mshambuliaji wa timu ya Singida,Kelvin Charles (10) akijaribu kumtoka beki wa timu ya Arusha,Yusuf Elias (15) katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliopigwa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imeshida 3 - 2 dhidi ya Arusha
Mshambuliaji wa timu ya Singida,Kelvin Charles (10) akiipatoa timu yake bao zuri sana na kufanya matokeo yawe ni 2-2 dhidi ya timu ya Arusha.hadi mwisho wa mchezo Singida iliweza kutoka kidedea baada ya kupata ushindi wa mabao 3 - 2 na kuifanya timu hiyo ya Singida kutinga fainali ambapo mshindi wa kesho kati ya Lindi na Ilala ndio atakaecheza nae.mechi hii imepigwa leo katika uwanja wa Uhuru jiji Dar.
...ngoma imekataa,sijui inekuwa vipi kama ingekubali...
mshambuliaji wa timu ya Arusha,Bakari Kigodeko (10) akichomoka na mpira kuelekea langoni mwa timu ya Singida huku beki wa timu hiyo,Joachim Kimolo akimkimbiza kutaka kuodoa hatari hiyo langoni mwake katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imesonga mbele kwa hatua ya fainali mara baada ya kushinda goli 3 - 2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2010

    Aisee Singida iko juu kwa sasa. The most improved team this year!! SINGIDA OYEEEEE!

    ReplyDelete
  2. Tanzania tuwe wazalendo tusiwekama kuu au wanyama pori. Hii biashara ya kushabikia timu za Manchester au Ulaya na kuwa wanachama kwa bei kubwa inatudumaza kimichezo katika ngazi za michezo na kiuchumi. Tumekuwa na silika kuwa wazungu ndio watu wa maana zaidi yetu, sio uungwana huo. Kwenye familia yangu kuna wazungu na nimekua na wazungu, wao masiki zaidi ya wabantu. Sasa michangi hiyo inayotolwa na wabongo huko Ulaya ingejenga timu kibao kabambe hao home, na TZ tungeweza kushindana katika ngazi za kimataifa kama SA vile. Tuzidi kuwa wazalendo na waungwana. Piamambo ya ushuru mkubwa kwa vitu ambavyo Tanzania hatuproduce haisaiidiii kwani hatulindi masoka ya ndani na tunakwamza maendeleo. Naona kizazi cha siasa za Ujamaa na kujitegemea kikipita labda tutapata viongozi bora wenye incentives za maendeleo na sio siasa za ujamma.maanake ujaama umekwisha duniani na sio mfumo mzuri wa kiuchumi, na bila uchumi bora, hakua maiha au afya bora.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2010

    Hello hivi hizi namba kwenye mabano ni umri wa wachezaji au ni nini..?? Kama ni umri mbona ni wadogo sana..??!!. Hawa bwana wadogo wa Singinda inaonekana wamepania kuchukua kote, wanacheza kwa kuijtuma sana, kwa nguvu zote muda wote pamoja na ku-miss "tick tucker" ya kufa mtu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    Hongera Singida.Na hongera Mohamed Dewji Mbunge wa Singida mjini kusaidia maendeleo hapo. Ingawaje hii timu itaitambulisha Singida kwenye Dunia ya Tanzania. Go Singida!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...