Habari za Kazi Ankal Michuzi,
Nilikuwa naomba nitoe hii habari kwenye blog yako inayofikiwa na watu wengi. Mimi ni Mchungaji huku Mbezi . Tulikuwa na mlinzi Mmasai tuliyemwamini sana na alikuwa analinda kanisani.

Wiki iliyopita kafungua kanisa tukakuta Mmasai hayupo na kuna kutoweka na amplifaya ya keyboard combo. Tulipoanza kufuatilia tukagundua alikuwa anafanya kazi sehemu mbali mbali ambako kote ameshawaibia na kutoweka. Tulipowafuata wamasai wenzake wote wakawa wanaficha habari za mwenzao. Tukaambiwa na watu wanaowafahamu vizuri kuwa sasa hivi wamasai wameunda magenge ya wizi huku wakilindana na kufichana.

Nilikuwa naomba kutoa taarifa kwa jamii kuwa
wachukue tahadhari kutumia walinzi wa kimasai.

Mchungaji Mbezi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2010

    NAOMBA MUHESHIMIWA RUASA ATUSAIDIE KUTATUA TATIZO HILI HARAKA SANA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2010

    Mchungaji vipi tena mbona lugha ya kibaguzi namna hiyo, unaweza kuwasilisha ujumbe wako na tahadhari kwa jamii kwa namna inayokubalika na Watanzania.

    Kuna walinzi wengi tu( hapa sitaji kabila) ambao wameshafanya uhalifu kama huo na hata mauaji.

    Suala ni kuwa makini kuelewa dunia hii sasa imebadilika, hivyo waajiri kuchukua hatua za tahadhari kama kupata 'historia' ya mlinzi mtarajiwa toka Polisi au kuajiri walinzi wanaoeleweka makazi yao yapo wapi n.k n.k

    Mdau
    Ngorongoro.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2010

    sisi ni bin adamu . napenda kusema kuwa hakuna aliyekamilika ila muumba wa mbigu na ardhi. sasa mmmoja wa masai akiiba ndiyo wote??. wafanya kazi ya ulinzi wengi ni wezi .iliyobaki ni wewe mwenye mali ulinde mali yako . chunga mali yako mwenyewe. na ikiwa mali ya kanisa. basi haijapotea imerudi kwa wenyewe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2010

    Mwana FA kaimba usije mjini,wamasai walishaiba deal yao makonde.Mchungaji mwajiri Mmakonde wao waaminifu sana hata kama ukiwa unamcheleweshea mshahara utamkuta tu.
    By the way pole.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2010

    namna gani michuzi mbona hili jambo halija fikishwa polisi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2010

    mchungaji chunga ulimi wako . hiyo nakupa nasiha. sababu umeandika kabla ya kutamka . lakini itabidi uwwe na walinzi zaidi ili wakuchunge na kutaja makabila. kama uliwahi kusikia kashfa ya wachungaji na papa hawakutaja mak....abila wamesema makosa ya wachungaji wa makanisa .

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2010

    walinzi wa kimasai walikuwa wakiaminika sana kwakuwa hawana tabia za udokozi lkn sasa hivi wameingia kwenye lile kundi la watanzania. hata mimi nyumbani tulikuwa nao lkn sasa hivi tunaweka walinzi wakawaida kwasababu hawana tena tofauti na wengine, pia wakati wa usiku walikuwa wanaiba mbuzi wa watu wanachinja usiku huo huo na kula nyama hlf lawama zinakuja kwetu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2010

    Mchungaji acha kuhukumu watu usije ukahukumiwa. Wewe unavyosema sio sahihi kabisa kutumia group la kabila la watu. Ina maana ulikua humjui huyo mtu jina lake? Unasema wamasai unajuaje ni wote au kwa vile huyo alikua mmasai basi umewachanganaya wote..

