JK na Rais Guebuza wa Msumbiji wakisalimia wanachi katika daraja la Umoja linalounganisha TAnzania na Msumbiji kijiji cha Mtambaswala mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa daraja hilo mapema leo JK na Rais Guebuza wa Msumbiji wakiwa na marais wasataafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mh. Benjamin William Mkapa kwenye sherehe hizo za uzinduzi wa Daraja la Umoja

Wananchi wakishangilia uzinduzi wa daraja la Umoja.
Picha na Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2010

    kama mdau alivyosemahapochini,hilo daraja liitwe daraja la mwinyi,maana alojenga mzee ruksa liliitwa daraja la mkapa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    Hili daraja tayari lina jina "Daraja la Umoja". Kwanini libadilishwe jina? Hakuna ubaya kwa lilealojenga mwinyi kuitwa mkapa hakuwa na jina, Mwinyi hakutumia pesa zake alitumia pesa za TZ na alikuwa anawakilisha wa TZ.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    UNAONGEA PUMBA WE HUELEWI MAANA YA DARAJA LA UMOJA

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2010

    wakaibe sasa vyuma na ziki zao

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2010

    Wahandisi (Engineers) waliojishughulisha na ujenzi wa hilo daraja wanapaswa kupongezwa for a job well done.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2010

    Wahandisi hawatakiwi kupongwezwa wala nini. hiyo ni sehemu ya maadili na shughuli zao za kila siku. Its not miracle.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2010

    Anon, May 13, 02: 02, wacha hizo. Je kama hao waandisi wangelijenga chini ya kiwango? Maghorofa mangapi yanaporomoka? Madaraja mangapi yanakorofisha na kusababisha mushkheri katika ratiba za usafiri. Na wewe hongera basi, kwa kile ukifanyacho, kama wakifanya sawa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2010

    Hili ni daraja linalomilikiwa na nchi mbili litaitwaje Mwinyi! Au liwe na majina mawili ukiwa Msumbiji jina lingine na Tz jina tofauti. Msiwe na wivu wa mstuni, jina ni jina tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2010

    Kuzinduwa tunazindiwa lakini mbona sisi hatuanzishi cha kwetu? Uwanja wa Taifa sawa tumezindua, daraja la umoja sawa tumezinduwa, lakini sisi tumefanya nini sasa au tumeanzisha nini kizuri ambacho kama tusipokimaliza kufanya sisi tuliopo watamalizia na kuzindua watakao kuwepo wakati huo?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2010

    Hivi wadau, barabara ya Mandela ina mkono wa mtu au ina nini? Barabara hii imeanza kujengwa tangu mwaka 2005 kama sikosei, lakini cha kushangaza hadi sasa, kipande cha kuanzia ubungo hadi buguruni hakijamalizika, hivi ni kwa nini Jamani? Barabara muhimu na nyeti kama ile inachukua miaka saba kujengwa bila kumalizika hivi hawa viongozi wetu wanafikiria nini? Waziri wa Miundo mbinu yuko wapi? Leo kulikuwa na foleni sana pale watumishi wamefika maofisini saa nne asubuhi achilia mbali wafanyabiashara waliochelewa na wasafiri waliochelewa ndege au mabasi. Au ndo kusema wanasubiri wafungue wakati wa kampaign za uchaguzi? Ni aibu jamani kwa serikali iliyoko madarakani.Ebu amkeni jamani, mnatusababishia usumbufu mkubwa sana sisi tuliowachagua. Daraja la umoja sawa, barabara ya Mandela mtazinduwa lini?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2010

    yaani nimekuwa nikifuatilia sana maoni ya wadau mara kwa mara , lakini hata siku moja sijaona wadau wakisifia kitu au jambo zuri ambalo limefanyika tz , wao saa na siku zote wanakandia , jamani angalieni vitu vya kukandia na vingine vya kusifia , mnakuwa kama mizigo ya mavi hambebeki !!! tena wadau wa tz wanaoishi nje ya tz ndo wanaongoza kwa kuidharau tz , kila kitu kikifanya tz kwao tabu, sasa mnatakaje ? tz iwe kama usa au uk ? unafananisha mnazi na mdizi ? mnanichosha ,huko ulaya mko kama watumwa wazungu wanawanyanyasa kama nini , hawana amri tu ya kuwafukuza ila wangelifanya , sifia kwenu , HOME SWEET HOME , kama kuchafu kwenu kama kubaya kwenu , njoo upasafishe njo upatengeneze , unakaa huko na kupatengeneza huko then unakashifu kwenu..
    acheni hizo

    MDAU
    TZ

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2010

    mzee prezzde, anaonekana smati kama OBAMA, Hata vidole anavyo nyoosha ni sawa kabisa au wadau mnasemaje eee jamani, mnaonaje kama angeiga mambo ya uchumi, msimamo, maana mwanzo alikuwa anaiga Bill clinton, hata bush rafiki yake sana kweli anaenda na wakati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...