Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akipokewa na Mwenyeji wake, Spika wa Bunge la Uturuki Mhe. Mehmet Ali Sahin mara baada ya Kuwasili katika Vıwanja vya Bunge la Uturuki Mjini Ankara Uturuki jana. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wa nchi hiyo.
Ujumbe wa wabunge toka Tanzania ukiongozwa na Spika wa Bunge wa Tanzania Mhe. Samuel Sitta, ukiwa katika mkutano wa pamoja na wenzao wa Bunge la Uturuki pamoja na Spika wa Bunge la Uturuki Mhe. Mhe. Mehmet Ali Sahin kujadili namna ya kuimarisha mahusiano ya mihimili hii Miwili pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika sekta mbalimbali za Maendeleo. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wa chi hiyo.

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akiwa katika mazungumzo na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Uturuki Mhe. Mehmet Ali Sahin (kulia) mara baada ya Kuwasili katika Bunge la Uturuki Mjini Ankara. Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Bunge cha Urafıkı baina ya Bunge la Uturuki na Tanzania Mhe. Lazaro Nyarandu
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan mara baada ya kumtembelea Ofisi kwake. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wanchi hiyo.
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akiwa katika maongezi na Waziri Mkuu wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan mara baada ya kumtembelea Ofisi kwake. Ziara ya Mhe Spika nchini Uturuki inafuatia Mwaliko wa Spika wanchi hiyo alio utoa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la Uturuki na Tanzania pamoja na Kuhamasisha wawekezaji katika sekta mbalimbali. Picha zote na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2010

    Napata utata hivi hili jina linatamkwa Sam-yu-eli au kama tulivyozoea Samweli?Naomba msaada tuta!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    Komba wapi Komba??? Kajilipua au anacheki microphone madukani???

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    Mdau uliyeuliza Komba wapi,kwani hujamwona amesimama hivyo viti havimtoshi kwa size yake.
    Wangesema mapema wangemchongea kingine kwa special order

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2010

    Mshkaji anon. Wed May 12, 09:06:00 PM, simuoni Komba hata kwa waliosimama...nadhani ameenda kununua zile vitu XXXXXXXXXXXL, kushonesha kunaumbua mwana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...