Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Mh. William Lukuvi akikabidhi kombe la ubingwa wa Kili Taifa Cup kwa Kapten wa timu ya Singida,Rajab Mohamed huku mfungaji wa magoli mawili kati ya matatu yaliyoizima timu ya Lindi katika mchezo wa leo,Kelvin Charles akishuhudia.wengine ni Rais wa TFF,Reodger Tenga (kulia) na Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. John Chiligati (kulia),Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mh. Parseko Kone (alieshika kombe) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya mkoa wa Singida mara baada ya kupata ubingwa wa Kili Taifa Cup katika mchezo uliomalizika jioni hii dhidi ya Lindi ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imenyakua ubingwa kwa kuichapa mabao 3 - 0 timu ya mkoa wa Lindi.
mshambuliaji wa timu ya Singida,Kelvin Charles akipachika bao la tatu katika mechi iliyochezwa jioni ya leo dhidi ya Lindi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imeshinda 3 - 0 na kuweza kunyakuwa ubingwa wa Kili Taifa Cup. mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Lindi,Omari Matwiko akijaribu kutaka kumtoka kiungo wa timu ya Singida,Rajab Mohamed.


Mkuruenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akibadirisha mawazo na wadau mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali baina ya Singida na Lindi uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imeshinda 3 - 0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2010

    Singida yetu inapaa,tunawapongeza wachezaji na benchi zima la ufundi kwa mkoa wa Singida.Bigup my brother MO.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2010

    So proud of Singida. Singida Hoyee!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2010

    Baaaaaaa, sikupenda mwenzenuuu, imekuwaja jameniii

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2010

    Ushindi wa Singida haukuwa wa kubahatisha hata kidogo. Mashindano ya mkoani kwao yallianzia toka ngazi ya kijiji, tarafa mpaka wakapata timu ya mkoa. Walijipanga sasa imelipa. Hilo ni fundisho kuwa katika soka hakuna mambo ya kubahatisha ila ni kujipanga na maandalizi ya kisawasawa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2010

    Mo kafanya jambo no sweat lindi bado tunayeya mtajibebaaa,warugaruga

    ReplyDelete
  6. Na we Michuzi Sin ya sasa umeanza kuchafua lugha kama mdogo wako DOGO Michuzi Jun ya?

    Sasa "...akibadiRisha mawazo..." ndio nini badala ya "...akibadiLisha mawazo..."

    Tutamuita MzeeKifimboCheza hapa. we haya tu.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Singida kwa kuiweka kanda ya kati katika kumbukumbu za soka, ni imani yangu ile dhana ya kusema mikoa ya Dodoma, Singida,Arusha, Manyara ni ya wakimbiaji wa mbio ndefu tu..sasa itajadiliwa kwa kina.Pia ni imani yangu kuwa wachezaji wote walioshiriki wanachezea vilabu vya ngazi tofauti MKOANI SINGIDA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...