Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mh. Omary Ayoub Juma akiongea na wanahabari leo kwenye ofisi za ILO jijini Dar ambapo alitoa tamko la Kamati ya Utendaji ya TUCTA kuhusu mgomo shinikizi wa wafanyakazi nchi nzima (protest action). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Mh. Nicholas Ernest Mgaya
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mh. Omary Ayoub Juma akiongea na wanahabari leo kwenye ofisi za ILO jijini Dar ambapo alitoa tamko la Kamati ya Utendaji ya TUCTA kuhusu mgomo shinikizi wa wafanyakazi nchi nzima (protest action). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Mh. Nicholas Ernest Mgaya

Kumbe Mgaya sio Raisi wa TUCTA. Mbona JK alimbebea Bango?
ReplyDeleteWana wa Mungu kuweni Macho. Tunatafutwa kila upande. Mara tuwafutie misamaha ya kodi, mara tuwanyanganye madaraka tugawane sisi. Wana wa Mungu angalieni msije mkaumizwa. Maana huyu bwana kapania.
Ndugu zangu naomba niangalie na upande wa pili. Ukimsikiliza JK alitoa point muhimu tu katika hotuba yake. Pato la serikali halitoshelezi kuwalipa wafanyakazi mshahara wanaotaka wao.
ReplyDeleteTatizo ni kwamba awamu hii ya nne. Wafanyakazi wanavunjwa moyo na ufisadi wa viongozi. Wao wanaishi maisha mazuri na ya starehe. Wakati wafanyakazi wanaishi kwa taabu. Ingekuwa vizuri JK akaonyesha ukali dhidi ya mafisadi na wala rushwa. Hii ingewafanya wafanyakazi wajisikie kuwa serikali iko upande wao. Wakati wa Nyerere maisha yalikuwa magumu sana wala huwezi kulinganisha na sasa. Tofauti ilikuwa ni kwamba wote tulikuwa tunaishi maisha ya kuteseka pamoja. Sasa iweje wateseke wafanyakazi tu wakati wanapishana na ma
Range Rover ya mafisadi viongozi kila kona. Mengi alijaribu kukemea naye akatishwa. Sheria ikiwa msumeno hakuna atakayelalamika. Kama ni mateso tuteseke wote na kama ni kula tule sote.
Ankal utakubaliana nami tangu blogu hii imeanzishwa, maada hii ya Tucta a.k.a Mgaya imechangiwa ipasavyo na wachangiaji wote wapo mwelekeo mmoja(wanaongea lugha moja) naomba usizitoe madaa hizo hapo chini mpk mwisho wa wiki hii. Na mwisho wa mwaka uje utoe tathmini ni maada ipi imepata comments nyingi kushinda hii.
ReplyDeletePia hata comments zilizopo kwenye magazeti mengi ya leo pamoja na blogu za Tz zimemponda sana mwajiri mkuu bila kujali waliompa huo uajiri mkuu!
Ni mtazamo tu.
La kunifanya hamna-JK
Kauli ya JK rais wa Tanzania kwa wafanyakazi; ni ya kutia aibu na isiyotegemewa kutamkwa na kiongozi wa nchi inayofuata misingi ya haki na utawala bora.Kutamka kutumika kwa silaha za moto kuzuia mgomo wa watumishi(raia)ambao wanadai haki yao ya msingi;huko ni kulewa madaraka.Rais anataka kuuwa raia wake kwa sababu ya kudai haki,hili sijambo jema na ni dalili mbaya kwa hatima ya nchi yetu.Wafanyakazi wa Tanzania wataendelea kunyanyaswa hadi lini!! Pato la nchi hata kama ni dogo kama lingegawanywa kwa haki kwa wote maisha yasingekuwa kama yalivyo sasa.Mbunge analipwa posho ya siku moja iliyokubwa kuliko kima cha chini cha mwezi mzima cha mfanyakazi; jamani haki iko wapi hapa.Rais kila leo yuko ziarani nje ya nchi;gharama zake za ziara hizo ni mishahara ya walimu wote kwa mwaka.Sasa anapotumia lugha ya kwamba pato la nchi ni dogo hivyo wafanyakazi waendelee kuteseka; huo ufanisi wa kazi utatoka wapi; kazi inafanywa na wenye njaa.Rais alitakiwa kuwa mwenye huruma kwa watumishi wake,badala ya kutoa vitisho; hivi hajui mgomo uko ndani ya moyo wa mtu, hata ukimsimamia kwa bunduki kazi atakayo fanya itakuwa haina ufanisi wa kweli.Na huyo anayebeba bunduki naye ana njaa vilevile.Rais akumbuke kuwa hata punda ukimlazimisha hufikia mahali akataa kwenda hata kama utamchapa mijeledi kiasi gani.Rais inabidi waombe msamaha wafanyakazi kwani kwa kauli yako hujawatendea haki.