    Najua inauma sana ukiibiwa lakini try to be reasonable and act professional unapopost vitu kwenye public forums

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    Tesa na mbwa tu, ni watiifu, waaminifu, wapambanaji yakinifu,na wana akili. Vile vile wanathamini hata kuliko mke.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2010

    MIMI NI MMASAI NA NIKO OSLO NASOMA. NIMECHUKIA SANA WEWE MCHUNGAJI KUSEMA WAMASAI WOTE NI WEZI. NAFURAHI NIMEKUFAHAMU KUWA WEWE SI MCHUNGAJI BALI UMEFUATA AJIRA TU NA FUNGU LA KUMI. KUSEMA WAMASAI NI WEZI INAMAANA SASA HATA SISI WAUMINI WA KIMASAI HUTATUPOKEA KANISANI KWAKO? WACHUNGAJI NENDENI SHULE, MJUE NAMNA YA KUONGEA SI KUKURUPUKA TU NA KUONGEA ETI KWA VILE MNAHESHIMIKA. TUTAWAHESHIMU KWA JINSI MNAVYOONGEA LAKINI ULIVYOONGEA UMEKOSEA NA OMBA MSAMAHA KWA MUNGU NA MTAFUTE HUYO MTU ALIYEKUIBIA

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2010

    Wanajua kila kitu Ulinzi, kusuka nywele, uganga.........na baadhi yao sio waaminifu(wezi).

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2010

    MBONA WAMASAI MMEKUJA JUU NAKUONGELEA ISSUE YA UKABILA MLIPO MALIZA MBONA HAMJACHANGIA CHOCHOTE KUHUSU HUU WIZI INAONEKANA NIASILI YENU KUFUGANA. MAANA KWELI MMEMUONYA MCHUNGAJE THEN, MLIKUWA MCHANGIE KUHUSU HILI LILILOTOKEA LAKINI KIMYA. MBONA IKIONGELEWA ISSUE YA WASUKUMA WACHAWI WANAUWA ALBINO, WAKURIYA WANAMALIZANA KWAKUCHINJANA KWA NG'OMBE MBONA HAMINGILI NA KUSEMA NI UBAGUZI LEO YAPO KWENU KINAWAUMA POLEELLLEEENI

    MDAU MPENDA HAKI

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2010

    Pole sana ninyi nyoooote mlio guswa na tahadhari hii LAKINI NI KWELI KABISAAA WAMASAI WALINZI WAMEKUWA WEZI/WAIZI KUPITA KIASI. JUZI TU NIMEIBIWA MATAIRI MANNE MAPYA NDO NILITOKA KUYACHUKUA TAYARI KWA KUVALISHA GARI LANGU HAYOOOO YAKAONDOKA NA AKWII/MZLINZI AKAKIMBIA SASA LEO NI SIKU YA 5!! POLICE WANATAARIFA HIYO. ukweli upo pale paleeee...Asante

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2010

    Acheni kumzingua mchungaji, kasema mmasai ili watu waweze kuelewa kwa urahisi kwa sababu ndio hasa wanaojishughulisha na shughuli za ulinzi binafsi, yani makubalinao ni baina yako na yeye sio kampuni.

    Pia kaamua kutaja kabila kwa vile watu wengi walikuwa wakiwasifu kwa kuwataja kabila haswa kwamba "Wamasai ndio walinzi bora na waaminifu."

    Sasa basi mbona hapo walipokuwa wakisifiwa mlikuwa hamlalamiki namna hii.

    MCHUNGAJI WASIKUBABAISHE, HAO WOTE WANAOSEMA UMEKOSEA KUTAJA WAMASAI SI WAKRISTO, KWA MAANA HIYO BASI WANA SABABU ZAO BINAFSI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2010

    Huyo mchungaji naye kaishiwa, sadaka zinakwenda wapi?? kwa nini msiajiri walinzi wa makampuni binafsi??? acha muibiwe!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2010

