Robo Fainali ya mashindano ya Kili Taifa Cup yanatarajiwa kutimua vumbi kesho Mei 24, 2010 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam..

Timu nane zilizoingia Robo Fainali ni Singida, Temeke, Mwanza, Arusha, Iringa, Ilala, Lindi na Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa ratiba ya michezo hiyo, mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Singida na Temeke Jumatatu ya Mei 24, 2010 saa 8 alasiri wakati Mwanza itakwaana na Arusha saa 10 jioni siku hiyo hiyo.

Iringa itaumana na Ilala Mei 25, 2010 saa 8 alasiri wakati Lindi itapambana na Kilimanjaro saa 10 ya siku hiyo hiyo.

Mechi ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Jumatano Mei 26, 2010 wakati ile ya pili itafanyika Mei 27 mwaka huu. Timu zitapumzika Ijumaa Mei 28, 2010 tayari kwa ajili ya michezo ya Mei 29, 2010 wakati fainali itakuwa Jumapili Mei 30, 2010.

“Hadi sasa mashindano yamevutia watu wengi kote nchini na bado tunatarajia mvuto zaidi pamoja na kuibuliwa kwa vipaji vingi, kuanzia robo fainali hadi fainali zenyewe,” anasema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Larger, George Kavishe.

Timu zote zinazoshiriki Robo Fainali zimeshakabidhiwa vifaa vyaotayari kwa mashindano.
Mwaka huu bingwa wa Kili Taifa Cup atapokea kitita cha Tsh milioni 35,

mshindi wa pili - 20m, mshindi wa tatu - 10m, mshindi wa nne - 5m, kipa bora - 2m, kocha bora - 2m, refa bora - 2m, mchezaji bora - 2m, timu yenye nidhamu ya hali ya juu - 2m na mfungaji bora - 2m zote kwa hisani ya Kilimanjaro Premium Lager.

Kwa mujibu wa TFF mchezajo bora wa kila mechi atatangazwa baada ya kila mechi na kuzawadiwa Tsh 50,000.

Hii ni mara ya pili kwa Kilimanjaro Premium Lager kufadhili Kombe la Taifa, ila ni mara ya nne mfululizo kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kufanya hivyo. Miaka miwili ya mwanzo ikiwa chini ya bia yake nyingine ya Safari Larger, ambayo ni mojawapo ya bia maarufu za TBL.
Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) huzalisha, kuuza na kusambaza bia safi, vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL ina maslahi ndani ya Tanzania Distilleries Limited, na kampuni zinazohusiana nayo, Mountainside Farms Limited.

Bia za TBL zenye umaarufu zaidi ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Balimi Extra Lager,Eagle Dark, Bia Bingwa, Safari Sparkling Water, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Castle Lite, Castle Milk Stout, Redds Original, Grand Malt, Miller Genuine Draft na Peroni. Vinywaji vya aina nyingine vinavyohusiana na kundi la TBL ni Konyagi Gin na Amarula Cream.

Kundi la TBL limeorodheshwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na imeajiri karibu watu 1,300 na inawakilishwa kote nchini na viwanda vitatu vya bia, konyagi, malta na depo nane za usambazaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...