Kikosi cha Simba SC

Nyota ya ngekwewa ya timu ya Simba imezidi kung'ara mwaka huu baada ya mshambuliaji wake hatari, Mussa Hassan Mgosi, kuwatoa kidedea wana wa Msimbazi kwa kufunga goli kwa njia ya penati katika dakika ya 90 ya mchezo uliochezwa nchini Rwanda katika michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na kati baada ya timu hiyoya Simba kuibanjua timu ya Atraco goli 2-1 mchezo uliomalizika jioni hii.

Goli la kwanza la Simba lilifungwa na mshabuliaji mpya wa timu hiyo mganda Robert Ssentongo aliyesajiriwa kutoka timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam,

Timu ya Atraco ilijipatia goli la kufutia machozi dakika ya 76 ya mchezo huo hivyo mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa Simba ya Tanzania 2 na Atraco ya Burundi 1 hivyo Simba imejitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika kundi lao kwenye michuano hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2010

    Marakhabaa!!

    ReplyDelete
  2. YANGA BOMBAMay 18, 2010

    ANGALAU WAMETOA ULE MKOSI WA WA KIPIGO CHA AIBU KULE MISRI JAPO NASIKIA WAMESHINDA KWA KUTUMIA MAMLUKI MCHEZAJI WA AFRICAN LYON YA TMK ROBERT SENTONGO,OTHERWISE ILIKUA MAJI YAZIDI UNGA TENA

    ReplyDelete
  3. Nonda Shabani "papii"May 18, 2010

    Hee....simba imeshinda?simba ipi kwanza...?hii iliyopigwa tano last week au?kama ndio lazima watakua waliazima wachezaji wa timu nyingine,hata hivyo hongereni kwa kumpa zawadi ya kwanza mwenyekiti wenu mpya bwana Ismail Aden Rage "mtu wa mpira" na uongozi wake

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2010

    Hongera mnyama, lakini kwa nini umetumia picha hii ya zamani sana? wachezaji ambao bado wapo na simba ktk picha hii ni wawili tu Kaseja na Mgosi. Zipo picha nyingi za karibuni mojawapo ikiwa ile ya bao nne walizopigwa yanga ambazo hadi leo bado wanatafuta mchawi!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2010

    Hawa jamaa siku hizi hawaitwi tena 'Mnyama', bali tangu watoke Misri ambako walipigwa 'Khamsa' sasa hivi wanaitwa 'Khalua Khalua'!!! Wameshinda lakini hawajawahi kuleta kombe nje ya ardhi ya Tanzania kwahiyo tunajua mwisho wao ni kurudi bila kikombe....mambo hayo wanaweza wenyewe...mnawajua.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2010

    wewe unaesema simba imeazima wachezaji inaonekana utakuwa shabiki wa yanga.LAkini simba hiyo hiyo unayoibeza ndo imefunga mara mbili tena mabao manne.Bado huamini uwezo wao tu.Kweli walifungwa Misiri ila si ulioona game ilochezwa?Jifikirie kwa game ile Hodood ndo ingekuwa yanga wangefungwa mangapi?Kumi kidogo.Simba oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

    Masoud Masoud
    Dodoma

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2010

    YaleYale alosema Hasheem Thabeet, hatuwajui kwa majina wachezaji wa timu kubwa za Tanzania, tutundikieni majina ya hao 'first eleven' wa Simba ktk hii picha.

    Na itakuwa vizuri tukiendeleza utamaduni wa kutaja majina ya wachezaji wa timu ktk picha.

    blogu ya jamii tuanze utamaduni huo.

    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2010

    Yanga msiseme lolote kuhusu Simba kufungwa huko Misri mpaka nanyi mpate ushindi hata wa 1-0 tu nyumbani dhidi ya timu za Misri.
    Timu iliyochukua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mara nyingi kuliko zote mnaifahamu?
    Timu iliyochukua kombe hilo 'lote lote' mnaifahamu?
    Give credit where it's due. Heko Msimbazi, endeleeni kuliwakilisha taifa letu na kuliletea heshima.

    ReplyDelete
  9. NicholasMay 18, 2010

    Hii picha ni ya zamani ,Ankal wekeni picha ya kikosi cha sasa cha timu ya Simba SC.

    Wachezaji waliopo sasa katika picha hii ni Kaseja na Mgosi tu.Tujaribu kwenda na wakati.Nurdin Bakari msimu yuko Yanga kwa miaka miwili sasa.

    Tujaribu kwenda na wakati.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 19, 2010

    Mdau yuko sahihi kabisa kuwa janaja ya Simba ikiwa Tanzania tuu haina ubavu wa kuchukua hicho kikombe nje ya Tanzania. Ni Yanga tuu ndio imeweza hiyo kazi.
    Uchawi hauvuki mipaka

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2010

    WATU WENGINE WANAFURAHISHA SANA JINSI WALIVYO VIHIYO ETI SIMBA IMEFUNGWA 5 INGEKUWA YANGA INGEKUWA ZAIDI!, YAANI MAWAZO DUNI ANAFANANISHA MPIRA NI HESABU ZA MLINGANNYO????
    MPIRA HAUENDI HIVYO HATA SIKU MOJA, NA UNAYEMFUNGA LEO KESHO ANAKUFUNGA YEYE. WEE KUBALI TUU KUWA SIMBA IMEFUNGWA KAMA KUFUNGWA BASI YANGA INA AFADHALI ILIFUNGWA TATU MWAKA JANA NA AL-AHLY AMBAYO NI KALI ZAIDI.

    ACHA U-KIHIYO.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2010

    Haya tena PakaWaSofa amng'ata Simba bila Majibu, Sofapaka 1 Simba0, matokeo ya Kombe la Kagame 19/05/2010.

    Mdau
    Jangwani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...