    MChungaji naona umechapia kwa taarifa uliyoitoa, kwanini mnamwajiri mtu kufanya kazi hasa ya ulinzi wakati hamjui historia yake ya kazi ya nyuma. Na kwanini walinzi wawe wamasai tu kwani hakuna walinzi wa aina nyingine tofauti na wamasai? Mtakuwa mlichemsha kumwajiri mtu na kumwamini kiasi hicho wakati hamkufanya background check na kupata references angalau za watu wanaojulikana hapo mjini! Ndo kujifunza kutokana na makosa inatakiwa ujue mtu ametokea wapi na anaishi wapi ili akitokomea kama hivyo unajua wapi pa kuanzia kumsaka.
    Next time muwe makini.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 20, 2010

    Muulize huyo Mchungaji huyo mlinzi wake alikuwa anavaa nguo rangi gani unajua watu wanachanganya sana haya makabila Mkwere na Mmasai...Mdau USA

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 20, 2010

    POLE SANA MCHUNGAJI KWA TUKIO HILI. LAKINI UNGEKUWA UNAELEWA WAMASAI SI WATU WA KUFANYA ULINZI WA AINA YOYOTE.
    NENDA KITUO CHA POLISI CHOCHOTE NA UTAAMBIWA HAWA WATU NI-PERSONS OF NO FIXED ABODE.
    KIFUPI HAWANA ADDRESS YA NYUMBANI KWAO-NI WAZURURAJI.
    SISI TULIIBIWA HAPA MIKOCHENI NA POLISI WALITUSHAURI KUACHA KABISA KUWEKA WALINZI WA KIMASAI, NA HII NI BAADA YA WAO POLISI KUPELEKEWA MATUKIO MENGI SANA YA AINA HIYO

    PILI UNGEKUWA NA PICHA UNGEIFLASH HAPA MTANDAONI KABLA MWINGINE HAJA CHAPWA.
    MWISHO AINGIAE KATIKA KANISA LA BWANA NA KUIBA MWISHO WAKE SI MZURI, LAZIMA UTASIKIA MSUBA WA HUYO MMASAI HIVI KARIBUNI

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 20, 2010

    waswahili bwana!!! yaani mtu kajitolea kutuonya mnaanza kulalamika mara ukristo, mara ubaguzi. Acheni hizo, wengine mko nje na wengine hamna hata mali ya kuibiwa. WAMASAI WENGI WA SASA NI WEZI WAKUBWA na walinzi FEKI. Nenda kituo cha polisi uulize na uambiwe. Sisemi wote ni wezi bali namba inakua na tunawaajiri kwa imani kuwa WAMASAI WOTE ni waaminifu kumbe majambazi maana wengine wasuka na dili na majambazi halafu wanafichiana siri. Shame on you!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 20, 2010

    As mchungaji, you yourself you sin against God for profilling a person, do you really have to mentioned the tribe of the person(Mmasai)? for this I dont have any sympathy with you.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 20, 2010

    We unayejiita mchungaji, wacha upumbavu wako wa kuwatukana jamii nzima kwa kosa la mtu mmoja au watu wachache. Wamasai wamekuwa wakiajiriwa kuwa walinzi kwa ajili ya ushujaa na uaminifu wao. Hao wachache waliopotoka ni kuwa sasa wameanza kuchukua tabia ya Watanzania wengine. Kama kweli wewe ni mchungaji wa kanisa nawaonea huruma wafuasi wako. Huna akili. Halafu wewe anon wa 20 May 06:16:00 a.m. Nieleza wapi katika biblia imeandikwa kuwa mtu mmoja akitenda kosa basi jamii yake nzima itahukumiwa. Wewe na huyo mchungaji wako si wakristo.... Nyinyi ni makaburu tu!!! WaTanzania wenzangu, tuupige vita ukabila bila huruma. Tukiwachia ukabila usambae utatumaliza kama Rwanda, Burundi na Kenya.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 20, 2010

