Marehemu Prof. David Kapinga
(23/07/1943 – 13/03/2010)

Familia ya Marehemu Prof. David Kapinga, Inatoa shukrani za dhati kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wote kwa kushirikiana nasi katika kipindi kigumu cha msiba uliotokea ghafla Morogoro wa Mpendwa Baba yetu, Prof. David S. Kapinga.

Shukrani za pekee ziwaendee, Mwenyekiti wa CCM Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM Lut. (Mst) Yusuph Makamba, Mkuu wa Chuo na Uongozi mzima wa Chuo cha Mipango Dodoma, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, UDSM, Takukuru Makao Makuu, Viongozi mbalimbali wa Serikali, Waumini na Uongozi mzima wa kanisa la Mt.Patrick Morogoro, Wanakwaya na Wanajumuiya wa Bikira Maria mama wa shauri jema.

Kwa kuwa sio rahisi kumshukuru kila mmoja peke yake, tunaomba mzipokee shukrani zetu kwa namna ya pekee na Mungu awabariki sana!

Baba yetu tulimpenda lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe, Amina.

Lilian Kapinga,
Kwa niaba ya familia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. RIP,Prof.Kapinga,very sorry for Kapinga's family for this sudden and mourning occassion,he taught me DS at SUA,real that mzee was very good and considerate,hajawahi kumkamata mtu kwenye somo, unless real uko very lazy.He was not only a lecturer but our father due to his habit of being considerate in his exams,as opposed to other lectures who used to discontinue students purposely or makusudi,anyway this is an irreplaceable loss for our father.
    Very sorry Kapinga's family.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2010

    RIP prof. you will always be remembered!

    ReplyDelete
  3. H. kangoma kapinga UKMay 07, 2010

    poleni sana ndugu zangu niko mbali nilishindwa kuhudhuria lakini ni pengo kubwa sana kwa wamatengo..yeyote niliyekutana naye popote nje ya nchi yetu ukitamka jina la kapinga kwenye circle za wasomi hawakosi kumtaja huyo marehemu mzee wetu...alifanya yaliyopaswa popote alipobahatika kufundisha...na mwenyezi mungu amlaze pema peponi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2010

    R.I.P PROF. KAPINGA

    Nawapa salaamu za pole kwa ndugu,marafiki na familia yote kwa msiba wa Prof Kapinga.
    Mzee Kapinga ni mmojawapo kati ya wengi waliokuwa mstari wa mbele katika kujenga maendeleo ya Taifa.

    Ushauri wake kwangu katika juhudi za uongozi bora kazini nilipokuwa kijana mdogo saana kama kiongozi msaidizi katika bwalo la maofisa wa polisi-Oysterbay miaka ya 70`s ulinisaidia saana kumudu nafasi ambayo kwa wakati ule ilikuwa juu ya kiwango changu.
    Mungu amlaze mahali pema peponi.
    Mickey Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2010

    Yaani unakwenda Chuo unasoma DS halafu unategemea kukamatwa? Sasa CORE subjects inakuwaje?

    ReplyDelete
  6. RIP Professor. Heshima yako ni kubwa sana na naamini hii itaendelea kujidhihirisha kwa vizazi vingi vijavyo.

    kwa wanafunzi wako wote hukuwa mwalimu tu, bali baba zaidi. ulichukua muda wako kuhakikisha kuwa hakuna mtu amejisikia kuonewa na mara zote umesimama na mwenye kujisikia kupungukiwa. ulikuwa mshauri wa wote si tu darasani lakini pia hata nje ya darasa. mara nyingi tulikufuata kuomba ushauri binafsi na hukuisita kuutoa bila kujalisha muda wako ambao ulikuwa unahitajika na wengi.

    binafsi umenifundisha busara, uvumilivu, upendo, hekima, na kuamini kila mtu ana mchango wake duniani bora tu apewe fursa.mara zote hata walipokuwapo wagombanao ulisisitiza upendo na amani. na hii ni tunu kubwa tuliyojifunza kutoka kwako. kuridhika na mara zote kumshukuru Mungu ni tabia njema ambayo inakinzana na ufisadi na ulafi ambao ni mateso kwa wengi waishio duniani mara zote ilikwa kinyume na mzee wetu.

    japo wengi wanaweza kutosema, lakini prof amekuwa ni daraja kubwa la mafanikio yao. binafsi alinipa shime kusoma digrii ya uzamili nikilipa ada kidogo kidogo na ni kweli niliweza.

    kwa familia ya Prof. tunawaombea Mungu awape uvumilivu. mtenda mema siku zote atakumbukwa kwa wema wake. naommba muamini tuko wengi ambao ni ndugu zenu tumeunganishwa na upendo wa mzee wetu. mtazidi kulitambua hilo kwani mtakutana nasi wengi ambao hatujaweza kumlipa marehemu hadi leo hii!

    Dr Mark

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2010

    Familia ya Marehemu Prof. Kapinga (Mke wa marehemu mama Kapinga, watoto wa marehemu Dada Terma, Lily & Bite, wajukuu wa marehemu, wakwe, ndugu wote, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu napenda kutumia fursa hii kutoa pole sana kwa msiba huu mzito uliotugusa kwa namna moja ama nyingine, Mungu awape nguvu na faraja hasa ktk kipindi hichi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu marehemu Prof. Kapinga, Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Mungu ilaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen. GLORY MLAY

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2010

    RIP Prof Kapinga! Nakumbuka ulivyokuwa good in your lectures at SUA,vichekesho vyako wakati wa Lectures miaka ile no one wanted to miss your class (you are, and always be one of a kind). Mungu aibariki familia ya Kapinga tunaimani siku moja tutaonana mbinguni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...