ReplyDeleteTuktam mmemsikia wenyewe kuwa JK hana haja na kura zenu. Amesema kuwa kura ni chache mno, yaani kura zenu laki tatu na ushehe hazimtishi.. yeye anathamini kura za wazee za wazee wa Dar waliompigia makofi na za wale watanzania mamilioni 39, sasa mnamwambia nini mtu huyo? Hivyo basi tunawakaribisheni Chadema Tukta wote kwani CCM hawana haja na nyie. karibunijamani Chadema ili tujenge nchi yetu, baadaye mishahara kibao!!
ReplyDeleteMdau wa Khonda, Moro
Nyie kina Michuzi na Blog hii si wafanyakazi? au mnalipwa tofauti na wengine? Mei Mosi hamkuionyesha hapa kabisa.
ReplyDeleteLa kusitisha mgomo ni busara kwa TUCTA na ni kukosa busara kwa JK. Sijaona tofauti ya Makamba na JK. Rais asingekuwa na wasemaji kama alivyo Makamba tungekwisha sikia ugolo kama huu na tungekuwa tumeshazoea. Masikini Tanzania!
Tanzania inatia huruma, kama viongozi wenyewe ndo hivyo si mchezo...
ReplyDeleteHuku ndo nimefika sirudi ng'o bongoland labda kusalimia.
mdau, USA....
Mdau wa 2 kutoka comment yangu big up...u wrote sense.
wafanye mgomo silence..Kila mmoja ana call sick siku hiyo.
ReplyDeleteSerikali haina hela za kulipa watu lakini inazo za kulipa mafisadi na kununua magari mazuri
Yale yale ya miaka ya 90 wanafunzi chuo kikuuu walipogoma. Waliitwa wazee wa Dar na kuambiwa wanafunzi wanadai pesa za sigara wakati KCC (Kima cha chini) kilikuwa 9,000!!!! Si makofi hayo na wanafunzi kuonekana maharamia. Hawa wanaoitwa wazee wa Dar ni kundi gani hili? Ni vema Raisi angekutana na wafanyakazi wahusika na kuongea nao na baadaye kuruhusu maswali. Hivi wale wazee waliuliza maswali? Na kati yao kulikuwa na wafanyakazi wangapi? Hiyo ni kutafuta mob saikolojic support.
ReplyDeleteIli tuendelee tunahitaji vitu vinne - Watu, Ardhi, siasa safi na uongozi bora.
Watu - wapo (lakini mafisadi pia yamo); ardhi - bwerereeee, siasa - mmmmh! Uongozi bora - ?/bora uongozi?
sisi walimu tutakuwa tukifika madarasani, hatufundishi wala hatushughuliki na mtoto wa mtu, aelewe asielewe shauri yake;serikali ya kijinga hii...sisi ndio tunaowafundisha watoto wa hao wazee wa dsm;sasa cha moto watakiona..tunawapiga shalow shalow tu..wanamaliza shule hawajui kusoma wala kuandika..kwani wazazi wao ni wapumbavu!!
ReplyDeleteLeo Serikalini kuna roll call..ole wake asiyefika...
ReplyDeleteTunarudi palepale...kama enzi zileeee za vidudu! Mie nishafika tangu saa kumi na moja alfajiri. Nani anayependa marungu? Thubutu! Hata hizo mwananyamala Hosptal zao nitapata ARVs au Mseto za kutibu hiyo minundu?
Jamani...akili zenu zifunguke..Watanzania tumelishwa moshi wa mwenge...hii ndo product yake.
Na bado...
