Maandalizi na shughuli za mipango ya kuchagua viongozi wa jumuiya ya watanzania London imekamilika. Uchaguzi utafanyika jumamosi tarehe 05-06-10 kwenye jengo la ubalozi wa Tanzania Uingereza.
Viongozi kumi (10) wa kamati kuu watachaguliwa ili kutuongoza kwa kipindi cha miaka miwili ijayo. Nafasi kumi zitakazokuwa zinawaniwa ni: viongozi watano (5) wakuu (mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu, katibu mwenezi na mweka hazina) pamoja na wajumbe watano ambao kwa pamoja wanaunda kamati kuu.
Taarifa hii na fomu za wagombea zimetumwa kwa wanajumuiya wote wa TA-London kwa njia ya e-mail. Kwa wale ambao hatuna e-mail zao tafadhali tutumie e-mail address yako kwenye address hii: uchaguzi@hotmail.co.uk
Utaratibu wa kugombea ni kama ifuatavyo:
Mtanzania yeyote mwenye sifa za uongozi anaruhusiwa kugombea (soma listi ya sifa za mgombea zilizorodheshwa katika fomu ya mgombea iliyoambatanishwa na taarifa hii kwa wale tulio na email address zao)
Kila anayetarajia kugombea uongozi lazima ajaze fomu ya mgombea (fomu imeambatanishwa na taarifa hii kwa wale tulio na email address zao)
Utaratibu wa kupiga kura ni kama ifuatavyo:
Mtanzania yeyote anayeishi London anaruhusiwa kupiga kura
Mpiga kura lazima awe amelipa kiwango cha chini cha ada ya uanachama yaani paundi 5
Washindi watapatikana kulingana na wingi wa kura (simple majority)
Maelezo zaidi yatatolewa siku hiyo ya uchaguzi.
Sherehe za kuwakabidhi rasmi madaraka viongozi wapya ambazo zilikuwa zifanyike siku hiyo ya uchaguzi zimesogezwa mbele kutokana na ratiba ngumu ya mgeni rasmi na timu yake. Tarehe na utaratibu kamili wa shughuli hii utatangazwa hapo badaye.
Watanzania waishio London tafadhali ni muhimu sana ushiriki katika uchaguzi huu. Viongozi hawa ndio watakaotuongoza kwa kipindi kingine cha miaka miwili.
Tupunguze lawama, tushiriki kwa kugombea na kuwachagua viongozi wenye sifa ili kuiendeleza jumuiya yetu ya London.
Dhumuni: Kuchagua viongozi wa jumuiya ya London
Tarehe: 05-06-10 saa 9 jioni (15pm)
Mahali: Tanzania High Commission
3 Stratford Place W1C 1AS, London.
Wahusika: Watanzania waishio London.
Malipo yote kwa jumuiya ya London kwa sasa tumia account ifuatayo:
Bank ni HSB – 79 Piccadilly, London W1J 8EU
A/C No: 41 22 96 72
Sort Code: 40 05 26.
Malipo yote kwa jumuiya ya London kwa sasa tumia account ifuatayo:
Bank ni HSB – 79 Piccadilly, London W1J 8EU
A/C No: 41 22 96 72
Sort Code: 40 05 26.
Tafadhali hakikisha unaandika jina lako pamoja na kuchukua reference number kwa malipo yoyote utakayofanya. Hii ni kwa ajili ya kumbukumbu za jumuiya na kujua malipo yamelipwa na nani.
HSB ndiyo bank gani tena hiyo au ulikuwa unataka kumaanisha HSBC
ReplyDeleteMimi ninaishi london na ningelipenda mno kujiunga na TA london, jee ni taratibu gani nitumie? jee naweza kuomba kwa njia ya mtandao?
ReplyDeleteAhsante sana.
Mbona kila siku huko London kuna uchaguzi hebu tuambieni niaje? Kila nikisoma humu naona uchaguzi uchaguzi.
ReplyDeleteNilikuwa London hivi karibuni, cha ajabu ni kuwa kuna baa za Waganda, Wakenya, Warundi nk.. na wateja wengi wa hizi baa ni Wa-Tanzania! Je kwanini msiwe na kijiwe chenu?? ili mikutano kama hii ifanyike huko au hampendani?
ReplyDeleteItakuwa ngumu sana kwa umoja Wa-Watanzania kufanikiwa kwani japo mko London, lakini kifkra mko Dar tu...
mdau wa tatu kukujibu suali lako ni kuwa hapa UK kuna jumuia tele zote zinajidai kuwakilisha watanzania, na cha ajabu nyingi zinatanbukika au kujulikana hadi nyumbani (ubalozini).
ReplyDeleteHata mimi nilishindwa kujua tafauti ya jumuia hii inayotangaza uchaguzi hapa na ile ambayo ilifanya uchaguzi hadi michuzi kufika huku.
Ni tatizo hili la jumuia nyingi ndilo linalotufanya watanzania kuwa na umoja dhaifu hapa uk, hakuna kuaminiana na wakati huo huo kuna watu wengu wana uroho wa madaraka na kutaka ufahari.