyoongea nyie solution mbadala ambazo zitasaidia serikali kupata mapato zaidi, unakuta yameishapitiwa na serikali...Msione serikali wajinga.

    Tushukuru Mungu tumepata Raisi mpole na msikivu. Raisi ambaye anapenda maoni ya watu na wala hajali mtu akiongea anachotaka kuongea. Kaweka freedom of speech kama USA, but itabidi tutumie hii freedom in a right way other than kumfanya Raisi aonekane kama hajui anachofanya.

    Inabidi tuwe kama WACHINA au WAHINDi, tuwe na umoja.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 08, 2010

    RAIS AMESEMA ATATUMIA ASKARI MABOMU NA VIRUNGU KUWASAMBARATISHA WAFANYAKAZI SASA MIMI SWALI LANGU NI LIFUATALO,HAO ASKARI AMBAO WATATUMIWA NA RAIS KUPIGA VIRUNGU NA MABOMU WAFANYAKAZI WENZAO SI WAFANYAKAZI PIA?NA WANAHITAJI ONGEZEKO HILO LA KIMA CHA CHINI?WANAHITAJI PUNGUZO LA KODI KWENYE MISHAHARA YAO PIA?SASA ITAWEZEKANAJE WAWAPIGE VIRUNGU WAFANYAKAZI WENZAO (WALALAHOI) RAIS ALIKUWA NA UHAKIKA GANI KUWA WANGEMSUPPORT MANAKE NA WAO PIA WANGEWEZA KUUNGANA NA HUO MGOMO MANAKE NA WAO NI WAFANYAKAZI PIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...