Bw. Amatus Liyumba

Na ripota wa Mahakamani
wa Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesho inatarajiwa kusoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba.

Hukumu hiyo dhidi ya kesi ya utumiaji mbaya wa madaraka inayomkabili Liyumba, inatarajiwa kusomwa na jopo la Mahakimu wa mahakama hiyo linaloongozwa na Hakimu Edson Mkasomongwa.

Liyumba ambaye anasota rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu, kesho anatarajia kujua hatima ya kesi yake hiyo.

Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.

Hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.

Upande huo wa mashtaka uliita mahakamani hapo mashahidi 8, wakiwamo waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa BoT, pamoja na kutoa vielelezo mbali mbali vinavyohusiana na kesi hiyo.

Baada ya ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasala ya bilioni 221 baada ya Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa hilo.

Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.

Katika utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.

Baada ya kumaliza usikilizwaji wa ushahidi huo, mahakam hiyo ilizitaka pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria, ambapo alipanga kusoma hukumu dhidi ya Liyumba ifikapo May 24, 2010 ambayo ni kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2010

    FREE Liyumba

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    duuh..kazi ipo!!hiyo kesho...!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2010

    jamni, sijui hiyo kesho itakuwa..lool!!

    ReplyDelete
  4. KalikaliMay 23, 2010

    Michuzi, unabana maoni. Lakini ukweli ni kwamba huu wote ni mchezo wa kuigiza tu. Ni changa la macho tu. ushahidi uliotelewa dhidi ya Liyumba ni wa kumsafisha. Bado serikali haijawa serious na ufisadi. na bado safari ni nedfu sana. Bana tu lakini huo ndo ukweli. Kesho Liyumba will be a free man. Amini usiamini. Wala huhitaji kuwa Jaji kujua hivyo....

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2010

    Hakuna kesi ya kujibu hapo..Ni viini macho na usanii mtupu tu ndugu zangu..Karibu tena uraiani Liyumba tuendelee kutesa..You are free man!..teh teh

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2010

    Wadau wa mambo ya sheria.. kesho Liyumba yuko huru. Kama hakuwa na shitaka la kujibu katika kuitia hasara Serikali??? ni madaraka gani aliyotumia kama mkubwa wako wa kazi alikuwa akikuingilia?????

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    kaka michuzi ni ccm !! mbona unabana comments

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    HUU NI UPUUZI MTUPU NA KUPOTEZEANA MUDA. HIVI KOSA LA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA LIKO KATIKA KIFUNGU GANI CHA SHERIA??! HILO SI KOSA LA KINIDHAMU?! SIJUI MAHAKAMA IMEKUWA INASIKILIZA KESI KWA SHERIA GANI MAANA SIONI KABISA NA WALA HUHITAJI KWENDA SHULE KUONA HAMNA KESI...ILA WAWEZA KUSHANGAA BONGO HII!
    MZAWA

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    Bongo tambarare wajameni!!! RUSHWA KWA KWENDA MBEREEEEEE, HAFUNGWI MTU HAPOOOO...HEHEEEE! KAZI IPO. DUU! WELCOME BACK TO THE SOCIETY MKUU WETU!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    weraweraaaaaaaa liyumba,karibu mtaani tuendelee kula bata,du umesota sana mtu wangu,come back baby!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2010

    mambo ndio hayooooo! ngoma lazima ichomoke leo, huu ndio mchezo wa serikali kujifanya imepitia process zote kumbe ..... haya leo njio leo, mbeleko zenu tu kuselebukaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2010

    MICHUZI ACHA KUBANA COMMENTS KAMA UNAONA HATUNA UHURU WA KUCHANGIA TUPENDAVYO TOA MWONGOZO WA NINI KINARUHUSIWA NA NI KIPI HAKIRUHUSIWI,

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2010

    ToKA LINI MTU MWENYE PESA AKAFUNGWA TANZANIA?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2010

    kesho ndiyo siku liumba atakuwa huru yani hakuna kesi hapo yuko huru kesho kukuche arudi kwake akaenjoy full kiyoyozi in ze house

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...