MAFANIKIO YA TUCTA YATATOKANA NA NGUVU ZA WANACHAMA NA SI VIONGOZI PEKEE,VIONGOZI NI WAHAMASISHAJI TU HIVYO KUSHINDWA KWA MGOMO UNATOKANA NA WANACHAMA KUTOJALI MASLAHI YAO STAHILI NA TUSIWALAUMU VIONGOZI, WANACHAMA TUMEWASALITI KWA KUOGOPA KUDAI HAKI ZETU ZA MSINGI NA HASA KUBWA YA KUTOZWA KODI ZAIDI YA VIWANGO VYA WAFANYABIASHARA! PAMOJA NA MIFUKO YETU YA JAMII KUWANUFAISHA ZAIDI WASIOCHANGIA NA SISI KUTUMIWA KAMA NG'OMBE WA MAZIWA.
ReplyDeleteTangu juzi, mpaka jana na usiku wote huu, nilikuwa najaribu kukusanya fikra zangu juu ya mheshimiwa RAIS wetu na hotuba yake kwa wazee wa Dar, sipati jawabu kabisa. Kwa kadri ninavyopima mamlaka na nafasi ya mheshimiwa Rais na kauli zile, sipati jawabu. Kwanza siamini kabisa kama kweli kauli zile alikuwa anasema mwenyewe au mbadala. Na NAAMINI KABISA KUWA KAMA AMERIWAINDI MKANDA KUJISIKILIZA MWENYEWE JINSI ALIVYOKUWA ANASEMA, NAAMINI KABISAAA, ANASIKITIKA. UNAJUWA, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, MIMI NAAMINI KUWA, DHAMIRA INAKUSUTA KAMA HUTENDI HAKI. YAANI HATA MWIZI AKISHAMALIZA KUIBA ANAFIKIA MAHALI YEYE MWENYEWE ANAJUTA KWA NINI ANAIBA. LAKINI YOTE HUISHA PALE MSHITAKI WETU IBILISI ANAPOPANDIKIZA MAWAZO YA KUPOTOSHA NA KUKUAMBIA KUWA UMEFANYA VEMA ENDELEA; NA NDIYO MAANA MWIZI ANARUDI TENA MZIGONI KUIBA MARA NYINGINE.
ReplyDeleteSikiliza kauli hii "kama mnaona mshahara hautoshi acheni kazi" na "kura zenu pia msinipe" Looh, mheshimiwa umefikia huko. Kuelezwa na wanao kuwa Baba kiasi cha chakula kinachopikwa hapa nyumbani hakitoshelezi, tunaomba ongeza kipimo, halafu unawaambia wanao kama hamshibi basi ondokeni acheni kula!!! Wakati huo huo wapo watoto wawili unawapa chakula kingi tena mpaka wanasaza. Hii ni busara kweli kwa mzazi.
Yoote tisa, kumi ni kwamba, MHESHIMIWA, SI WEWE ULIZUNGUKA MIKOA YOTE TZ KUTUOMBA KURA NA KUTUAHIDI MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA? Leo wafanyakazi kama miongoni mwa watanzania uliowaadihi maisha bora wakikukumbusha juu ya kuwatekelezea maisha bora, unawamenyea, unawatisha, na kuhamasisha kabisa vyombo vyako vya dola hata kutumia silaha za moto!!!! {Hongereni ninyi wafanyakazi wa dola maana maisha yenu ni bora, yameboreshwa).
"WAFANYAKAZI WA SERIKALI, MIMI NDIYO MWAJIRI MKUU" Kauli hii inakinzana na ahadi ya maisha bora, kwa hiyo hata kama ndani ya nyumba hatushibi tusikueleze? Kauli hii ni ya kidikteta, maana yake ni kwamba, MIMI NDIYE MWENYE MAMLAKA, MUTANIFANYA NINI?
Mimi naamini kabisa kauli nyingine wala hazikuwepo kwenye mpango wa hotuba ya mheshimiwa kwa wazee, ila naamini ilitokana munkari wa vifijo na huree za mabimkubwa na wazee aliokuwa anawahutubia. Hili ndilo kosa alilolifanya mheshiwa, kuwahutubia watu wasiohusika na mada. Waache washangilie, inawahusu nini? Wao wamealikwa na mheshimiwa, kuonyesha kuheshimu mwaliko basi ilibidi wamshangilie.
