Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa akijiandisha katika daftari la wanachama wa chama hicho watakaopiga kura za maoni kwa ajili ya wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani katika kata ya Msasani, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa tawi hilo, Dk.Suleiman Mohamed na Katibu wa tawi hilo, Edward Mbwambo. Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa akifafanua jambo leo mara baada ya kujiandisha katika daftari la wanachama wa chama hicho watakaopiga kura za maoni kwa ajili ya wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani katika kata ya Msasani, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2010

    Ticha kumbe na wewe kibosile mtaani kwangu!!

    Che

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2010

    Hahaha ama kweli CCM ni chama Dume, Kinakusanya mpaka Kina Mudi na Mbwambo, IFM cronies LOL!. Ngoja na mimi nianze kulipia kadi yangu, huwezi jua siku zali linaweza kukuangukia pwaa umeukwaa ukatibu wa Wizara. Au U-Director somewhere!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2010

    Wapendwa wana CCM, nafurahi kuona mnajitahidi kutekeleza taratibu zenu kama katiba yenu inavyohitaji. Ila naomba nitoe maoni juu ya muonekano/sura ya hiyo ofisi ya sijui tawi au vyovyote ilivyo, hailingani na sifa ya CCM, na wadau, au wanachama katika hilo tawi/shina! Naona aibu kumuona Mhe. Makamu Mwenyekiti wa CCM-Taifa, na wapambe walioko nae, wameketi na nyuso za furaha wakitekeleza hatua muhimu ya chama, ndani ya ofisi ambayo hata ukuta wake hauna rangi, ua hadhi inayofanana na chama, au wadau katika tawi/shina hilo! nawaomba mfanye juhudi za makusudi kutengeneza hiyo ofisi ilingane na sifa yenu! Hata kama mnaingia ofisi hiyo kila baada ya miaka "mitano" namaanisha chaguzi zinapokaribia!! Mniwie radhi iwapo nitawakera kwa maoni yangu!
    Mungu awabariki katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu!

    ESK!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2010

    spot on anonymous 07.54 pm.....

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2010

    Kwanini wasiwe wanaenda kujiandikisha na kupiga kura majimboni/vijijini/mijini kwao

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2010

    tunaomba mtuachie na sisi vijana jamani lakini daaah wazeee tumechokaaa

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2010

    kibabu kati Wa busara...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    NIA YA DAFTARI HILI NI KUWADHIBITI WAFANYABIASHARA WASIOCHANGIA CCM KWANI HAWATAKUWEMO KWENYE HILO DAFTARI, PIA WAKAZI MITAANI WATAJULIKANA NANI WAPINZANI NA HIVYO KUNYIMWA HAKI ZAO, KURA NI SIRI NA HIVYO SI SAHIHI KUJUA NANI ATAKAYEKUPIGIA KURA. CCM ITATUMIA DAFTARI HILI KUHESABIA KURA! HAKUNA SABABU YA KUWA NA UCHAGUZI, TUJIULIZE NA HUKO PEMBA CUF IKIANDIKISHA WATAKAOKIPIGIA KURA NA IKATUMIA KAMA USHAHIDI KWENYE UCHAGUZI DHIDI YA CCM ITAKUWAJE? HUU MTINDO WANANCHI TUUKATAE KWANI UNAWEZA KULETA VURUGU KWENYE MAJIMBO MBALI MBALI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...