Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, anondoka Nchini LEO tarehe 9 Mei, 2010 kwenda nchini Uturiki kwa ziara ya mwaliko wa Spika wa Bunge la nchi hiyo, Mhe. Mehmet Ali Sahim. Katika Ziara hii, Mhe. Spika ataambatana na wabunge saba wanaounda chama cha ushirikiano baina ya Bunge la Uturuki na Bunge letu ambao ni:

1. Mhe. Wilson Masilingi (Mb)
2. Mhe. Lazaro Nyarandu (Mb)
3. Mhe. John Komba (Mb)
4. Mhe. Zuberi Maulid (Mb)
5. Mhe. Suzan Lyimo (Mb)
6. Mhe. Felista Bura (Mb)
7. Mhe. James Musalika (Mb)

Ziara hii ya Mhe. Spika Nchini Uturuki, inafuatia mwaliko wa Spika wa Nchi hiyo aliyoitoa Mwishoni mwa Mwezi March, 2010 na kuwasilishwa na Balozi wa Uturuki nchini Dkt. Sander Qubuz kwa Spika wa Bunge ikiwa ni jitihada za nchi hiyo kutoa fursa ya kipekee kwa viongozi wa kitanzania kutembelea nchi hiyo ili kuweka hamasa ya kukuza ushirikiano wetu kati ya Uturuki na Tanzania.
Katika ziara hii Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Spika utajionea shughuli mbalimbali za maendeleo na kiuchumi ikiwa ni jitihada za kuwahamasisha waturuki kuja kuwekeza chini katika sekta mbalimbali za maendeleo hususani katika sekta za viwanda vya nguo na utalii . Mwaliko huu wa ziara ya Mhe. Spika nchini uturuki utakuwa ni wapili kufanywa na viongozi wa Tanzania katika nchi hiyo ambapo awali Mapema Mwaka huu, Mhe. Rais wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea nchiyo kwa Mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo. Ujumbe huu wa Tanzania unategemea kurejea nchini mwishoni mwa wiki hii.
Imetolewa na
Owen Mwandumbya
Afisa Habari wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2010

    Jamani naomba kuuliza, mheshimiwa John Komba atalipa nauli ya watu wangapi? Manake ni dhahiri kwamba seat moja haiwezi kumtosha na itabidi atumie viti viwili katika ndege.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    "MUHESHIMIWA" kwanini mnapenda kuabudiwa??ili neno halifai kabisa tumieni ndugu tu..aggggggrrrr

    mataifa mengine makubwa uko wala hawajiiti ili jina.iyo list vyama vingine wapo?

    ovyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...