Hotuba yooote, ni kwa Mgaya tu, maskini Mgaya. Lakini usivunjike moyo, wewe ni mwakilishi wa wawafanyakazi tu ulipaswa kutajwa.
HATA KAMA IKIBIDI KULA NYASI TUTAKULA, LAKINI RADA ITANUNULIWA, HATA KAMA TUTAKULA UDONGO, MA-VX TUTANUNUA. HATA KAMA IKIBIDI WATU WAFE NJAA, WABUNGE TUTAWAPANDISHIA MISHAHARA TU KMWA KADRI WAONAVYO WAO INAWATOSHA. HATA KAMA IKIBIDI NCHI KUUZWA, TUTSAFIRI NJE TU. LAKINI WAFANAYAKAZI HATUTWAPANDISHIA MISHAHARA, HATUNA UWEZO HUO, HATUNA PESA, SIWADANGANYI.
HITIMISHO, ole wenu mugome, nitawafukuza kazi wooote, wapo watu weeengi wanasubiri nafasi hizo.
EEH EEH, NAOGOPA KAULI HIZI!!! HUU SII UDIKTETA. Naomba msaada.
WAPENDWA WAFANYAKAZI WOTE TANZANIA, POLENI KWA KAULI MBAYA NA ZA KUSIKITISHA ZILIZOTOLEWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TZ.
ReplyDeleteMIMI SIKUWA NA MPANGO KABISA KATIKA MGOMO HUU, LAKINI KAULI ZAKE RAIS NDIZO ZIMENICHOCHEA NAMI NIANZE KUJIONA NAUSIKA JAPO MWAJIRI WANGU SIO SERIKALI.
MHESHIMIWA RAIS NAOMBA NIKUKUMBUSHE KIDOGO MAANDIKO MWANZO 8:22"MUDA NCHI IDUMUPO, MAJIRA YA KUPANDA, NA MAVUNO WAKATI WA KASKAZI NA WAKATI WA KUSI, MCHANA NA USIKU HAVITAKOMA"
HUU NI WAKATI MUHAFAKA WA SERIKALI YA CCM KUVUNA WALICHOPANDA. SIKUZOTE MJINGA AKIELEVUKA, MWELEVU UWA MASHAKANI.
UNADILIKI KUTUAMBIA KUWA HUNA SHIDA YA KURA ZETU? HIVI UNAJUA KWAMBA HAO WAZEE WA DAR NI WAZAZI WETU,SHANGAZI, WAJOMBA,NK?
SIKUZOTE UKIWA KIONGOZI JARIBU KUONGEA BILA JAZBA, YAANI MHESHIMIWA UMEHARIBU KABISAAAAA. WATOTO WA MTAANI WANASEMA UMELIKOLOGA LAZIMA ULINYWE.
MGAYA NA WENGINE WOTE MSIOGOPE WAFANYA KAZI WOTE WA TANZANIA TUKO NYUMA YENU, ENOUGH IS ENOUGH
SLOGAN "TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"
ONGERA MGAYA. UMEKUWA KIONGOZI MAARUFU WA WAFANYAKAZI TANZANIA SASA. NA UMEONEKANA KUWA UNATUMIA BUSARA ZAIDI YA RAIS JK.
ReplyDeleteACHA TU AKUANDAME LAKINI WATANZANIA WENGI SASA WANAJUA KUCHAGUA MCHELE NA MPUMBA.
KAZI HII MLIOIANZISHA VIONGOZI WA TUCTA MSIRUDI NYUMA KAMWE KWANI MNAFANYAKAZI KUFUATA SHERIA WAKATI WAO WANAONGEA TU KWA VITISHO BILA KUJUA SHERIA ZA NCHI AMBAZO WAO WANATAKIWA KUSIMAMIA ZINASEMAJE. NA HII NI HATARI SANA KWA TAIFA LETU
Kwenye hili mi bado nasikitishwa na watu wa staili za kina KIBONDE wa clouds. Kwenye alichofanya rahisi hakuna cha kusifiwa kabisaaaaa kwa jinsi huyu jamaa alivyokuwa anaongea kwenye Jahazi jioni ya siku JK alipoongea.