    Mchangiaji wa 20 May 06:16:00 una akili sana! kwa sababu naona wengine wanalopoka tuuuu hawajui hata wanachokiandika, watu wanalazishwa kufuta ukabila? Huyu jamaa kama ni mmasai mchungaji aseme ni mmakonde au mkara? au aseme mtanzania wakati tukio limetokea Tanzania? Watu wanatakiwa waelewe kwanza kabla ya kuandika! Makabila ya watu yapo na wala huwezi kuyafuta. Kama wewe unaona aibu kuwa kabila lako shauri yako.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 20, 2010

    mimi hata sioni kosa kwa mchungaji kusema masai mlinzi, mlitaka aseme nini ? mtanzania mlinzi ? hata haijaelekea , hata vyombo vya habari wakitoa taarifa ya uhalifu wanataja na makabila ya wahalifu umri wao na hata wanapotokea , sasa tatizo liko wapi ? mnakuwa kama hamjaenda shule jamani !! alivotaja masai haimaanishi ni wote ila kataka mjue aliyemuibia ni kabila gani,ni kweli asilimia kubwa ya wamasi sasa ni wezi na sio wote .. mimi nishaibiwa na masai lakini aliiba kitu cha kipuuzi kwake aliona cha maana.. ni bora kufuga mbwa , kuliko kuweka mlinzi wa aina yoyote ....masai wala mzungu

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 20, 2010

    Wewe anon wa 06:16 na huyo mwenzako wa 11:53 na mchungaji wenu feki wote hamna akili. Mimi ni mchaga na nakubali identity yangu, lakini sikubali kabisa ukabila na kutukana kabila zima kwa ajili ya makosa ya watu wachache. Bahati nzuri kwa Tanzania watanzania tulio wengi tunajua kuwa watu kama nyinyi ni sumu kwa taifa letu na tutawashinda!!! Kitu ninachokionea aibu ni kuwa mtu anayejiita mchungaji anweza kuandika utumbo kama hou. Kwa maoni yangu, huyo si mtumishi wa Mungu bali ni mfuasi wa lucifer.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 20, 2010

    Jamani Kama unalipenda kabila lako basi jiepushe na tabia mbaya. Wewe unawakilisha kabila lako. Ndiyo maana ukisema kabila linalopenda pesa wote mnajua ni kabila gani bila hata kulitaja. Maana yake nini? Tabia unazozifanya zinahusishwa na kabila lako. Penda usipende.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 20, 2010

    Ninawashangaa Watanzania yaani mchungaji kajitolea kutoa tahadhari ili wengine wasirudie makosa na kuibiwa lakini watu wanamwacha mwizi na kumshambulia mchungaji ambaye ameibiwa. Sasa mfuasi wa lucifer si hao wanaotetea wezi na mafisadi. Ndiyo maana mafisadi wanaimaliza nchi na hakuna wa kukemea.

    Mchungaji umefanya kazi nzuri Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 20, 2010

    Kazi gani aliyo fanya so called mchungaji? kwanini asinge andika jina la huyo aliye muibia tu bila kuhusisha kabila lake? kwahiyo unataka kusema wale changu doa wote pale Dar ni wahaya, au wezi wote wa tanzania ni wachaga? au kubwa zaidi wanao ua Albino wote ni wsukuma? unainoje hii? tuwe wa aangalifu tunapo andika kashafa..

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 20, 2010

    Watu wengine bwana et mimi mmasai,kama wewe mmasai so what?, ulitaka mchungaji asiseme kwa kile kilichotokea, pale kanisani, na mlinzi alikua jamii ya kimasai na walimwamini, kama mwenzao na ni mfanya kazi wao, lakini matokeo kaiba na kutimka, unazani hiyo ni khaki kweli, anawatadhalisha na watu wengine wasijisahau na kuzani wamasai waminifu kwa kuwa ndio wanaopata ajila ya ulinzi kwa uraisi.Hapa sio mimi fulani.Hapa ni tatizo. Tatizo ni wizi.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 20, 2010

