Video ya mambo yalivyokuwa usiku wa kuamkia leo huko Wiesbaden, Ujerumani
Kushoto ni Bw. Edwin Gafa, kiongozi wa msafara wa Nile Breweries ya Uganda ambao wamepata tuzo ya kushiriki mara nyingi kwenye Monde Selection, Wawakilishi wa kampuni ya TBL ,Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo akiongozana na Mpishi mkuu wa kampuni hiyo (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe. Jioni ya leo Ndovu itanyakua tuzo yake ya Gold Grand Award kwa ubora
Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo (TBL) pamoja na Mpishi mkuu wa kampuni hiyo (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe wakiwa na bidhaa yao ya Ndovu ambayo leo jumatatu usiku itapokea tuzo ya Dhahabu kwenye sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yatazawadiwa.

Mpishi mkuu wa kampuni ya TBL (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe akiangalia vinywaji mbalimbali vilivyopo kwenye sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yalizawadiwa.
Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo (TBL) akiangalia moja ya kinywaji kilichoibuka kwenye ushiriki wa kunyakua tuzo usiku wa kuamkia leo,ambapo hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kurhaus mjini Wiesbaden,chini Ujerumani. Meneja wa kinywaji cha Ndovu Oscar Shelukindo na mpishi mkuu wa TBL Gaudence Joseph Mkolwe wakipeperusha bendera ya Tanzania katika sherehe za Monde Selection ndani ya ukumbi wa Kurhaus jijini Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo
Sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yatazawadiwa
Wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo.
Meneja wa kilaji cha Ndovu Oscar Shelukindo na mpishi mkuu wa TBL Gaudence Joseph Mkolwe wakijiandaa kuingia katika gari maalumu lililokuja kuwapokea katika uwanja wa kimataifa wa Frankfurt, Ujerumani, tayari kupokea tuzo ya dhahabu iliyopewa kilaji cha Ndovu
Oscar na Mzee Mkolwe wakiwa katika jumba la Kurhaus mjini Wiesbaden wikiendi hii ambako sherehe za Monde Selection za kutuza bidhaa bora duniani zinafanyika. Tuzo ya Dhahabu iliyopata kilaji cha Ndovu inatolewa jioni ya leo katika ukumbi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2010

    Huyo Shelukindo haoni kama bendera yetu ipo kichwa chini miguu juu akawambia warekebishe? Kwa wasio jua bendera ya Tanzania rangi kijani huwa juu na bluu huwa chini, mistari hutoka chini kushoto kwenda juu kulia hii ni njia rahisi kuiweka sawa bendera yetu adhim, kuna pia wasiojua hata maneno ya mwimbo wetu wa Taifa tujitahidi kujua jamani
    Balozi/ABUDHABI

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2010

    Mambo ya bendera hayawahusu. walishikizwa tu wao walienda kwa ajili ya shughuli ya kilaji. kama nendera wangetoka nayo huku walipaswa kuelezwa na wataalamu wa bendera jinsi ya kuiweka. Na kama waliikuta huko basi potezea kwa kuwa labda huko wanaijua ki hivyo. Pole sana mwana ABUDHABI. nani niko hukuhuku.
    Kwetu TZ vitu vidogo sana kuviweka sawa huwa issue, sembuse kitu kama bendera! wengine hawana mpango nayo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2010

    next time tubuni basi hata kitu cha maendeleo basi !!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2010

    Bendera ipo sawa rangi ya buluu ipo chini na kijani juu.

    Hongera bia ya Ndovu kunyakua tuzo ya juu duniani.

    Mdau1

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2010

    Nimefurahishwa na jina la mpishi mkuu wa bia (Gaudence Mkolwe), katika kabila langu "mkolwe" humaanisha "mlewe", very appropriate! Ndio maana tuzo imeitika!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2010

    Acheni hizo nyie,hiyo bendera iko sawa,sema imejipindua tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2010

    Michuzi nakushangaa sana umeanza tena ule mchezo ambao baadaye uliamua kulia hapa mwenyewe kwa kuminya comments za watu. Jana nilisema na leo nasema tema na ukiminya nitakusema kwingineko!


    Quote:

    ".... wakijiandaa kuingia katika gari maalumu lililokuja kuwapokea katika uwanja wa kimataifa wa Frankfurt, Ujerumani..."

    Je haya maelezo ni ya lazima. Tujaribu kupembua cha kutundika katika jamii vinginevyo mnaonekana washamba!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2010

    Kutundika bendera yetu ni kitu cha msingi kabisa.

    Hiyo hapo pichani imekosewa!

    Nyeusi ipo: Kusini Magharibi - Kasikazini Mashariki; ni mstatili unakata pembe kwa pembe na kanda nyeusi yenye milia za njano (dhahabu) kando.

    Ikiwa hatujui bendera yetu ikoje, tutajuaje tanzania imekaaje!

    Pembetatu juu ya majani. Pembetatu chini ya buluu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...