Uongozi wa muda wa jumuiya ya watanzania London umekamilisha kazi mliyotupa ya kutengeneza mfumo mpya wa kiuendeshaji pamoja na kuitisha uchaguzi wa viongozi. Sasa tuko tayari kuwakilisha taarifa hii kwenu wanajumuiya. Shughuli hii itafanyika Ijumaa tar 14-May 10 kuanzia saa 11 jioni.
Uchaguzi wa viongozi wa kudumU utafanyika tar 5-June 10 na ili kufanikisha hayo kikao hiki ni muhimu sana hivyo tunaomba ushirikiano wenu, mhudhurie na kutupa mawazo pale inapohitajika.
Agenda:
--MFUMO: mfumo mpya wa kiutendaji
--KATIBA: kuichambua katiba yetu
--UCHAGUZI: kupata wagombea na upigaji kura.
--KUSIMIKWA: maandalizi ya kusimika viongozi wapya
--BALOZI: kuhusu wanajumuiya kumuaga balozi na kuwasimika viongozi
--ADA: ada za uanachama, kiasi cha kulipa na jinsi ya kulipa
--Mengineyo
Fika mapema, sote tutakuwa pale tayari kayapitia hayo yote.
-Kikao: kikao cha wanajumuiya
-Waalikwa: watanzania London
-Mahali: TANZANIA HIGH COMMISSION,
3 Stratford Place,
W1C 1AS,
London.
Muda: Tar 14 May 10, Saa 11 jioni

N.B: Iweke tarehe 5 June kwenye ratiba yako,
inaandaliwa party safi.

G Mboya -
TA Director of Communication

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2010

    Yaani unadhani ukitutajia kuwa kuna Party nzuri sana ndio tutakuja!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    wabongo tunapenda kujipa vyeo ovyo ovyo, hata hapo napo kuna director,duh yangu macho mie,

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2010

    Balozi ana kismati cha kuagwa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2010

    Maadam msema kutakuwa na party, basi ni lazma nitakuja, tuombe uzima. Maana najua vitu vya nyumbani kama Mapakacha, na vinyago ambavyo ndio zawadi zetu za kawaida wabongo, havitakosekana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...