    Jamani ebu tuambiane ukweli, hivi sio kweli kwamba WAMASAI wanajulikana zaidi kwa kabila lao? Mbona wale wanaosuka tunawaita Wamasai hamsemi, mbona tuwaita wafanya biashara ndogondogo wamachinga, hamlalamiki? Bwana acheni kashfa na matusi kwa mchungaji humu. Yeye ametumia jina maarufu linalojulikana kwa wote na wala sio ukabila! Huyo mwingine anayesema yeye ni mmasai anasoma Oslo na anamwambia mchungaji akasome, namwambia hivi hata akisoma vipi haitambadilisha yeye kuitwa Mmasai, kwanza iwe Oslo na hata huku Ulaya kwenyewe wanawatambua wamasai kwa kabisa na wala sio Utanzania! Wamasai wanajulikana hivyo uende popote duniani na wengi wapo proud na hilo. Inapotokea mmefanya ualifu hamtaki kuitwa Wamasai, why?

    Mtumishi wa Mungu, pole kwa kuibiwa, tena kanisani. Lakini inabidi kuwa makini next time, msimuajiri mtu bila kuwa na details zake zote, hata sio tu kwa walinzi ni kwa mtu yeyote mnaemuajiri kufanya kazi yoyote ile ni vyema kupata information zake zote mapema.

    Tuendelee kuelimishana jamani na wengine humu acheni lugha za matusi. Hivi michuzi kwa nini unatoa hewani comments za watu wanaotumia lugha chafu kwa wenzao? please, ziweke kapuni ili wajifunze lugha inayokubalika. Hivi hizo lugha ungesikia unaambiwa wewe ungevumilia kweli? Jirekebisheni bwana, acheni jazba zisizo na msingi.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 20, 2010

    me sioni kosa la mchungaji liko wapi.yani kwa kuwa kadokeza suala la wizi ndo mumkalie kooni hivyo?
    mbona kipindi watu wanamwagasifa kemkem juu ya umahili wa walinzi wa kimasai hamkujitokeza kupinga kutajwa kwa kabila.
    acheni upuuzi,wamasai wanajulikana kwa kutaja kabila kutokana na mavazi na wala sio majina yao hivyo kama kuna makabila mengine wanavaa kimasai ili kupata kazi za ulinzi ilo ni jukumu lenu wamasai kupambana nao wasiwachafulie kabila.

    ReplyDelete
  31. Baba UbayaMay 20, 2010

    mchungaji katoa tu tahadhari kuwa makini na walinzi wa kimasai.sasa kama wewe ni mmasai na tena sio mlinzi unalialia nini sasa?ni rahisi kutaja kabila kuliko jina la mtu.na hiyo haimaanishi kuwa wote ni wadokozi.
    ni sawa na kutoa tahadhari ya kusema "tuwe makini na machinga wa Kichina,ama kuwa makini na vijana wa mtaa fulani".ingawa si wote wenye mambo hayo ya kupewa tahadhari.
    acheni kuleta siasa zenu.

    ReplyDelete
  32. MmachingaMay 20, 2010

    hahaha wamasai wamekuja juu kisa suala la wizi.mchungaji angetoa sifa za kumwaga kwa kusema "Wamasai ni Walinzi Waaminifu sana" ina maana mngemjia juu na kusema asitumie ukabila?ktk shughuli kadhaa,ni rahisi kutaja kabila kuliko jina sababu wengi wa wahusika wa kabila hilo hujulikana zaidi kwa kupitia ukabila kuliko majina yao.
    mbona MR. EBBO anawapaisha ktk bongo flava na hamji juu?
    na kama wewe si mlinzi wa kimasai ina kuuma nini?mchungaji kasema "walinzi wa kimasai" na si vinginevyo.
    suala ni kuwaonya hao walinzi wa kimasai kuacha kuchafua jina la jamii nzima ya kimasai.kama unamjua mlinzi yeyote wa kimasai basi pitisha ujumbe kwake naye atapeleka kwa mwingine.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 21, 2010

    We Mmasai mwizi mpeleke O.K PLAST, atakutana na NGIDA kule ataacha wizi, sijui bado yupo?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...