ReplyDeleteSijui amepandikizwa au ni nini. Mtu kama yeye ndio angekuwa mstari wa mbele kueleza kilicho cha kweli na sio kusifia RAIS wa nchi akiwaambia watu wake KURA ZENU SITAKI na kama ni NJAA ZENU MFE NAZO while tunaona MAFISADI wakiendelea kupeta.
RAIS alichofanikiwa kukiongelea ni kipengele kimoja tuu kati ya vipengele ambavyo TUCTA wametaka virekebishwe, vingine hakuviona na kwahilo atakuwa amefanikiwa kuwaonesha watu wengine kuwa TUCTA ni vichaa wakati sio.
MAPUNGUFU:
1. Maelezo ya RAIS ni ya upande
mmoja. 2. Imefanywa kishabiki kama KUSUTANA flani hivi na wale akinamama "wazee wa Dar" waliondoa maana ya "wazee" 3. Rais hajazungumzia vipengele vingine muhimu kama kupunguza PAYE. n.k.
Mwisho KIBONDE abadilike, naona anaaza kulewa sifa au ana kitu anatafuta na anapitia mlango ambao sio kabisaaaaaa.
Kibonde ni mwana CCM. Si unajua mtu ukikosa namna ya kufanikiwa kimaisha inabidi udandie CCM. Kama wanavyofanya wanajumuia za watanzania huko UK na sehemu zingine za ulaya.
ReplyDeleteJamani watanzania wenzangu, naomba tukiri kuwa kuwa bado tuna ombwe la viongozi na wasomi, sababu;
ReplyDelete1. Rais alitakuwa katika hotuba yake aongee na wafanyakazi na watanzania kwa ujumla. badala yake aliongea na Mgaya/ viongozi wa TUCTA. Mbaya zaidi jukwaa lake pia lilijaa wastaafu wasiojua adha wanayopata wafanyakazi wa sasa.
2. Rais alitakiwa kuonyesha mbadala wa kutatua tatizo la madai ya Wafanyakazi ambao shida yao ni kupata kiasi kinachokidhi mahitaji yao ya msingi. Mfano badala ya kuangalia Kiini cha Tatizo ambalo ni MFUMUKO WA BEI uliopelekea hicho kidogowanachopata wafanyakazi kisitoshe. Hapa pia ndipo nawalaumu wasomi wetu wanaomzunguka raisi wetu- Hao washauri wake na wataalam.
3. Rais alionyesha wazi kuwa anachokililia ni Uraisi wa 2010 hata kabla hajatangaza nia ya kugombea. Aliwashutumu akina Mgaya kuwa wana nia nyingine (labada kugombea kiti chake au kuanzisha chama cha siasa kumg'oa), akasahau kuwa ni wazi kuwa wafanyakazi wanakumbana na hali ngumu ya maisha. Siasa ilijitokeza dhahiri alipo tamka wazi kuwa hizo kura zao Laki tatu na nusu za wafanyakazi wasimpe. Akasahau kuwa wafanyakazi wanazo extended families na wategemezi ambao ni mara tano ya idadi aliyo nayo kwenye makaratasi. Je washauri wake hawakuweza kutafakari hilo.
USHAURI
Rais wetu atafuta mbinu ya kudhibiti mfumuko wa bei ili hicho kiasi kidogo anacholipwa mfanyakazi kikidhi mahitaji yake na familia. Suluhu hii haitakuwa kwa mfanyakazi tu bali italeta nafuu kwa maisha ya kila mtanzania.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
hawa tucta waoga kweli au wameogopa kikwete aliposema huyo nani sijui hataonekana tena ameona atauliwa nini? SI WAFANYE KAMA WENZAO HAPA UGIRIKI HAPO TZ BILA KUFA MTU HAKUENDI SIO ZANZIBAR SHWARI SASA SERIKALI YA KUNDE SIJUI MSETO KWA KUWA WATU WALIKUFA LAKINI BARA WAMELALA KWELI...
ReplyDeleteHapa kuna shinikizo la Ikulu nini? Jana niliona comments 56, leo ghafla zimepungua na kuwa 25. Kulikoni?
ReplyDelete